Hayawi hayawi, sasa yamekuwa...Watanzania kama hatutachukua tahadhari mapema, tumeliwa! Huu ni mwanzo tu na bado; CCM haina
nia wala
sababu ya kuheshimu maoni ya Watanzania walio wengi kama yalivyoanishwa kwenye rasimu ya Katiba mpya. Muundo wa Bunge la Katiba pekee unaonesha taswira ya wapi CCM inataka kutupeleka kuhusu upatikanaji wa katiba itakayokidhi matakwa ya wananchi bila kujali itikadi, dini, jinsia, rangi wala uwezo wa mali. Toka mapema walianza kujitokeza watu wa ajabu ajabu na kuanza kuhoji wakibeza ripoti ya Tume ya Katiba wakimlenga Mwenyekiti wake
Jaji Joseph Sinde Warioba. Wengine pamoja na kushangaa tulijiuliza ni wapi wana CCM hawa walikuwa wanapata ujasiri huo wa kumrushia madongo kada wao, Waziri Mkuu Mstaafu na mteuliwa wa Mwenyekiti wa chama tawala CCM!
October said:
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Abdallah Bulembo amemshambulia kwa maneno makali Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Joseph Warioba. Akihutubia mkutano wa CCM Tanga Bulembo amesema Warioba hana haki wala mamlaka ya kuwasemea Watanzania kuhusu Katiba mpya.
Bulembo ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu CCM amesema Warioba anapaswa kukaa mbali na kuwaamulia Watanzania Katiba aitakayo yeye. Huku akisisitiza kupinga kinachofanywa na Warioba aliwauliza wananchi kwa msisitizo..'Kwani Warioba ni Nani?' ....
Na kama vile hiyo haikutosha...
Januari said:
MBUNGE wa Kwimba (CCM), Shanif Mansoor, ameishambulia Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji mstaafu, Joseph Warioba. Akizungumza jimboni kwake juzi alipokutana na wazee na waganga wa tiba za asili katika Kata ya Mankulwe, alimtaka Warioba na wenzake kuacha mara moja kuwa wapiga debe katika vyombo vya habari kuhusu Serikali tatu.
Bado nakumbuka msimamo wa serikali ya CCM toka mwanzo kabisa...Alianza Waziri wa Sheria na Katiba wakati huo,
Celina Kombaine, akafuatia Mwanasheria mkuu wa Serikali
Jaji Fredrick Werema, akafuatia Waziri Mpya wa Sheria na Katiba
Mathias Chikawe na viongozi wengine wa Chama na serikali, wote wakidai hakuna umuhimu wa katiba mpya. Sasa lazima sote tujiulize na kujitafakari saana tu ndugu zangu, je kweli uongozi wa CCM uko tayari kuukubali rasimu hii kama ilivyotolewa na Tume ya Katiba? Jibu ni hapana. Mpango wote huu mpaka sasa ni kama danganya toto ila kuna kitu wanasahau; Tanzania ya sasa ni kitu kingine kabisa! Somebody is in for a rude shock!
Now enter Mwanazuoni na Mwanasheria nguli
Profesa Issa Shivji! Shivji hakuachwa kwenye Bunge la Katiba kwa bahati mbaya, hapana; Shivji,
muumini wa serikali mbili, ama aliachwa makusudi ili wakati muafaka ukifika CCM imtumie kulivuruga Bunge hilo kwa kupinga mapendekezo ya tume au hizi tetesi za kuwepo Katiba mbadala iliyoandaliwa na kikundi kisichojulikana (
chini ya Shivji?) huenda ikawa kweli. Hivi sasa kuna juhudi kubwa zinazofanyika kuonesha mapungufu ya rasimu kama ilivyotolewa na Tume na kama asemavyo
Mzee Mwanakijiji, si ajabu rasimu itakayofikishwa kwa wananchi ikawa tofauti kabisa na ya tume. Je Shivji naye kanunuliwa? Yangu macho.