Bunge: Hali ya Utegemezi Nchini inatisha. Katika Watu 100, watu 87 ni Tegemezi



Tunarud

Mawazo kwa nchi haya hapa mkifuata watu tegemezi kiasi hiki hawatakuwepo

 
Kwamba watu wenye uwezo wa kufanya kazi na Kuzalisha ni 13 tuu ndio wanawalisha watu 87.
Sijawahi kusikia Upuuzi kama huu..., anamaanisha wenye uwezo wa kufanya kazi au walioweza kupatiwa kazi ili wapate ujira kulingana na Ujuzi wao ?

Kuna wauguzi wangapi kitaa hawana kazi ? Kuna waalimu wangapi kitaa hawana kazi wakati bado tuna uhitaji wa wakufunzi ?

Wangapi wanakwenda kulima na mwisho wa siku kukosa masoko ? If anyone ambaye hafanyi kazi yake ni hao so called watunga Sera ambao wapo out of touch....
===============
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imesema watu 87 kati ya 100 ni tegemezi nchini, hivyo kushauri itengwe bajeti ya kufanya utafiti wa mapato na matumizi ya kaya, ili kupata takwimu ya hali ya umaskini.
.
Yaani Kodi za hawa masikini zitumike ili eti kufanya utafiti wakati mambo yapo wide open ? Ukiweka kazi ya kuhitaji watu kumi wanatokea watu elfu 10,000 kutafuta hio ajira ili wapate ujira..., Tatizo lipo hapo wala halihitaji degree kuweza kuliona unless wewe ni kipofu...
 
Tatizo la viongozi mfu wa Tanzania ni kujadili symptoms za tatizo na si tatizo lenyewe
Tatizo la utegemezi na umasikini ni after effects za ukosefu wa ajira na fursa za kiuchumi za kuwawezesha watu kupata kipato cha kujikimu na chenye muendelezo ili kuendesha maisha yao .
Na hii inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mgawanyo mbovu wa cake ya taifa na sera +uongozi mbovu wa kudeal na hili tatizo sugu nchini
 
Kama watu hawana ajira , hawana fursa za masoko ya uhakika kwa bidhaa zao za kilimo , hawana masoko ya uhakika kwa shughuli zao pia wanazifanya kwa dhiki ,hilo ni tatizo ,zaidi ya asilimia 60 ya unaoitwa ujasiriamali kitaa hauna hadhi ya kufaa kuwekwa kwenye ujasiriamali ni shughuli za kufanya ili adife njaa ila si shughuli za kuondoa tatizo la utegemezi na extreme poverty humu nchini
Never
 
 
Hivi hata wabunge wenyewe sini tegemezi pia. Maana ili mtu usiwe tegemezi ni lazima uzalishe zaidi ya kile unacho kichukuwa. Kwa mfano kama unashamed la eka tatu ukalilima na kupanda mazao unayo taka yq kuuza . Baada kuuza ukapiga mahesabu ya gharama za kulimisha kupanda na matuzo ya mazo mpaka kuuza ukakuta gharama ni kubwa kuli hela uliyo ipata baada kuuza . Maana yake shamba lake ni tegemezi kwako. Tukija kwa wabunge na mawaziri wa Tanzania tukahesabu gharama zinazo tumika kuwalipa mishahara na marupurupu kwa kipindi chate cha utumishi wao ukalinganisha michango yao kwa maendeleo ya walipa kodi utakuta wabunge ni tegemezi maana kuwapo kwao na kutokuwepo kwa hakuna faida Bali hasara zaidi kwa walipo kodi.
 
Hawa ni viongozi wapuuzi kabisa!
Wanaongea kama hawana vichwa!
Serikali inakopa pesa Kila kukicha lakini utasikia Wakandarasi hawalipwi na wengi wamefilisika!
Pesa haziwekwi ktk miradi yenye kuzalisha ajira bali ni upigaji tu !
Huyu Mbunge anazungumzia wanaowategemea kwa kuwapiga mizinga kwa kuwa wao ndo wanakula keki ya Taifa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…