Bunge la Ulaya: Hii ni bahati mbaya au ni malengo maalum?

Bunge la Ulaya: Hii ni bahati mbaya au ni malengo maalum?

Ungekuwa umenisaidia sana kunishtua kwenye hizo post ili nirekebishe au nitoe mtazamo wangu

Yawezekana umeyaona hayo kwa kuwa MITAZAMO yetu Tofauti. Mimi natumia biblia kwa majira yote, yaliopita, haya na yajayo; sijui kwa hilo kama tuna mtazamo sawa. Kwangu mimi BIBLIA NI DIRA/MWONGOZO kwa vile jinsi Mungu atanijaria kufahamu. Nakubari kukosolewa na huwa napima ukosoaji kama sahihi au la.
Swali langu la msingi umejibu kuhusu lengo lao hasa (nashukuru). Zaidi nilitaka kupata mawazo zaidi na yangu, kwa nini Mungu alitumia njia ile kuwazuia na ujenzi (pia umenielewesha).
Maswali yako ya mwisho ni kweli jiografia yao ilikuwa ndogo ukilinganisha na leo. Kwa upande wangu naona Mungu aliamua kuwaokoa na janga la ajali ambalo ingeweza kutokea baada ya ghorofa kuwa juu.
Pia kuwawezesha waende kufanya mambo yao ya maisha kuliko kupoteza muda pale kwa kufuata mawazo ya wachache.
ahsante mkuu nashukuru sana.........................
ila kama kuna sehemu nimetumia lugha ya kuudhi au ambayo si nzuri naomba uniwie RADHI MKUU..............................
au kama kuna POINT nitakuwa nimekukwaza naomba uniwie RADHI pia...................

otherwise nashukuru kwa michango yako...........................
 
Shida siyo tu kuwa jengo ni ghorofa bali ni namna lilivyo.Jengo linalodhaniwa kuwa ni mnara wa Babeli linaonekana halijakamilika sawa sawa na jengo la bunge la Ulaya.Wakati wanajenga au kutafuta mchoro wa jengo hili walijua kabisa kuhusu habari ya Babeli....
mkuu ni kweli kuhusu hayo majengo kufanana na pia nadhani waliojenga hilo jengo la bunge walijua uwepo wa mnara wa babeli enzi izo.................

ila pia nafikiri ni vema tukitazama na upande wa pili yaani lengo/dhamira yao kati ya jengo la bunge na mnara wa babeli na sijui kwa upande wako unazungumziaje kuhusu hilo

Lakini zaidi wakaweka picha ya mnyama akiwa juu ya mnyama kama ufunuo 17 inavyosema.Ninafahamu kuwa inawezekana sanamu hiyo isihusiane na mnyama wa kwenye Ufunuo na ikahusiana na mwanamke EUROPA ambaye ni mungu mke aliyesababisha bara la Ulaya kUpewa jina EUROPE....
hapo kwenye red nadhani ulitaka kumaanisha MWANAMKE na sio mnyama.............
na kama ndivyo yaani MWANAMKE JUU YA MNYAMA (ufunuo 17), nachofahamu mimi ni kuwa hiyo iliotumika ni lugha ya picha ila haimaanishi MWANAMKE KAMA MWANAMKE(kwa maana ya jinsia) na kuhusu mnyama haimaanishi MNYAMA KAMA MNYAMA(kwa maana ya viumbe kama simba au chui nk)

ila enzi izo za uandishi wa kitabu cha ufunuo wahusika walielewa vyema kabisa..............

so kuhusu uwepo wa MWANAMKE JUU YA MNYAMA kwenye jengo la hilo bunge nadhani inaweza kuwa na mahusiano na hiyo factor ya upatikanaji wa jina EUROPE na mambo ya mungu mke japo sina uhakika sana sababu sijafuatilia sana hayo mambo ya jina EUROPE na mungu mke

so nadhani ili kufahamu vyema na kupata majibu sahihi zaidi kuhusu HIYO SANAMU YA MWANAMKE JUU YA MNYAMA, itakuwa ni lazima kutafiti na kufuatilia MILA NA TAMADUNI zao kuhusu mambo mbalimbali kama matumizi ya wanyama na alama zao zingine.........

mkuu pia ni muhimu kufikiria kuwa kila nchi au jumuiya ina VITAMBULISHO VYAKE VYA KITAIFA AU JUMUIYA (mfano waweza rejea nembo yetu ya taifa, na ambayo utaikuta kwenye maeneo nyeti na muhimu kama bungeni, ikulu nk na sehemu zingine imewekwa si kipicha tu ila SANAMU, nadahi vitu vilivyomo kwenye nembo yetu ya kitaifa unavifahamu na maana zake)

nawaza tu labda picha au sanamu ya aina kama ya nembo yetu ya taifa ingekuwa imetajwa/kuonekana kwenye kitabu cha ufunuo/danieli tungewaza na kufikiria nini mkuu ??..

