Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni?

Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni?

Nchi haitarudi nyuma sababu ya mfumo wa vyama vingi.Tangu 2015 wapinzani hawajafanyakazi zao za kibajeti, wamekuwa wakisusa kufanya maamuzi kama wabunge, bajeti zote za Magufuli zimekuwa xikipitishwa na wabunge wa ccm.

Sisi wananchi hatuoni value addition ya kambi ya upinzani bungeni.Mh Paskali Mayala umeleta hoja nzuri na ya mashiko, lakini kwa upinzani wa nchi hii sidhani kama watakubali, Lipumba tayari ametangaza hatashiriki yeye na chama chake chaguxi zoxote zijazo.Kuingia kwake bungeni utakuwa muendelezo wa misimamo yao ya kupinga hadi kieleweke.
 
Ni kweli kwani maisha hayataenda? Mwl.nyerere alituongoza kupitia mfumo huo na maisha yakaenda.Inaumiza sana kuwa na upinzani umaolifanyia udalali nchi yetu, upinzani uliotayari kupiga bei nchi.Hatuhotaji bora mfumo wa chama kimoja na rasilimali zetu xikabaki salama

Mpaka Leo una mawazo ya mtu kuuza inchi

Karne ya 21 bado unawaza kuuzwa

Ndio maana slogan ya lowasa ilikuwa ni ELIMU ELIMU ELIMU
 
Kwa ushauri wangu, napendekeza rais Magufuli awateue hawa wafuatao
1. Tundu Lissu- aligombea nae
2. Zitto Kabwe - Most Interactive MP
3. James Mbatia- Very Compromising
4. Prof Haruna Lipumba - Good Puppeteer
5. JJ.MNYIKA- Mjengaji hoja mzuri
Utmost cynical!
 
Nimesoma na kushangaa. Malengo ya ccm yametimia sasa kwanini ihangaike na walioshindwa kihalali. Meko alisema wapinzani wanachelewesha maendeleo sijui kama unalijua hilo.
Huruma hii ya ccm inatoka wapi. Pascal uwe mkweli ccm na Meko hawajawahi kuwa na busara hizo na hawatakuwa nazo.
 
Mbwana Mayala!

Mimi nina swali binafsi kukuhusu wewe, Je, umewahi kusafiri nje ya nchi hasa za magharibi na kukaa kwa muda kidogo? kama bado naomba ufanye haraka sana, maana naona una mapungufu makubwa sana kwenye upeo wako wa uelewa na hili limejidhihirisha kwenye mada zako zote uzitoazo.

AU UNAFANYA KUSUDI

Maana Mayalla yule aliyeuliza swali Magufuli siyo huyu ninayemuona kwenye makala hizi....

Mayalla huyu ni muoga, mwenye kujipendekeza n.k
 
Moja, Inawezakana Pasco umesahau au unajisahaulisha, unakumbuka mkuu alilalamika kuwa wapinzani ndiyo wamechelewa maendeleo??? walikuwa wanatoka nje au kuikataa bajeti iliyoletwa na serikali ya ccm??

Mbili, Unapendekeza JPM ateue wapinzani ili wakaunde KUB lakini jiulize, Je JPM bado anahitaji watu wa kumkwamisha??? au anataka mwaka 2025 awatumie kama sababu ya kutotimiza ahadi zake alizotoa maeneo mbalimbali????

Tatu, wakati wa kampeni JPM alisisitiza sana inshu ya connection na connection ameipata, mwambieni apeleke maendeleo kila kona ya nchi isipokuwa Nkasi na Mtwara vijijini, kwa sababu huko hawajampa connection.

Nne, Kwa wapinzani makini sana, nashauri hizi teuzi kama zikitokea basi wazikatae, CCM wanapaswa itambue kuwa upinzani siyo Chadema au ACT, ni idea, ni ideology, huwez kuiondoa kirahisi.

Hongereni ccm, sasa tunataka tuone utendaji kazi wa bunge lililo chini ya chama kimoja, Je kuna ufisadi utaibuliwa??? je taarifa ya CAG itajadiliwa kwa upana gani??? Je kamati za bunge zitafanya kazi kwa weledi gani???? Je bajeti zitakazowasilishwa na serikali zinapita kama zilivyo??? Je mlala hoi ataendelea kununuliwa ndege??? Je sheria zipi zitatungwa na kupitishwa???

Any way karibu kwa miaka mitano ijayo chini ya mfumo wa chama kimoja!
 
