Tuanzie kudadisi mawasiliano yake ya simu na huyo mdaiwa na pia katika biashara kuna michezo mibovu. Yaani inabidi simu zake line zichunguzwe kwa kina na zile za ndugu zake wa karibu pia. Nina imani mitandao ya simu ikikaa vyema inaweza kabisa kupata namba za simu zilizotumika eneo gari lilikutwa na msafara za kwenda kutupa maiti hiyo. Ila kwa kweli Tanzania sijajua ile amani tuliyoikuta tunazaliwa imekwenda wapi. Ukweli ndiyo maana tunapata alama za mkia kwa matendo ya furaha Tanzania kwa kuwa kila siku mambo na matukio ya kuhuzunisha yamejaa tu. Sisi tuliolelewa kwa imani za dini na kuzishika huwa inatupa shida sana. Ila tunaamini tukisimama katika maombi tunaweza kurejesha tena nchi hii katika amani. Haya yanayotokea leo tulikuwa tunayasikia huko Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya ila si Tanzania kwa hakika.