Bunge la Ulaya lapiga kura ya kutowaondoa wamaasai Ngorongoro

Shida ya kujitia kiherehere na mikataba/maazimio ya UN na kuunga mkono kila kitu matokeo ndiyo haya, wenzenu hata The Hague haiwahusu.

Bado tupo zama za Devonshire White Paper (1923),kuamriwa namna ya kufanya mambo.
 
Huu ni utumwa mamboleo!! Yakwao yanawashinda bado wanaleta za kuleta kwetu!
 
Bunge la Ulaya limepiga kura leo ambapo kura 493 zilikubali kuwa wamaasai waachwe katika maeneo yao, 29 zimekubali kuwa wamasai waondolewe huku kura 17 zikiwa ni za wale wasiotaka kusema chochote.
Ina maana Ngorongoro ipo ulaya sio ?
 
Wanatakaje kutufanyia maamuzi, ya kwao mbona yanawashinda kusolve
 
Labla ulayaya kilosa ilakamawazunguwatakuwa wavubangi na mashoga maanahayawahusu
 
Ngoja tuone labda itakuwa kama kesi ya kinamdee,na ccm
 
Bunge la Ulaya limeitaka serikali ya Tanzania kusitisha mara moja uondoaji kwa nguvu wa jamii za Wamasai katika Wilaya ya Ngorongoro nchini humo kutokana na, miongoni mwa sababu nyinginezo, kugeuza maeneo makubwa ya malisho ya asili katika eneo la Loliondo kuwa hifadhi. Akizungumzia umuhimu wa kudhamini kurejea kwa usalama kwa jumuiya hizo, azimio hilo linasisitiza haki yao ya kupata haki na tiba madhubuti kwa waathiriwa. Bunge pia linaitaka serikali ya Tanzania kutambua na kulinda haki za watu wa kiasili na jumuiya za mitaa, na kutambua ardhi na rasilimali ambazo jamii za Wamasai zimesimamia kwa vizazi na nafasi zao katika kudumisha wanyamapori na viumbe hai. Wabunge wanaitaka serikali ya Tanzania kuruhusu taasisi za Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya kutembelea maeneo husika. Pia wanatoa wito kwa Tume ya Ulaya kutoa ripoti kwa Bunge la Ulaya kuhusu programu za msaada wa bajeti ya Umoja wa Ulaya na mipango mingine nchini Tanzania, kwa kuzingatia hasa miradi inayohusu upotevu wa viumbe hai na mabadiliko ya hali ya hewa na ulinzi wa haki za binadamu.

Source: European Parliament
Kwa maelezo zaidi soma link hii: Human rights breaches in Belarus, Tanzania and Tibet | News | European Parliament
 
Nchi tegemezi haina uhuru! Sawa wamasai hawako ulaya lakini wazungu ndio wenye kauli ya mwisho kama watahamishwa au la!! Ndio maana ya kupiga kura.
Upumbavu mtupu. Ya kwao yanawashinda hadi wanaruhusu ndoa za jinsia moja (mwanaume kuoa mwanaume mwezie au mwanamke kwa mwanamke), halafu ndiyo waje watuamulie sisi.

Hawa wamasai wanowatetea wamejaa Mwenge na Ilala wanasuka Rasta ma wengine wanauza sandals na mikanda
 
Matusi hayakusaidii kupata maendeleo bali yanadumaza akili yako!! Uhuru wa bendera ndio lakini kila siku Samia anahaha kutembeza bakuli kila kona ya Dunia!!
Mikopo watatoa tu kwa vile ni biashara ya taasisi za kifedha. Ila wamasai lazima watoke Ngorongoro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…