Nchi haitarudi nyuma sababu ya mfumo wa vyama vingi.Tangu 2015 wapinzani hawajafanyakazi zao za kibajeti, wamekuwa wakisusa kufanya maamuzi kama wabunge, bajeti zote za Magufuli zimekuwa xikipitishwa na wabunge wa ccm.Sisi wananchi hatuoni value addition ya kambi ya upinzani bungeni.Mh Paskali Mayala umeleta hoja nzuri na ya mashiko, lakini kwa upinzani wa nchi hii sidhani kama watakubali, Lipumba tayari ametangaza hatashiriki yeye na chama chake chaguxi zoxote zijazo.Kuingia kwake bungeni utakuwa muendelezo wa misimamo yao ya kupinga hadi kieleweke.
Value addition ni wao wapinzani kuwa Bungeni kurumbana na wenzao wa CCM

Maozaoza mangapi yameibuliwa na upinzani,au umesahau?

Wapinzani hawana haja ya wao kumuunga mkono,aliekuwepo madarakani..

Wapinzani kazi Yao ni kutafuta Makosa yako wapi halafu walifanyie kazi hilo kosa

MAWAZO ya wengi ni mtaji wa Taifa,Warumbano ya wanasiasa ni mtaji kwa raia
 
Nahisi haya mawazo siyo yako Bali Kuna mahali umekuta wanaccm Makini wanayajadili mahali Fulani nawe ukayachota na kuyaleta hapa!
Ccm ilidhani kuwa imefanya vyema kujishindisha na ikasahau kuwa katiba ya jmt inaitambua uwepo wa vyama vingi vya siasa pamoja na bunge kuwa na kambi rasmi ya upinzani!
Lazima kichwa kiwaume ccm kwa uzwazwa walioufanya! Wajiteue wenyewe Sasa kuunda kambi ya upinzani bungeni!
Na Kama Kuna walioandaliwa kuteuliwa Basi no wale waliokuwa wagombea wa nafasi ya urais aliowaalika siku Ile ya kukabidhiwa Cheti chake Cha ushindi wa kubumba!
 
"Kufuatia poor performance ya vyama vya upinzani kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, kwa Watanzania kuvikataa na badala yake kukichagua CCM pekee, but 4!, idadi hiyo haiwezi kutimiza akidi inayotakiwa kuweza kuunda kambi rasmi ya upinzani Bungeni".

Haya maneno hapa yata kuhukumu Siku moja Mkuu kwa kujifanya hukuona mambo yalio fanywa na upande wa pili dhidi ya Wapinzani.
 
Tundu Lisu yupi? Huyu ambaye sio raia wa Tanzania? Kesha ukana uraia kwa nini abembelezwe? Hawa wapumbavu wakae huko huko ndiko size yao.

Zito Kabwe yupi? Huyo mnafiki mwenye chama cha mfukoni? Kama umeshindwa kumwelewa huyu mnafiki toka atishiwe maisha yake kule Kenya hutamwelewa kamwe.

CCM ipo imara haina haja ya upinzani Bungeni. Watanzania sio wajinga, watu ambao kila uchwao wanatusengenya tena kwa makuwadi ati ushoga ndio kitu muhimu hapa duniani. P usipotoke.

 
Wapinzani jengeni hoja inaonekana hamjajifunza kutokana na makosa.Mmebaki kulalamika bila evidence.Iwapo mmeibiwa ni kesi ngapi mmefungua kupinga matokea, mnashangaza.Trump kadai kuibiwa kapeleka ushahidi mahakamani japo ni ushahidi weak usio na madhara kwa matokeo.

CHADEMA mmebaki kulalamikia wizi wa kimbunga bila kuwa na evidence.Ndiyo maana mleta hoja katumia phrase ya poor performance kwa upinzani. Pelekeni wawakilishi tujenge nchi na iwapo rais atateua kati yenu nendeni mkaape msaidie kujenga nchi yenu.Wapinzani mnatakiwa mchague hoja japo moja inayowagusa wananchi.

Mfano mkiamua kupigania kila kijiji kipate maji itawabebe na wananchi wataunga mkono.JENGENI NCHI YENU KWA KUTOA MICHANGO POSITIVE ACHENI KUISHI KWA KUKARIRI
 

jiwe.png


Hongera sana CCM !​
 
Ulichokiandika hapa ni ijinga wa hali ya juu sana.

1) Unaupongeza ushindi wa kishindo wa chama chako
2) unajishangalisha kwamba Zitto types hawatakuwepo bungeni
3) unataka wateuliwe bure kumpinga aliewateua?

Huo ukada wako usiokuwa na uzalendo kaa nao mwenyewe.

Sisi tunaoipenda nchi yetu tunajua nyie mnaojiita makada ni watu wa namna gani.
 
Back
Top Bottom