Kuna mengi ya Ulaya mkuu na hili ni dogo tu....
mkuu hayo "mengi ya ulaya" na makubwa zaidi ningeomba utuoneshe japo kiufupi walau kwa kutaja tu pia .................
na LINK za kuyafuatili zaidi kama utapenda kutupatia ili nasi tuongeze wigo wa kujifunza na kujua mengi zaidi
 
jukwaa ladini siku hizi hamna kitu, labda tuite jukwaa la wasabato!
 
mkuu ni kweli kuhusu hayo majengo kufanana na pia nadhani waliojenga hilo jengo la bunge walijua uwepo wa mnara wa babeli enzi izo.................

ila pia nafikiri ni vema tukitazama na upande wa pili yaani lengo/dhamira yao kati ya jengo la bunge na mnara wa babeli na sijui kwa upande wako unazungumziaje kuhusu hilo

Hapa kenye dhamira ndipo kwenye maana sana mkuu.Nashindwa hata nianze vipi lakini kwa nijuavyo ni kwamba wakati wa ujenzi wa mnara/jengo la Babel wakati wa Nimrod alikuwa na lengo/malengo....

1;Kuhakikisha mafuriko/gharika ikija tena watu wasife...
2;Kuunganisha watu wote wa dunia mahali pamoja kinyume na maagizo ya Mungu watawanyike..[Mwanzo 11:9]

Sababu za ujenzi wa mnara huu zipo nyingi sana lakini siyo zote zimeandikwa kwenye biblia...

Kimsingi,umoja wa Ulaya kujenga jengo lenye picha au muonekano kama wa mnara/jengo la Babeli ni kuonesha kwamba wanataka kukikamilisha kile ambacho Nimrod hakukikamilisha,hii ina maana kwamba watalimalizia jengo lile....

hapo kwenye red nadhani ulitaka kumaanisha MWANAMKE na sio mnyama.............
Ni kweli mkuu nilikuwa namaanisha hivyo,ni makosa ya uandishi tu...

Ahsante kwa kunisahihisha....
na kama ndivyo yaani MWANAMKE JUU YA MNYAMA (ufunuo 17), nachofahamu mimi ni kuwa hiyo iliotumika ni lugha ya picha ila haimaanishi MWANAMKE KAMA MWANAMKE(kwa maana ya jinsia) na kuhusu mnyama haimaanishi MNYAMA KAMA MNYAMA(kwa maana ya viumbe kama simba au chui nk)

ila enzi izo za uandishi wa kitabu cha ufunuo wahusika walielewa vyema kabisa..............
Ni kweli kabisa mkuu na sipingani na wewe kwenye hili,labda cha kuongezea tu ni kwamba lengo lao la kuweka sanamu hii ni ile ile ambayo imesababisha Ufunuo 17 kutajwa kwa mnyama akiwa amembeba mwanamke...
so kuhusu uwepo wa MWANAMKE JUU YA MNYAMA kwenye jengo la hilo bunge nadhani inaweza kuwa na mahusiano na hiyo factor ya upatikanaji wa jina EUROPE na mambo ya mungu mke japo sina uhakika sana sababu sijafuatilia sana hayo mambo ya jina EUROPE na mungu mke
so nadhani ili kufahamu vyema na kupata majibu sahihi zaidi kuhusu HIYO SANAMU YA MWANAMKE JUU YA MNYAMA, itakuwa ni lazima kutafiti na kufuatilia MILA NA TAMADUNI zao kuhusu mambo mbalimbali kama matumizi ya wanyama na alama zao zingine.........
Yote haya yanaunganisha kitu kile kile mkuu...

Tatizo lililosababisha Yohana kumuona mwanamke juu ya mnyama lina maana mbili...

