Bunda: Lissu atangaza kubadili Sheria ya madini, kwamba atajayeyagundua kwenye ardhi yake yatakuwa yake

Sahihi kabisa, Ila madini yapo ardhini na mmiliki wa ardhi ni mwananchi na sio Serikali !! ...... ulaghai huu ulianzia kwa wakoloni na kurithishwa kwa mamlaka zetu za juu.

Kusema ardhi ni mali ya wananchi chini ya usimamizi wa Rais huu ni wizi wa kitaasisi tena mchana kweupe ambao unatakiwa kukomeshwa kupitia katiba mpaya.
 
Hakika
 
Anafuata sheria za Marekani, sheria inatakiwa ibaki kama zamani. Chamsingi tu kuwe na equal allocation ya hayo madini kwa watanzania wote. Nchini China wanatumia sheria kama yetu.
Lissu ana idea nzuri sana, juzi nilikuwa na angalia Documentary kuhusu ugunduzi wa Gesi huko Papua New Guinea, wale wenye mashamba kwenye eneo lile walipewa share kwenye mapato ya gesi na royalty na Kampuni ya EXXON.

Sisi hapa tumejifungafunga na masheria ya kiroho mbaya.
 
Rais mtarajiwa
Kipaji cha Lisu ni kuwa MWANAHARAKATI!! Hawezi kuwa Rais!! Tutamfaidi vizuri akibakia mwanaharakati!! Chadema watafute mtu mwingine presidential material!! Lisu aje kuwa mwanasheria mkuu wa Serikali huku akiendeleza uanaharakati wake!!
 
Mhuu hili kidogo lina walakini, kwani sheria inasema ardhi ni mali ya Serikali, ukinunua unapewa possession right tu lakini siyo mali yako. Aisee labda kama ataanza kwa kulibadili hilo.
Sheria haisemi ardhi ni Mali ya serikali boss. Sheria ya ardhi na 4 ya mwaka 1999 inasema ardhi ni yote ni ardhi ya UMMA na imewekwa Kwa rais kama mdhamini. (Trustee
 
Lissu ni mtu makini sana.
 
Wachagga na Walambya na Wasukuma na Waha watanunua ardhi yote hadi milele sasa itakuweje!
 
Kipaji cha Lisu ni kuwa MWANAHARAKATI!! Hawezi kuwa Rais!! Tutamfaidi vizuri akibakia mwanaharakati!! Chadema watafute mtu mwingine presidential material!! Lisu aje kuwa mwanasheria mkuu wa Serikali huku akiendeleza uanaharakati wake!!
Walikuwepo wenye chuki dhidi ya Lissu na sasa hawapo. Na wewe utapita.
 
Lissu kachanganyikiwa. Hicho anachokisema ni ujinga mtupu. Bora hata angesema kwamba madini yakigunduliwa kwenye ardhi yako na wewe unakuwa shareholder wa kampuni itakayochimba uwe unapata mrabaha.
We jamaa hata kama ni uchawa punguza kujiaibisha.

Yaani Ardhi ikiwa na Mawe na michanga ni yako ikiwa ma Dhahabu ni ya ccm😆😆
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…