Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Spika wa Bunge, Mussa Zungu amemuagiza Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi kukutana na Kamati ya Bunge ya Nishati ili kujua hatma ya hali na mwenendo wa kupanda kwa bei ya mafuta nchini.
Zungu amesema kuwa bila mafuta upo uwezekano wa kukwama katika mipango mbalimbali ya nchi.
Hayo yanajiri baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kutangaza bei elekezi mpya za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa zilizoanza kutumika rasmi kuanzia leo Aprili Mosi, 2026, ikiwa ni sehemu ya marekebisho ya kila mwezi yanayozingatia mwenendo wa soko la dunia.
Sababu kuu ya kupanda kwa bei hizo ni mgogoro unaoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati, hususan kati ya Marekani, Israel na Iran, ulioanza Februari 28, 2026 na kuathiri kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa mafuta duniani.