Mutakyamirwa
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 4,942
- 1,358
Hili limesemwa na wengine na limesemwa vizuri na Prof. Shivji kwamba Bunge la Katiba lina madaraka ya kuweza kufutilia mbali rasimu ya Katiba ya Tume ya Warioba ambayo kimsingi ni mahali pa kuanzia tu siyo mwisho. Kuna watu wanasema ati Bunge liko kwa ajili ya Kuboresha sijui wamepata wapi mawazo hayo; hayako kwenye sheria ya Katiba Mpya! Sheria ile - ambayo wengine tuliikosoa toka mwanzo - imelipa Bunge uwezo wa kufutia, kuongeza na hata kubadili rasimu ya Katiba ambayo ililetwa kwao na TUme ya Katiba chini ya Jaji Warioba.
Kwa vile madaraka ya Tume hiyo yamekoma, chombo pekee chenye madaraka ya kuandaa rasimu ya Katiba ambayo italetwa kwa wananchi kuulizwa ni Bunge la Katiba. Bunge la Katiba halitaleta rasimu ya Jaji Warioba bali rasimu yao ambayo wameiandaa kutokana na rasimu ya Warioba. Kama wajumbe wengi wanakubaliana na rasimu ya Warioba basi kitakacholetwa kwa wananchi kitafanana sana na ile; lakini kinyume chake ni kuwa Watanzania wanaweza kupigia kura rasimu ya Katiba tofauti.
Well.. habari ndiyo hiyo...
Basi kama ni hivyo hapakuwa na haja ya kuunda Tume ya Warioba,tungeanza na Bunge la Katiba moja kwa moja ili kuepuka gharama zisizokuwa za msingi. Kwa sababu kama Bunge la Katiba lina uwezoa pia wa kutengeneza rasimu tofauti kabia na ile ya Jaji Warioba, maana yake ni kwamab litakuwa ni Bunge la kutunga Katiba kulingana na linavyoona lenyewe. Rasimu a Warioba ndiyo imebeba mapendekezo ya watanzaina wote, Bunge la Katiba likitengeneza rasimu nyingine tofauti na ile ya Warioba, litakuwa limetengeneza rasimu isiyotana na maoni ya watanzania, sasa je, in case ikitokea hivi kutakuwa kulikuwa na hjaa gani ya kuwa na tume ya Warioba?
Na ikiwa itatokea watafanya kubadili maoni ya rasimu ya katiba kutoka kwenye tume ya Warioba ambayo yametokana na wananchi halafu wakaweka madudu yasiyo na chembe ya utaifa bali vyama vyao kwenye kura ya maoni lazima tuiteme, NI HERI KUWA NA PENGO KULIKO KUWA NA JINO BOVU LITAKALOKUSUMBUA USIKU NA MCHANA KWA MAUMIVU
Wazo hili ndilo lilikuwepo tangia mwanzo, kuwa mtawala ambaye amekuwa akikumbushwa mara zote kusimamia na kufuata katiba iliyopo huku akipuuza hawezi hata siku moja kuanzisha mfumo wa kuzirekebisha sheria zile zile ili zimbane yeye.
Wanaodhani kuwa hili linawezekana wakumbuke kuwa katiba mpya lilikuwa wazo la wapinzani na watawala walilidandia. Kutokana na nia yao kutokuwa halisi (sincerely) ndio maana limezungukwa na usanii ili 'lionekane limefanyika'.
Kinachoendelea hadi sasa ni ushahidi wa MMK kuwa mawazo feki yalizaa mchakato feki ambao umepelekea sheria feki, bunge feki (kama alivyoliita Mtikila) na mwisho itakuwa product feki.
October said:Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Abdallah Bulembo amemshambulia kwa maneno makali Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Joseph Warioba. Akihutubia mkutano wa CCM Tanga Bulembo amesema Warioba hana haki wala mamlaka ya kuwasemea Watanzania kuhusu Katiba mpya.
Bulembo ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu CCM amesema Warioba anapaswa kukaa mbali na kuwaamulia Watanzania Katiba aitakayo yeye. Huku akisisitiza kupinga kinachofanywa na Warioba aliwauliza wananchi kwa msisitizo..'Kwani Warioba ni Nani?' ....
Bado nakumbuka msimamo wa serikali ya CCM toka mwanzo kabisa...Alianza Waziri wa Sheria na Katiba wakati huo, Celina Kombaine, akafuatia Mwanasheria mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema, akafuatia Waziri Mpya wa Sheria na Katiba Mathias Chikawe na viongozi wengine wa Chama na serikali, wote wakidai hakuna umuhimu wa katiba mpya. Sasa lazima sote tujiulize na kujitafakari saana tu ndugu zangu, je kweli uongozi wa CCM uko tayari kuukubali rasimu hii kama ilivyotolewa na Tume ya Katiba? Jibu ni hapana. Mpango wote huu mpaka sasa ni kama danganya toto ila kuna kitu wanasahau; Tanzania ya sasa ni kitu kingine kabisa! Somebody is in for a rude shock!Januari said:MBUNGE wa Kwimba (CCM), Shanif Mansoor, ameishambulia Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji mstaafu, Joseph Warioba. Akizungumza jimboni kwake juzi alipokutana na wazee na waganga wa tiba za asili katika Kata ya Mankulwe, alimtaka Warioba na wenzake kuacha mara moja kuwa wapiga debe katika vyombo vya habari kuhusu Serikali tatu.
Hili limesemwa na wengine na limesemwa vizuri na Prof. Shivji kwamba Bunge la Katiba lina madaraka ya kuweza kufutilia mbali rasimu ya Katiba ya Tume ya Warioba ambayo kimsingi ni mahali pa kuanzia tu siyo mwisho. Kuna watu wanasema ati Bunge liko kwa ajili ya Kuboresha sijui wamepata wapi mawazo hayo; hayako kwenye sheria ya Katiba Mpya! Sheria ile - ambayo wengine tuliikosoa toka mwanzo - imelipa Bunge uwezo wa kufutia, kuongeza na hata kubadili rasimu ya Katiba ambayo ililetwa kwao na TUme ya Katiba chini ya Jaji Warioba.
Kwa vile madaraka ya Tume hiyo yamekoma, chombo pekee chenye madaraka ya kuandaa rasimu ya Katiba ambayo italetwa kwa wananchi kuulizwa ni Bunge la Katiba. Bunge la Katiba halitaleta rasimu ya Jaji Warioba bali rasimu yao ambayo wameiandaa kutokana na rasimu ya Warioba. Kama wajumbe wengi wanakubaliana na rasimu ya Warioba basi kitakacholetwa kwa wananchi kitafanana sana na ile; lakini kinyume chake ni kuwa Watanzania wanaweza kupigia kura rasimu ya Katiba tofauti.
Well.. habari ndiyo hiyo...
Well ,kumbe wamevaa mamlaka makubwa kiasi kile; basi watumie mamlaka hayo ya kisheria kubadilisha kipengele cha serikali tatu katika Rasimu ya Warioba na waje na mpango mzima wa serukali moja!!
Mheshimiwa kabisa HKigwangalla, naomba nikuulize tuswali tuwili;Ndg. Mwanakijiji,
Mimi si Mwanasheria lakini ni msomaji mzuri na makini wa nyaraka mbalimbali. Mzee Shivji na wewe mko sahihi sana. Sitaki kuchangia huko, ila nataka kuweka sawa jambo moja kidogo hapo kwenye post yako, kwamba; Bunge la Katiba halitozalisha 'Rasimu ya Katiba' tena, bali kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya Sheria za JMT ya Mwaka 2013, kifungu cha 25 (1), Bunge la Katiba litazalisha kitu kingine kabisa kinachoitwa 'Katiba inayopendekezwa'. Hii si lazima ifanane na ile ya Jaji Warioba na wenzake, hii ni zao la mijadala na maridhiano na hatimaye maazimio ya Bunge hili. Na hii ndiyo itapata uhalali wake kutoka kwa wananchi kupitia kura zao za ndiyo ama hapana. Kura zitapigwa kwa mujibu wa utaratibu unaopewa masharti na sheria ya kura za maoni ya mwaka 2013.
