Mnajua hata ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ulikuwa una-involve vitu gani hasa au mnajisemea tu mradi CNN,BBC walisha anza muda mrefu kuzulia Wachina kuhusu hasa ujio wa Wachina barani Afrika.
Kinacho wasumbua mabeberu hawa ni wivu na roho mbaya tu - wao waliwahi kuliachia bara la Afrika vitu gani vya kutusaidia kimaendeleo zaidi za wizi wa African vast natural resources na kwenda kujenga kwao, hapa mnajifanya kusahau Wachina vitu walivyo tujengea/achia in a record time, mfano: barabara,madaraja,viwanda,hydro electric dams(Ugand,Ethiopia na Ghana),mashule,vyuo vya ufundi, umeme,mawasiliano, mechanised Agriculture you name it, sasa hawa mabeberu walituachia vitu gani vya maana tangu waje barani Africa kwenye miaka ya 1885/86, nothing to speak about.
Kumbukeni mwaka juzi hapa si the late Dr.Magufuli aliwashika red handed Barrick wakitorosha ma containers ya madini wakijidai ni mchanga - mbona walikubali kulipa fidia - hilo hamlisemi? Badala yake masaa yote mnakalia kuwasema sema vibaya Wachina kwamba ni wezi, wachina ni wezi, wachina ni wezi!! Mnarudia rudia propaganda zile zile za vyombo vya habari vya magharibi - so called Chinese DEBT TRAP, debt trap - wakati nchi za magharibi zinadai Afrika mara kumi ya mikopo na riba lukuki kuliko madeni ambayo Wachina wanaidai Afrika, hilo mabeberu na baadhi yenu huwa hamuyasemi, mnashikilia MANTRA ya Wachina wezi, Wachina WEZI!!.