Moja, Inawezakana Pasco umesahau au unajisahaulisha, unakumbuka mkuu alilalamika kuwa wapinzani ndiyo wamechelewa maendeleo??? walikuwa wanatoka nje au kuikataa bajeti iliyoletwa na serikali ya ccm??
Mbili, Unapendekeza JPM ateue wapinzani ili wakaunde KUB lakini jiulize, Je JPM bado anahitaji watu wa kumkwamisha??? au anataka mwaka 2025 awatumie kama sababu ya kutotimiza ahadi zake alizotoa maeneo mbalimbali????
Tatu, wakati wa kampeni JPM alisisitiza sana inshu ya connection na connection ameipata, mwambieni apeleke maendeleo kila kona ya nchi isipokuwa Nkasi na Mtwara vijijini, kwa sababu huko hawajampa connection.
Nne, Kwa wapinzani makini sana, nashauri hizi teuzi kama zikitokea basi wazikatae, CCM wanapaswa itambue kuwa upinzani siyo Chadema au ACT, ni idea, ni ideology, huwez kuiondoa kirahisi.
Hongereni ccm, sasa tunataka tuone utendaji kazi wa bunge lililo chini ya chama kimoja, Je kuna ufisadi utaibuliwa??? je taarifa ya CAG itajadiliwa kwa upana gani??? Je kamati za bunge zitafanya kazi kwa weledi gani???? Je bajeti zitakazowasilishwa na serikali zinapita kama zilivyo??? Je mlala hoi ataendelea kununuliwa ndege??? Je sheria zipi zitatungwa na kupitishwa???
Any way karibu kwa miaka mitano ijayo chini ya mfumo wa chama kimoja!