1;Dini
2;Siasa

Haya yote yanahusiana na dini ya kipagani ambayo itapewa nguvu na serikali [siasa] na dini hiyo ni ya kipagani na ndiyo hiyo hiyo inayohusiana na huyo mwanamke aliyesababisha jila hilo la bara la Ulaya....

mkuu pia ni muhimu kufikiria kuwa kila nchi au jumuiya ina VITAMBULISHO VYAKE VYA KITAIFA AU JUMUIYA (mfano waweza rejea nembo yetu ya taifa, na ambayo utaikuta kwenye maeneo nyeti na muhimu kama bungeni, ikulu nk na sehemu zingine imewekwa si kipicha tu ila SANAMU, nadahi vitu vilivyomo kwenye nembo yetu ya kitaifa unavifahamu na maana zake)

nawaza tu labda picha au sanamu ya aina kama ya nembo yetu ya taifa ingekuwa imetajwa/kuonekana kwenye kitabu cha ufunuo/danieli tungewaza na kufikiria nini mkuu ??..
Ni kweli kabisa mkuu kila nchi ina nembo zake na vitu mbali mbali vya kuitambulisha nchi husika,lakini kinachofanya nembo fulani zijadiliwe na kuhusishwa na unabii wa biblia siyo kwamba alama/nembo hizo zimeandikwa/kutajwa kwenye biblia bali kuna mambo mengine zaidi....

Mambo ya imani wanayotumia,malengo yao na ulimwengu ujao na mambo mengine mengi ndiyo yanayojumuisha sababu zinazofanya tuhusishe nembo/mataifa fulani na unabii wa biblia wa nyakati wa mwisho....

mkuu hayo "mengi ya ulaya" na makubwa zaidi ningeomba utuoneshe japo kiufupi walau kwa kutaja tu pia .................
na LINK za kuyafuatili zaidi kama utapenda kutupatia ili nasi tuongeze wigo wa kujifunza na kujua mengi zaidi
Kiukweli yapo mengi sana tena sana na tukianza kuyajadili hapa ni kazi ngumu kweli kweli.Lakini tu ni kwamba mambo ya kisiasa na kiimani ya nchi za ulaya na America hadi Asia huko ni mojawapo....

Malengo yao ya baadaye kuhusu maisha ya binadamu pamoja na usalama wa binadamu wenyewe...

Kuanzishwa kwa harakati mbali mbali kuanzia haki za wanawake,kuanzishwa kwa UN,vita vyote vya dunia,uchumi wa mataifa yote yalioanguka na yaliyo imara leo,maendeleo ya sayansi,maradhi,majanga yanayoonwa ya kiasili kama Tsunami,mafuriko n.k,uanzishwaji wa shirika la afya duniani WHO,benki ya dunia,mashirika ya ujasusi duniani na mengine mengi sana yanafanya kuwepo na ushahidi wa haya ninayokuambia...

Sina link moja ambayo utaweza kusoma ukaelewa ninachokueleza bali ni muunganiko wa utafiti mrefu wa siku nyingi sana uliofanya nikafahamu mengi sana....

Kwa maana hii nashindwa kujibu swali lako moja kwa moja mkuu juu ya kukupa link,lakini fahamu tu kwamba hatuko salama kabisa na kuna watu wana mipango mibaya kabisa na maisha yetu na hao ndiyo wameelezwa kwenye unabii wa Biblia ili tuwe makini....
 
mkuu unaposema tuwe makini natak kuamini hatuambii sisi wa hali ya chini, maana hatuna tunachoweza kufana. labda ungesema serikali na taasisi zetu na dini. lakini wakina sisi tungojee tu matokeo.
 
Nani alipiga picha mnara was babeli,kamera zilikuwa hazijagunduliwa,hamna conspiracy theory hapo,ni mambo ya kawaida tu
 
Hapa kenye dhamira ndipo kwenye maana sana mkuu.Nashindwa hata nianze vipi lakini kwa nijuavyo ni kwamba wakati wa ujenzi wa mnara/jengo la Babel wakati wa Nimrod alikuwa na lengo/malengo....

1;Kuhakikisha mafuriko/gharika ikija tena watu wasife...
2;Kuunganisha watu wote wa dunia mahali pamoja kinyume na maagizo ya Mungu watawanyike..[Mwanzo 11:9]
mkuu kiukweli mimi bado siamimini na kukubaliana katika hoja ya ufanano na kushabihiana kwa vitu (majengo) pekee ...........

hivyo sidhani kama fact ya ufanano/kushabihiana pekee inajitosheleza sababu kuna vitu/mambo mengi tu hasa majengo yametokea kufanana lakini kila mmoja akiwa na lengo/malengo yake tofauti na mwingine......

mfano kisu/pamga kama kisu/panga si dhambi lakini aina ya matumizi/malengo aliyopanga mtumiaji kukitumia ndo inaweza kuwa dhambi au isiwe dhambi mkuu......

na ndoo maana mkuu kuhusu hayo majengo mimi nimejikita kwenye lengo/malengo....
so mi nadhani pia ni vyema tukatazama malengo ya wajenzi wa bunge la ulaya huko belgium then tukalinganisha na lengo/malengo ya ujenzi wa mnara wa babeli

ila kubaki kwenye ufanano tu sidhani kama tunaweza kuwa sahihi mkuu......

