Bunge: Hali ya Utegemezi Nchini inatisha. Katika Watu 100, watu 87 ni Tegemezi

Bunge: Hali ya Utegemezi Nchini inatisha. Katika Watu 100, watu 87 ni Tegemezi

Hawa ni viongozi wapuuzi kabisa!
Wanaongea kama hawana vichwa!
Serikali inakopa pesa Kila kukicha lakini utasikia Wakandarasi hawalipwi na wengi wamefilisika!
Pesa haziwekwi ktk miradi yenye kuzalisha ajira bali ni upigaji tu !
Huyu Mbunge anazungumzia wanaowategemea kwa kuwapiga mizinga kwa kuwa wao ndo wanakula keki ya Taifa!
Hakuna mwenye suluhisho wananchi wanalalamika na serikali pia inalalamika
 
Leo umeleta Data muhimu sana.

Hii inathibitisha namna gani jamii yetu ni masikini.
Halafu unakuta anayetegemewa mwenyewe na hao watu naye anaungaunga maisha tu.
Tunapaswa pia kuitoa hii mentality kwa watu wetu kwa watu wote ambao ni above 18.

Tunapaswa kuweka nguvu sana kiasi cha kufikia zero katika kila watu 100.
Ndani ya watu 100 wenye zaidi ya 18yrs kusiwe na tegemezi hata mmoja mikoa yote.
 
November 27, 2024 RIPOTI YA TAKWIMU :

Asilimia ya watoto ni kati ya asilimia 40 hadi 45 na si vinginevyo.

View: https://m.youtube.com/watch?v=y9oF0mu09zQ

Mtakwimu mkuu wa serikali atetea takwimu zilizotolewa na TAMISEMI kuhusu waliojitokeza kujiandikisha katika daftari la mkaazi, lililo maalum kwa ajili ya kuweza kupiga kura November 27, 2024 katika uchaguzi wa viongozi wa mitaa, vijiji na vitongoji

Mtakwimu Mkuu wa NBS Dr. Albina Chuwa amesema taarifa ya Serikali ilionesha kuwa, wananchi waliojiandikisha kushiriki katika uchaguzi huo ni 31,282,331 sawa na asilimia 96.83 ya watu wote wenye umri wa kujiandikisha kwa mwaka 2024.

Dr. Albina Chuwa asema kumekuwepo na upotoshaji baadhi ya ya mitandao ya kijamii tangu kutolewa kwa taarifa hiyo kwa kudai takwimu zilizotolewa kwamba wananchi walioandikishwa hazina uhalisia takwimu ya watu walio jiandikisha na kwamba idadi hiyo ni kubwa ikilinganishwa na idadi ya watu wanaostahili kujiandikisha kupiga kura inayotokana na matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.

“Makadirio haya kwa Tanzania Bara yanakadiriwa kufikia watu milioni 64.2 na kwa Tanzania Zanzibar yanakadiriwa kufikia watu milioni 2.03, kwa makadirio haya, wananchi tunapaswa kufahamu kuwa idadi ya watu kwa mwaka 2024 haiwezi kuwa sawasawa na ile ya mwaka 2022,” amesema.

Dr. Chuwa amesema watu waliokuwa na umri wa miaka 16, 17 na 18 katika Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 hivi sasa wana umri wa miaka 18, 19 na 20 ambao idadi yao ni 3,785,036 waliokidhi kigezo cha umri wa kujiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, mwaka huu kwa kuwa wana vigezo na sifa za kupiga kura.

Amesema idadi ya watu wenye umri wa kupiga kura ni sawa na watu wote ambao mwaka 2022 walikuwa na umri wa miaka 16 na zaidi ama kwa lugha nyingine ni wote ambao ifikapo Novemba 27, mwaka huu, watakuwa wametimiza umri wa miaka 18 au zaidi.

“Kwa hesabu hiyo inatokana na matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, makadirio ya idadi hiyo ya watu wenye umri wa kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambayo ni watu 32,987,579 ni sahihi na ni rasmi kulingana na Kanunuzi za Msingi za Umoja wa Mataifa Kuhusu Takwimu Rasmi na kama ilivyoripotiwa kwenye taarifa ya Serikali kupitia Ofisi ya Rais, TAMISEMI,” alisema.

Dr. Albina Albina amesema kuhusu kiwango cha uandikishaji kwa mikoa, imejitokeza baadhi yake kuwa na asilimia zaidi ya 100 ya watu walioandikishwa na kufafanua kuwa watu wana tabia ya kuhamahama kutoka eneo moja kwenda eneo na kusababisha uandikishaji wa watu wengi zaidi ya matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa baadhi ya mikoa.

“ Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ilihesabu watu kulingana na mahali walipolala usiku wa kuamkia siku ya Sensa yaani Agosti 23, 2022. Kwa hivyo, hili ni jambo la kawaida na linalowezekana kutokea kama ilivyotokea katika mikoa hiyo ya Pwani (asilimia 112.61); Tanga (asilimia 110.82); Mwanza (asilimia 106.58); Dodoma (asilmia 104.19) na Iringa (asilimia 100.54),” alisema.

Amesema idadi kubwa ya watu mkoa wa Pwani inatokana na watu wengi wa Dar es Salaam kuwa na makazi mkoa wa Pwani hasa katika wilaya za Bagamoyo, Kibaha, Kisarawe na Mkuranga. Kwa hiyo ongezeko hilo la watu kwenye maeneo hayo linachangiwa na kuhama kwa watu na si kwa kuandikisha watu waliokosa sifa.

Mikoa yenye asilimia ndogo ya uandikishaji ni ile ambayo chambuzi za kitakwimu zinaonesha ni mikoa yenye uhamaji mkubwa wa watu kwenda katika majiji.

Dk. Albina alitoa takwimu za sensa kwa makundi ya umri na kulingana na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, idadi ya watoto walio na umri chini ya miaka 15 nchini ilikuwa 26,399,989 sawa na asilimia 42.8.

Pia idadi ya watu wenye umri wa kufanya kazi wenye umri miaka 15 hadi 64 walikuwa 33,000,128 sawa na asilimia 53.4 na idadi ya wazee walikuwa 2,341,003 sawa na asilimia 3.8.

Amesema wastani wa watoto chini ya umri wa miaka 15 kuwa ni asilimia 60 hadi 70 ni upotoshaji mkubwa kwani hata viwango vya Afrika, asilimia ya watoto ni kati ya asilimia 40 hadi 45 na si vinginevyo.

“Hizi ndizo takwimu rasmi za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu sura 351 kwa maana hiyo, taarifa iliyotolewa na Serikali ya Idadi ya wananchi waliojiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba, 2024 ni sahihi kwa sababu kiujumla idadi ya watu wote waliojiandikisha nchini haijavuka ile inayotokana na matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022,” amesema

Amesema takwimu hizo hazina mashaka yoyote na kuonya kutopotosha umma kwani ni kosa kisheria kupotosha umma kwa kutumia takwimu rasmi kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu.

Kwa upande wake, Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Tanzania Bara, Spika Mstaafu Anne Makinda aliwataka Watanzania kuacha upotoshaji kwani takwimu zilizopo ni sahihi na zimefuata vigezo vyote.

“Hii ndio taarifa rasmi, takwimu za sensa ndio msingi wa kufanyia kitu kama zisingekuwepo tusingepata asilimia, takwimu za sensa ni mwongozo wa kufanya mambo yote ya maendeleo,” alisema
 
Halafu mnapitisha miswada ya kipumbavu bungeni! Nonsense!
 
Bado inatakiwa ifike ratio ya 1 kwa 99 ili kusudi lifanyike jambo la kimiujiza.😄
Jakaya aliwekeza kukuza middle class Ili waajiri wenzao,magu akakomaa na bwawa,lawiti uchumi, badala ya irrigation schemes zitazoajiri wengi
 
Watu 87 kati ya 100,hawana kitu ni wategemezi mheshimiwa sana anashauri itengwe bajeti(waendelee kula)ili kujua kiwango cha umasikini!!!!

Idara ya takwimu, maendeleo ya jamii,mioango na uchumi,ofisi ya wk sera,wote hao hawajui kiwango cha umasikini!!!!!!

Sawa,tengeni bajeti.
 
Kama hata kinachokusanywa kinapotea na hakuna value for money hata kikikusanywa zaidi bado kitapotea...


Alipe 10 percent ya kitu gani (yaani flat fee au kipato chake ambacho kama hakipo officially basi ni 0) au unamaanisha Kodi ya Kichwa ?
21) Hiyo ya watu kuiba oesa na kula, sheria ya kuuwana tu wanaofanya ufosadi ikipitishwa, ufisadi utakoma.

Nawashangaa wananchi, wana ubavu wa kumuua mpaka kumchoma moto anaewaibia chupi au simu lakini hawana ubavu wa kuchoma moto wanaowaibia mabilioni.

Huo ndiyo ujinga wa Mtanzania.

Hilo la kodi ya flat rate, maana yqke analipia kipato chake. Anatumia nini kama hana kipato? Ni lazima kuna anapozipata.

Hiyo kodi iite vyovyoge utakavyo haijalishi. Iwe ya kichewa, ya miguu, ya kipato, Sito tatizo.
 