Wakatabahu,
HK.
Kumbe tunajadili katiba mpya huku tumefungwa pingu; nilidhani Katiba ndiyo sheria mama!Pole sana. Serikali moja imefungwa na sheria. Huwezi kuijadili. Na ni kwa sababu moja tu. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lazima iwepo kwenye picha!
Basi kama ni hivyo hapakuwa na haja ya kuunda Tume ya Warioba,tungeanza na Bunge la Katiba moja kwa moja ili kuepuka gharama zisizokuwa za msingi. Kwa sababu kama Bunge la Katiba lina uwezoa pia wa kutengeneza rasimu tofauti kabia na ile ya Jaji Warioba, maana yake ni kwamab litakuwa ni Bunge la kutunga Katiba kulingana na linavyoona lenyewe. Rasimu a Warioba ndiyo imebeba mapendekezo ya watanzaina wote, Bunge la Katiba likitengeneza rasimu nyingine tofauti na ile ya Warioba, litakuwa limetengeneza rasimu isiyotana na maoni ya watanzania, sasa je, in case ikitokea hivi kutakuwa kulikuwa na hjaa gani ya kuwa na tume ya Warioba?
Mzee Shivji na wewe mko sahihi sana.
Serikali moja imefungwa na sheria. Huwezi kuijadili. Na ni kwa sababu moja tu. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lazima iwepo kwenye picha!
Hayo ni mawazo yako na Ben, lakini sio lazima wabunge ''kama unavyowaita wabunge wa CCM'' wapinge maoni yote ya Jaji Warioba, tusipende sana kuongea na kutabiri na kufikiri kwamba mna akili za kugundua mawazo na hisia za watu wengine, Ngoja tusubiri tuone! tatizo lako MM,Ben nk ni wanaharakati na sio wanasiasa............naamini baada ya Bunge tutakutana JF!
Mwanakijiji, naomba tafsiri ya kifungu cha 25(2) cha sheria ya mabadiliko ya katiba.
25.-(1) Bunge Maalum litakuwa na mamlaka ya kujadili na kupitisha masharti ya katiba inayopendekezwa, kutunga masharti ya mpito na masharti yatokanayo kama Bunge Maalum litakavyoona inafaa.
(2) Mamlaka ya Bunge Maalum ya kupitisha masharti ya Katiba inayopendekezwa yatatekelezwa baada ya Rasimu ya Katiba kuwasilishwa na Mwenyekiti wa Tume na kupitishwa na Bunge Maalum.
Well ,kumbe wamevaa mamlaka makubwa kiasi kile; basi watumie mamlaka hayo ya kisheria kubadilisha kipengele cha serikali tatu katika Rasimu ya Warioba na waje na mpango mzima wa serukali moja!!
Pole sana. Serikali moja imefungwa na sheria. Huwezi kuijadili. Na ni kwa sababu moja tu. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lazima iwepo kwenye picha!
Ndg. Mwanakijiji,
ila nataka kuweka sawa jambo moja kidogo hapo kwenye post yako, kwamba; Bunge la Katiba halitozalisha 'Rasimu ya Katiba' tena, bali kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya Sheria za JMT ya Mwaka 2013, kifungu cha 25 (1), Bunge la Katiba litazalisha kitu kingine kabisa kinachoitwa 'Katiba inayopendekezwa'.
HK.
Kwa kawaida wajumbe wa Bunge la Katiba hawateuliwi. Pia wabunge wa bunge la kawaida hawawezi kuwa converted automatically kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba.
The so called "Bunge la Katiba" linaloendelea huko Dodoma halipo pale kwa ajili ya kupitisha rasimu ya Warioba.
Rather, it is there to merely rubber-stamp the decisions of the ruling party.