Sababu za ujenzi wa mnara huu zipo nyingi sana lakini siyo zote zimeandikwa kwenye biblia...
mkuu na mimi unaweza nisaidia hiyo source yenye mengi kuhusu mnara wa baberi ili nami nikafuatilie zaidi........

Tatizo lililosababisha Yohana kumuona mwanamke juu ya mnyama lina maana mbili...

1;Dini
2;Siasa

Haya yote yanahusiana na dini ya kipagani ambayo itapewa nguvu na serikali [siasa] na dini hiyo ni ya kipagani na ndiyo hiyo hiyo inayohusiana na huyo mwanamke aliyesababisha jila hilo la bara la Ulaya....
ni kwamba lengo lao la kuweka sanamu hii ni ile ile ambayo imesababisha Ufunuo 17 kutajwa kwa mnyama akiwa amembeba mwanamke...
inshort mkuu kitabu cha ufunuo kilikuwa na wahusika wake wa kwanza kabisa ambao ni walengwa na waliosababisha kuandikwa kwa kitabu hicho cha ufunuo
mambo kama madhulumu ya wakristo wa wakati huo, dola ya warumi na makaisari wao kabla ya kaisari CONSTANTINE miaka ya karne ya 4BK , wakristo wa mwanzo hasa waliopitia madhulumu enzi izo, hao ndo wahusika na walengwa wakuu wa icho kitabu cha ufunuo.......

Hata hivyo, mkuu sina maana kwamba kitabu cha ufunuo hakituhusu au hakina mahusiano kabisa na wakati wetu/nyakati zetu hizi na nyakati zijazo la hasha ila NAMNA AMBAYO MIMI NA WEWE NA WENGINE NA MAMBO MENGINE KAMA SERIKALI, MADOLA, VIONGOZI NK HATUWEZI/HAVIWEZI KUHUSIKA KWA 100% (kwa maana ya aya hadi aya na sura hadi sura ya kitabu cha ufunuo na kila kitu kinacho elezwa humo)

kwa mfano
dola ya Warumi inayooneshwa kaika lugha ya picha inaweza kuwa ni mfano wa dola zote ambazo zitajaribu kulipinga Kanisa
nakadhalika.........

Kuanzishwa kwa harakati mbali mbali kuanzia haki za wanawake,kuanzishwa kwa UN,vita vyote vya dunia,uchumi wa mataifa yote yalioanguka na yaliyo imara leo,maendeleo ya sayansi,maradhi,majanga yanayoonwa ya kiasili kama Tsunami,mafuriko n.k,uanzishwaji wa shirika la afya duniani WHO,benki ya dunia,mashirika ya ujasusi duniani na mengine mengi sana yanafanya kuwepo na ushahidi wa haya ninayokuambia...
kama ni hayo mambo
hapo mkuu ni kweli kbisa sidhani kama unaweza yapata kwa pamoja sehemu moja(link)

in short hapo juu mambo mengi nayafahamu vizuri ila baadhi kama vita vyote vya dunia navifahamu kijujuu tu (kikawaida) na si kiundani sana........

nashindwa nianzeje kuhusu izo harakati ulizozihainisha hapo juu
so nachoomba mkuu labda ungejaribu kufafanua kidogo kwamba HIZO HARAKAI ZOTE ULIZOZIAINISHA HAPO JUU PAMOJA NA ZINGINE NYINGI ZA HAYO MATAIFA YA ULIMWENGU WA KWANZA, ZOTE KIUJUMLA WAKE HAZINA NIA NJEMA NA MAISHA YA BINADAMU ????
AU ULITAKA KUMAANISHA NINI ?????
 