Watu 87 kati ya 100,hawana kitu ni wategemezi mheshimiwa sana anashauri itengwe bajeti(waendelee kula)ili kujua kiwango cha umasikini!!!!

Idara ya takwimu, maendeleo ya jamii,mioango na uchumi,ofisi ya wk sera,wote hao hawajui kiwango cha umasikini!!!!!!

Sawa,tengeni bajeti.
Eti bajeti ya kufanya tafiti? Hii nchi ina viongozi wasiojielewa , badala aseme bajeti angalau isaidie hao wategemezi yenyewe yanasema bajeti ya tafiti
 
Hilo la kodi ya flat rate, maana yqke analipia kipato chake.
Kama ni flat rate basi itakuwa Kodi ya kichwa haijalishi ni nani au kipato chake kama inategemea kipato na watu wengi hawana officially recorded income hio itakuwa ngumu kuwa implemented
Anatumia nini kama hana kipato? Ni lazima kuna anapozipata.

Hiyo kodi iite vyovyoge utakavyo haijalishi. Iwe ya kichewa, ya miguu, ya kipato, Sito tatizo.
Huu uzi unasema katika watu mia; 87 nitegemezi sasa unataka hao 13 wawapatie hao 87 basic needs zao as well as kuwalipia Kodi ya Kichwa..., sababu kama ni kipato na officially wanapata sifuri basi watalipa sifuri...

Ndio hapo narudi nilipoanzia ni Jukumu la waliopo sasa / watunga sera wahakikishe wanatumia hii nguvu kazi iliyopo, kwa kufanya hivyo watakuwa sio tu wamezalisha kwa kutumia nguvu kazi bali kuepuka bomu la kesho la wazee ombaomba sababu watakuwa hawana pensheni...

 
Kodi ilipwe muda huohuo unapo toa huduma ama pata huduma kama vile miamala ya simu hakuna haja ya rundo la wafanyakazi wa TRa, natamani hapo baadae kodi ilipwe kama vile michango ya harusi ambao ukiambiwe ulipe milioni moja sema mimi nitalipa milioni 5
Tena hayo unayoyasema kwa teknolojia ya sasa yanawezekana kabisa. Hajalipa kodi hapati huduma yoyote. Kodi ndogo kumi kwa mia tu kwanini kila raia asilipe?
 
Kama ni flat rate basi itakuwa Kodi ya kichwa haijalishi ni nani au kipato chake kama inategemea kipato na watu wengi hawana officially recorded income hio itakuwa ngumu kuwa implemented

Huu uzi unasema katika watu mia; 87 nitegemezi sasa unataka hao 13 wawapatie hao 87 basic needs zao as well as kuwalipia Kodi ya Kichwa..., sababu kama ni kipato na officially wanapata sifuri basi watalipa sifuri...

Ndio hapo narudi nilipoanzia ni Jukumu la waliopo sasa / watunga sera wahakikishe wanatumia hii nguvu kazi iliyopo, kwa kufanya hivyo watakuwa sio tu wamezalisha kwa kutumia nguvu kazi bali kuepuka bomu la kesho la wazee ombaomba sababu watakuwa hawana pensheni...

Hujaelewa maana ya "flat rate".

Flat rate maana yake hakuna kila kodi na hesabu zake, tozo, sijui barabra, sijui nini. Inakuwa kodi moja tu across.

Kodi ya kichwa ni tofauti kabisa, niliikuta.
 
Kwanini ubebe mizigo ya wengine wakati uliyonayo bado yanakushinda.
Ni bora uonekani mbinafsi kuliko upate sonona.
 
Hujaelewa maana ya "flat rate".

Flat rate maana yake hakuna kila kodi na hesabu zake, tozo, sijui barabra, sijui nini. Inakuwa kodi moja tu across.

Kodi ya kichwa ni tofauti kabisa, niliikuta.
Twende polepole umesema kila mtu akimaliza shule achajiwe 10%.., sasa Nikuulize 10 percent ya nini ? Kama ni Kipato, kipato gani..., ambacho huyu tegemezi hana ?

Binafsi mimi naona na vyanzo vilivyopo Income Tax ingeweza kufutwa na bado Utalii, na Madini yakaendesha nchi ukizingatia sasa hivi kila kitu mwananchi analipia (Elimu; Bima ya Afya n.k.)...
 
Wala haihitaji akili nyingi sana ni uthubutu tu
Kabisa, watu wana "complicate" mambo ili kujitengenezea ufisadi.

Kama mafunndi gereji wa tabata au waganga wa kinyeji, kwanza lazima walikuze tatizo na walifanye kulitatuwa kwake ni complicated kweli kweli, ili wakulambe vizuri.

Adui yetu ni mmoja tu, ujinga.
 
Back
Top Bottom