Bunge la Ulaya: Hii ni bahati mbaya au ni malengo maalum?

Sasa mkuu kama huyo mkuu atakaekuja ni Mpinga Kristo,mbona waliolivunja hekalu ni watu wa Titus?

Kama ni Rumi inayoongelewa hapo hebu niambie unabii ulioko kwenye Danieli 7:24-26 imetimizwaje? Maana maandiko yanasema hayo yatatokea mara tu baada ya ule ufalme wa nne

Danieli 7:24-26
24 Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.
25 Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.
26 Lakini hukumu itawekwa, nao watamwondolea mamlaka yake, kuipoteza na kuiangamiza, hata milele.


Kama unakumbuka tuliwahi kujadili hilo na tukakubaliana kuwa hiyo pembe ndogo ni Mpinga Kristo,kama hapo inasema huyu atainuka baada ya kuondoka Rumi kisha kuinuka pembe ndogo na kisha kuinuka huyu Mpinga Kristo,tunatarajia haya yawe tayari yametokea kwasababu Rumi ilishaanguka ila hayo mengine sijui ni yapi hayo

Hebu nifafanulie hapo mkuu!!
 
Mkuu wa chuo anamzungumzia Mpinga Kristo na sio Rumi mkuu
Kwanini Uyunani na Umedi na Uajemi walitajwa wazi na Rumi isitajwe?
Mkuu hii hainiingii akilini,kwani Uyunani na Umedi na Uajemi walikuwa na umuhimu mkubwa sana kuliko Rumi?
Au hawakuwa na umuhimu wowote?
 
Sawa mkuu wa chuo naona nimepata maana kamili ya chukizo haribifu..

Je hekalu la Mungu hapa Duniani ambalo atakaa huyo Mpinga Kristo lipo Yerusalem au ni mahali popote wakristo walipokusanyika?

Kwa mtazamo wangu itakuwa pale pale lilipokuwa kabla halijzvunjwa na Warumi!
 
Mkuu wa chuo anamzungumzia Mpinga Kristo na sio Rumi mkuu

Sawa mkuu.. nimemuelewa ndo maana mimi nimetoa maelezo yangu binafsi. Kuwa inawezekana akawa ni mmoja wapo wa Wafalme waliovamia na kuongoza haonwatu kuharibu mji


Kwanini Uyunani na Umedi na Uajemi walitajwa wazi na Rumi isitajwe?
Mkuu hii hainiingii akilini,kwani Uyunani na Umedi na Uajemi walikuwa na umuhimu mkubwa sana kuliko Rumi?
Au hawakuwa na umuhimu wowote?

Yaani ni sawa na Hawa kwanini walionekana wazi. IBRAHIM, MUSA, NUHU, YAKOBO kwa Wayahudi n.k

Lakini YESU hakufunuliwa wazi kwa wayahudi na hawamkubali mpaka kesho. JE IBRAHIM NI MUHIMU KULIKO YESU?

Na mkuu kama unaona hiyo tu haiingii akilini.,.. Je itakuja kuingia akilini kwanini Mungu alificha siku ya Mwisho na hakuna ambaye aijuaye? Ila ametupa alama tu za mwisho utakuwaje katika Ufunuo yote
 
Sasa mkuu wa chuo huyo jamaa atakuwa nani?.... maana Daniel 9 hapo inaonyesha kwamba mkuu atakuja na kuuharibu mji.. Halafu mwenyewe umesema kuwa lilitimia 70AD

Huyo jamaa atakuwa ndio Mpinga Kristo ambaye hadi kwa sasa hajulikani, fungu la 26 katika Daniel 9 hajazungumziwa huyo mkuu ila wamezungumziwa hao Warumi lakini jamaa mwenyewe hajazungumziwa inawezekana hata pia Tito na yeye alikuwa ni mtu wa mkuu yeye sio mkuu... Baada ya Daniel 9:26 kukawa kuna gap

Fungu la 27 Daniel linazungumzia juma la 70 lile la Daniel ambapo halijatimizwa hadi sasa, kwa hiyo huyo mkuu hadi sasa bado hajaja... kwa kifupi hadi fungu la 26 kwa hiyo Daniel yametimia majuma yale 69 tu, na huo mwaka 70 AD ilikuwa ndani ya majuma 69, hadi kwa sasa juma la 70 halijatimia kuna pause kati ya juma la 69 na 70
 
Yaani ni sawa na Hawa kwanini walionekana wazi. IBRAHIM, MUSA, NUHU, YAKOBO kwa Wayahudi n.k

Lakini YESU hakufunuliwa wazi kwa wayahudi na hawamkubali mpaka kesho. JE IBRAHIM NI MUHIMU KULIKO YESU?
Hapana,

Musa,Ibrahimu hawakutabiriwa na nabii yoyote lakini Yesu alitabiriwa

Hivyo mfano wako sio valid!
 
Sawa mkuu wa chuo naona nimepata maana kamili ya chukizo haribifu..

Je hekalu la Mungu hapa Duniani ambalo atakaa huyo Mpinga Kristo lipo Yerusalem au ni mahali popote wakristo walipokusanyika?
Ni Pale Yerusalem ambapo kwa sasa kuna msikiti Dome of the Rock, Msikiti wa Al-aqsa...
 

Mkuu Hebu Angalia hii Daniel tena.. Je hao watu wanawezaje kuja peke yao bila huyo mkuu aliyetajwa

Daniel 9:26

Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa.

Na watu wa mkuu atakayekuja.. Inamaana hao walioharibu hekalu walikuwa na huyo mkuu wao...

Na mimi nijuavyo Mpinga kristo si lazima awe mmoja.. ila Wanaweza wakawa Wengi ila lengo lao ni moja lile lile la kumkana Mungu na Mwanae Yesu Kristo. ..kwahiyo inawezekana hiyo Daniel 9 ilishatimia Kwa huyo mpinga kristo aliyeliongoza jeshi kuharibu Mahali Patakatifu..
 
Ni Pale Yerusalem ambapo kwa sasa kuna msikiti Dome of the Rock, Msikiti wa Al-aqsa...

Ooooh Kwahiyo unahisi ule msikiti utabomolewa in Future? ? Na patajengwa hekalu la Mungu Halafu baadae mpinga Kristo atasimama pale na kujiinua?
 
Last edited by a moderator:
Sasa mkuu kama huyo mkuu atakaekuja ni Mpinga Kristo,mbona waliolivunja hekalu ni watu wa Titus?
Mkuu atakayekuja ameongelewa kwenye fungu la 27 Daniel 9, kwa hiyo Tito na yeye sio mkuu atakakayekuja, na hapo juu nimeonyesha ya kwamba kuna gap kati ya juma la 69 na juma la 70, nafikiri ipo haja ya kukokotoa yale majuma 69 ili kwamba atleast yaeleweke yamepigwa vipi...

Kwa msaada wa Sir Robert Anderson kwenye uzi wetu ule naweza nikawasilisha Hesabu hizo kwenye ule uzi wa Papa sio mpinga kristo, baada ya kupiga hizo hesabu nafikiri tutakuwa tunaenda vizuri sasa mkuu, na unabii unaweza ukawa unaeleweka vizuri sasa...

Hapo ninaweza kuweka nadharia hapo pembe iliyoinuka hapo juu ni mpinga kristo, ambapo aliinuka baada ya hizo pembe kumi Rejea ile concept ya Revived Roman Empire, halafu haya mambo yapo katika time frame ya majuma ya yale 70 na hapo juu nimekueleza kitu kuhusiana na hayo majuma...

Kwasababu kweli ukiangalia kweli hayo uliyosema hapo juu hayajatimizwa...
 

Sasa Mkuu wa chuo ulichosema kimetimia 70AD ni nini kwenye Unabii.. mbna kama wasema na mkuu wa watu atakayekuja kwamba bado hajaja

Halafu wasema tena kwamba Walioharibu Mahali Patakatifu walitimiza 70AD.. wakati stori ya kuharibiwa si kwamba imekatwa katwa ila Watu hao lazima waje na mkuu wao...

Hebu hapa kidogo tujadili
 
Last edited by a moderator:
Ok mkuu,hebu kaweke halafu tuone kama tunaweza kujifunza kitu kwa pamoja
Sasa mkuu,mnyama wa nne wa kwenye Danieli 7 ni nani?

Ni revival Roman au ni ancient Roman Emperor?
 
Na watu wa mkuu atakayekuja hiyo sentensi inazungumzia hao watu na wala haizungumzii huyo mkuu, ila inawakilisha kwamba hao ni watu wa mkuu

Watauangamiza mji na patakatifu hapo inaongelewa wingi wa watu watakaouangamiza huo mji na sio mkuu mwenyewe

Mkuu mwenyewe ni nani sasa!? fungu la 27 linaelezea

Daniel 9:27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.

kwa hiyo mambo yote yanaanzia hapo sasa kwenye hilo fungu la Daniel 9:27, hilo ndio mpinga kristo anaelezewa, ndio maana hata Yesu aliposema mkiona Chukizo la Uharibifu lililonenwa na nabii Daniel alikuwa akirejea hilo fungu la Daniel

Ni kweli pia roho ya mpinga kristo inafanya kazi, lakini mnyama Masihi wa uongo ambae Wayahudi watamkubali kwasababu walimkataa Yesu ni huyo mmoja na wala sio wengi kwa hiyo huyo ndio tunayemzungumzia, hiyo Daniel 9:27 bado sioni kama imetimia...

hiyo kuharibu hapo mahali patakatifu na mji imo ndani ya majuma 69, kwa hiyo juma la 70 hapo bado halijatimia...
 

Hoja nzuri ......!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…