Dah..
nimekuelewa mkuu...

samahani kwa mfano WHO (shirika la afya duniani) na benki ya dunia kivipi vinakuwa adui wa binadamu mkuu....
WHO ambalo ni shirika la afya duniani ndilo shirika linalosimamia masuala yote ya afya,hii inakuwa na maana tafiti zote na gunduzi zote za masuala ya afya ziko chini yao.Kama leo wakisema daswa fulani haifai kwa matumizi ya binadamu inakataliwa duniani pote na iko hivyo kwenye tafiti za maradhi,wakisema kuna ugonjw fulani inakubaliwa hivyo na wakisema hakuna ugonjwa fulani inakubaliwa hivyo....

Hawa wapo chini ya "binadamu" ambao wana malengo mengi na machache ni haya;

1;Kupata utajiri kupitia taasisi ya madawa duniani
2;Kuhakikisha kundi moja la binadamu linaendelea kuwa dhaifu kiafya ili litawaliwe...

Kwenye utajiri

Kuna maradhi kama kansa,maradhi haya yana tiba tena rahisi kabisa lakini WHO wanasema haya maradhi hayana dawa.Wapo watu wameshatibiwa na wamepona kwa vyakula tu.Tiba ya kansa ni miongoni mwa tiba ghali kabisa.Mashine ya mionzi inakwenda kwenye bil 3 huko.Dozi ya Chemotherapy ni zaidi ya mil 3 na tiba hii unaitumia hadi siku unakufa,sitaki kusemea madhara ya hii tiba maana ni hatari kweli kweli....

Hebu fikiria kuna hospitali ngapi duniani na zote zinahitaji hiyo mitambo ya mionzi,piga hesabu ni sh ngapi wanapiga hapo.Fikiria kuna wagonjwa wengi kiasi gani na wanatakiwa kupata hiyo tiba ya Chemo,piga hesabu ni sh ngapi wanapiga hapo,kumbuka hapo nimezungumzia ugonjwa mmoja tu na kuna rundo la maradhi duniani yaliyopo na yasiyokuwepo...

Kwenye udhaifu

Madawa mengi ambayo tunaletewa yana sumu nyingi kweli kweli.Mfano mzuri wa hili ni hiyo Chemotherapy ambayo wagonjwa wa kansa hupewa.Tiba hiyo inasababisha figo kufail,inavuruga kinga ya mwili kwa kiwango cha hatari kabisa.Hakuna mgonjwa wa kansa aliyewahi kupona kwa tiba hii zaidi atajisikia afadhali kwa muda tu na baadaye utasikia tumbo linajaa maji n.k na hayo ni madhara ya tiba hii....

ARVs,hizi ni miongoni mwa dawa zenye sumu kweli kweli.Madaktari watajitetea kwamba hakuna dawa yenye side efect,ni kweli lakini pale hizo side efect zinapokuwa mbaya zaidi ya ugonjwa basi inakuwa ni balaa na dawa hizi hazifai kabisa.....

Ukiachilia mbali hadithi ya HIV ambayo inashangaza sana,madawa haya ambayo wanadai yanaongeza maisha ya watu wenye virusi hivyo,madawa hayo ndiyo yanayowauwa...

Wale wanaotumia madawa haya lazima utakuja kuwasikia wamepungukiwa damu,nywele zao zinanyonyoka,wanapata kansa ya ngozi,ini linafail na mengine mengi ambayo wewe nw wengine wanadai ni matokeo ya HIV wakati siyo kweli....

Mkuu,kuna mengi lakini niishie hapo maana ni mengi na ukiyajua unaweza kupasuka kwa hasira lakini ukweli ndiyo huo....

Benki ya Dunia

Hii benki ipo chini ya Rothchild na Rockerfeller,tuachane na hawa maana unaweza kusema ni makonsipirasi....

Misaada inayotoka benki ya dunia haina jema lolote kwa nchi yoyote,Nipe jina hata la nchi moja tu iliyoweza kupiga hatua kwasababu tu ya misaada hii.Masuala yote ya kifedha duniani yanasimamiwa na benki hii,kwanini wanakaa kimya kwenye masuala ya kishetani ya kifedha huku duniani?

Mkuu,mikopo hii ndiyo inayodidimiza nchi zetu.Ukitaka kufahamu haya masuala wewe fuatilia hizi fedha zinazoletwa huku na World bank halafu utaona.Historia ya kuanzishwa benki ya dunia inaturudisha kule kule kwenye ubeberu wa nchi kutaka kuendelea kuzitawala nchi zingine.....
 
mkuu nashukuru nimekupata na nimekuelewa......

ni kweli kabisa kuwa kuna sera zingine za nje hazina malengo mazuri kabisa na nchi za Afrika. LAKINI SINA HAKIKA KAMA NI ZOTE.....

pia kwa ufafanuzi wako ulionipatia hapo juu pia naweza kukuunga mkono kwa upande wa baadhi ya sera na mpango wa mashirika ya nje (ya kimataifa) KATIKA KUPAMBANA NA ONGEZEKO LA IDADI YA WATU DUNIANI kuna sera hazina nia nzuri kabisa na watu weusi kwa mfano mpango wa nyota ya kijani nakadhalika

kwa mfano: tukiangalia WHO na benki ya dunia jinsi wanavopigia chapuo na mikazo na kiufadhili hasa katika nchi nyingi za kiafrika kuhusu MPANGO wa NYOTA YA KIJANI

Baada ya mafanikio ya Marekani katika miaka ya 1960 mpaka 1970 katika kudhibiti ongezeko la idadi ya watu duniani watetezi wa nadharia za udhibiti wa idadi ya watu walipiga hodi Umoja wa Mataifa na Benki ya Dunia. Shirika la idadi ya watu la umoja wa Mataifa-United Nations Fund for Population Activities (UNFPA), sasa linajiita United Nations Population Fund (UNPF), Shirika la Kimataifa la Mfuko wa Watoto (United Nations Children’s Fund-UNCEF), Shirika la Chakula na Kilimo (Food and Agriculture Organization-FAO), na Shirika la Afya Duniani (World Health Organization-WHO), yaliyounganisha nguvu zao kwa lengo la kudhibiti ongezeko la idadi ya watu, yakiweka mkazo mkubwa katika nchi maskini hasa afrika. Chini ya Roberts McNamara, Benki ya Dunia ilitoa fedha nyingi kwa serikali za nchi maskini kwa kuendesha program za kudhibiti idadi ya watu. kama mpango wa nyota ya kijani

pia mkuu kwa upande wa madawa,
madawa na sindano kama Sindano ya Depoprovera, Sindano ya Dawa ya Lunelle, Vitanzi

Ndugu yangu, tatizo linalotukumba waafrika wengi ni kudandia gari kwa mbele. Yaani kuchukua mambo bila kuchuja kisa eti yametoka kwa wazungu yaani Ulaya. Labda ni kwa sababu ya mfumo wetu wa elimu au fikra zilizoachwa na wazungu baada ya ukoloni. Vyovyote vile ukweli ni kwamba ukoloni bado unaendelea lakini umevaa miwani ya aina nyingine. Ukoloni huu tunauita ukoloni mamboleo “neo- colonialism”.hivyo Waafrika tunapaswa kuamka toka usingizini na kujikomboa kwanza na utumwa wa kifikra kishapo mengine yatafuata. Hapa ninamkumbuka gwiji la mziki wa reggae hayati Bob Marley katika wimbo Emancipation from Mental Slavery anatuambia “Jikomboeni wenyewe kutoka katika utumwa wa kifikra. Hakuna wa kutokomboa kutoka katika utumwa huo bali ni sisi wenyewe.”

hivyo katika hilo ni kweli kabisa mkuu Ni wakati mwafaka wa waafrika wote kuamka toka usingizini na kutokuwa watumwa wa baadhi ya sera za wazungu...

mkuu mi naomba niishie hapo sababu sina utaalamu sana wa kiutafiti na ufuatiliaji WA MIPANGO NA SERA NYINGI ZA KIZUNGU hasa za mambo ya kisasa zaidi (hapa kiukweli nami itabidi nianze kuyafuatilia haya masuala ya mipango na sera za kizungu kwetu afrika kiundani zaidi)

zaidi ya hapo mkuu nashukuru sababu kupitia baadhi ya post zako kama hizi za mipango na sera za kizungu kwetu afrika ZIMENITIA HAMASA YA NAMI KUANZA KUFUATILIA NA KUTAFITI MIPANGO NA SERA ZA HAYA MASHIRIKA YA KIMATAIFA ILI KUJUA MENGI ZAIDI....

nilijikita sana kwenye mambo ya kiimani na biblia zaidi lakini nadhani kwa sasa itabidi nipanue wigo zaidi.....

nakutakia majukumu mema mkuu....
 
Mpaka sasa mtu ukiwa na Yesu moyoni mambo a habar za siku ya mwisho hazitakutaabisha. Hii ni kwasabb yeye ni mambo yote katika yote.

Pia ufalme wa Mungu ukishuka ndani yako na kiti chakr cha enzi kitashuka.

Huyo mpunga Kristo hatakusumbua kwan anajua maziwa,i kwamba ww sio mmoja wao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom