Bunge la Senate lapongeza zuio la Paul Makonda kuingia Marekani. Lasema huo ni mwanzo wa kuwawajibisha walioua demokrasia ya Tanzania

Bunge la Senate lapongeza zuio la Paul Makonda kuingia Marekani. Lasema huo ni mwanzo wa kuwawajibisha walioua demokrasia ya Tanzania

Makonda aka Bashite hajawahi kufanya jambo bila kuacha alama...Haya ni machache tu ila yapo mengi sana aliyofanya ambayo yanakandamiza haki za binadamu na uhuru wa kuishi....Bashite anafanya hayo akikingiwa kifua na Baba Yake Meko na Mjomba wao Hi Now.

1.Bashite anahusika 100% kwa kuawawa kwa Ben Saanane.
2.Bashite anahusika 100% kwa shambulio la Lissu.
Kutekwa kwa MO
 
Makonda bado ni kijana mdogo ana familia inakua changa nadhani yeye mwenyewe ataangalia haya yanakuaje kwasababu inavyoonekana hawa wanaoitwa mabeberu wamemkalia vibaya..
Ni vizuri tukipata nafasi za uongozi tujue kuna kesho na tuna watoto wanakua..hili ni jambo zito sana.
Katumiwa sana sasa atatupwa kama hawamjui. usimuamini mwana siasa ukitumika ukawa huna jipya basi ujuwe umeisha. wanasiasa hawana tufe pamoja ukiwa unahatarisha maslahi ya mtu unapigwa chini na mahakamani unaenda. Hii ni hatari kuliko tunavyodhania..
 
Mabeberu wanamuogopa jemedari wetu JPM amezuia mianya yao ya upigaji kupitia miradi yao ya hovyo huku na vibaraka wao..JPM anawanyoosha mabeberu sasa wameanza chokochoko..
Miradi ipi na mianya ipi?

Sifahamu kama USA wana mradi wowote hapa kwetu zaidi ya wao kuwekeza na au kutupa misaada.

Tufahamishe hiyo miradi na ukishindwa basi wewe ni muongo.
 
Mabeberu wanamuogopa jemedari wetu JPM amezuia mianya yao ya upigaji kupitia miradi yao ya hovyo huku na vibaraka wao..JPM anawanyoosha mabeberu sasa wameanza chokochoko..
Endeleeni kumtia ujinga. Wenye teknolojia zao wameshakusanya ushahidi.

Wamevumilia sana wakidhani ni ugeni wake na uongozi ila wameona kumbe ni tatizo kweli na wameanza kulishughulikia
 
Sisi ndo tuna raw materials, tuwapige ban US kule Geita kuchimba madini, jino kwa jino, SASA KAMA MKUU WA MKOA KAZUILIWA KUINGIA US ,ITAKUWAJE RAISI ALIYEZUIA MIKUTANO HALALI YA KIDEMOCRACIA?
 
Na wenyewe wamechoka, wanampiga ban Makonda kwenda Marekani ataenda kufanya nini huko kwao. Ni sawa na mimi kunipiga ban kuwa rubani wa ndege wakati hata abc kuhusu hizo ndege sizijui

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom