mkuu ni kweli kuhusu hayo majengo kufanana na pia nadhani waliojenga hilo jengo la bunge walijua uwepo wa mnara wa babeli enzi izo.................
ila pia nafikiri ni vema tukitazama na upande wa pili yaani lengo/dhamira yao kati ya jengo la bunge na mnara wa babeli na sijui kwa upande wako unazungumziaje kuhusu hilo
Hapa kenye dhamira ndipo kwenye maana sana mkuu.Nashindwa hata nianze vipi lakini kwa nijuavyo ni kwamba wakati wa ujenzi wa mnara/jengo la Babel wakati wa Nimrod alikuwa na lengo/malengo....
1;Kuhakikisha mafuriko/gharika ikija tena watu wasife...
2;Kuunganisha watu wote wa dunia mahali pamoja kinyume na maagizo ya Mungu watawanyike..[Mwanzo 11:9]
Sababu za ujenzi wa mnara huu zipo nyingi sana lakini siyo zote zimeandikwa kwenye biblia...
Kimsingi,umoja wa Ulaya kujenga jengo lenye picha au muonekano kama wa mnara/jengo la Babeli ni kuonesha kwamba wanataka kukikamilisha kile ambacho Nimrod hakukikamilisha,hii ina maana kwamba watalimalizia jengo lile....
hapo kwenye red nadhani ulitaka kumaanisha MWANAMKE na sio mnyama.............
Ni kweli mkuu nilikuwa namaanisha hivyo,ni makosa ya uandishi tu...
Ahsante kwa kunisahihisha....
na kama ndivyo yaani MWANAMKE JUU YA MNYAMA (ufunuo 17), nachofahamu mimi ni kuwa hiyo iliotumika ni lugha ya picha ila haimaanishi MWANAMKE KAMA MWANAMKE(kwa maana ya jinsia) na kuhusu mnyama haimaanishi MNYAMA KAMA MNYAMA(kwa maana ya viumbe kama simba au chui nk)
ila enzi izo za uandishi wa kitabu cha ufunuo wahusika walielewa vyema kabisa..............
Ni kweli kabisa mkuu na sipingani na wewe kwenye hili,labda cha kuongezea tu ni kwamba lengo lao la kuweka sanamu hii ni ile ile ambayo imesababisha Ufunuo 17 kutajwa kwa mnyama akiwa amembeba mwanamke...
so kuhusu uwepo wa MWANAMKE JUU YA MNYAMA kwenye jengo la hilo bunge nadhani inaweza kuwa na mahusiano na hiyo factor ya upatikanaji wa jina EUROPE na mambo ya mungu mke japo sina uhakika sana sababu sijafuatilia sana hayo mambo ya jina EUROPE na mungu mke
so nadhani ili kufahamu vyema na kupata majibu sahihi zaidi kuhusu HIYO SANAMU YA MWANAMKE JUU YA MNYAMA, itakuwa ni lazima kutafiti na kufuatilia MILA NA TAMADUNI zao kuhusu mambo mbalimbali kama matumizi ya wanyama na alama zao zingine.........
Yote haya yanaunganisha kitu kile kile mkuu...
Tatizo lililosababisha Yohana kumuona mwanamke juu ya mnyama lina maana mbili...
1;Dini
2;Siasa
Haya yote yanahusiana na dini ya kipagani ambayo itapewa nguvu na serikali [siasa] na dini hiyo ni ya kipagani na ndiyo hiyo hiyo inayohusiana na huyo mwanamke aliyesababisha jila hilo la bara la Ulaya....
mkuu pia ni muhimu kufikiria kuwa kila nchi au jumuiya ina VITAMBULISHO VYAKE VYA KITAIFA AU JUMUIYA (mfano waweza rejea nembo yetu ya taifa, na ambayo utaikuta kwenye maeneo nyeti na muhimu kama bungeni, ikulu nk na sehemu zingine imewekwa si kipicha tu ila SANAMU, nadahi vitu vilivyomo kwenye nembo yetu ya kitaifa unavifahamu na maana zake)
nawaza tu labda picha au sanamu ya aina kama ya nembo yetu ya taifa ingekuwa imetajwa/kuonekana kwenye kitabu cha ufunuo/danieli tungewaza na kufikiria nini mkuu ??..
Ni kweli kabisa mkuu kila nchi ina nembo zake na vitu mbali mbali vya kuitambulisha nchi husika,lakini kinachofanya nembo fulani zijadiliwe na kuhusishwa na unabii wa biblia siyo kwamba alama/nembo hizo zimeandikwa/kutajwa kwenye biblia bali kuna mambo mengine zaidi....
Mambo ya imani wanayotumia,malengo yao na ulimwengu ujao na mambo mengine mengi ndiyo yanayojumuisha sababu zinazofanya tuhusishe nembo/mataifa fulani na unabii wa biblia wa nyakati wa mwisho....
mkuu hayo "mengi ya ulaya" na makubwa zaidi ningeomba utuoneshe japo kiufupi walau kwa kutaja tu pia .................
na LINK za kuyafuatili zaidi kama utapenda kutupatia ili nasi tuongeze wigo wa kujifunza na kujua mengi zaidi
Kiukweli yapo mengi sana tena sana na tukianza kuyajadili hapa ni kazi ngumu kweli kweli.Lakini tu ni kwamba mambo ya kisiasa na kiimani ya nchi za ulaya na America hadi Asia huko ni mojawapo....
Malengo yao ya baadaye kuhusu maisha ya binadamu pamoja na usalama wa binadamu wenyewe...
Kuanzishwa kwa harakati mbali mbali kuanzia haki za wanawake,kuanzishwa kwa UN,vita vyote vya dunia,uchumi wa mataifa yote yalioanguka na yaliyo imara leo,maendeleo ya sayansi,maradhi,majanga yanayoonwa ya kiasili kama Tsunami,mafuriko n.k,uanzishwaji wa shirika la afya duniani WHO,benki ya dunia,mashirika ya ujasusi duniani na mengine mengi sana yanafanya kuwepo na ushahidi wa haya ninayokuambia...
Sina link moja ambayo utaweza kusoma ukaelewa ninachokueleza bali ni muunganiko wa utafiti mrefu wa siku nyingi sana uliofanya nikafahamu mengi sana....
Kwa maana hii nashindwa kujibu swali lako moja kwa moja mkuu juu ya kukupa link,lakini fahamu tu kwamba hatuko salama kabisa na kuna watu wana mipango mibaya kabisa na maisha yetu na hao ndiyo wameelezwa kwenye unabii wa Biblia ili tuwe makini....