Bunge laagiza kikao cha dharura kujadili kupanda kwa bei za mafuta

Bunge laagiza kikao cha dharura kujadili kupanda kwa bei za mafuta

Haswa, viongozi wa kiaafrika lazima wabadilike, misafara Ile, magari yote yale for what?! Sababu hela hazitoki mifukoni mwao? Ila ni za mlipa Kodi, watuonee huruma basi, na ukitafakari hakuna sababu, umuhimu wala ulazima kuwa na msururu mkubwa kama ule! It's too much benefiting no one apart from misusing public funds!
Hawana habari na nyie mtaishi vipi kwenye mfumuko wa bei...

Wanawaza misafara na posho zao itakuaje?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Spika wa Bunge Letu Tukufu Mheshimiwa Zungu Ameitisha Kikao cha Dharura kwa ajili ya kujadili Mwenendo Mzima wa hali ya upatikanaji wa Mafuta Nchini,bei ya mafuta na hatua za kuchukua kukabiliana na hali hiyo ya Upandaji wa Mafuta katika soko la Dunia.

Hai hiyo inatokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la Dunia kutokana na vita vya Marekani kwa kushirikiana na mshirika wake Israel kufanya mashambulizi ya kijeshi kupitia anga la Iran . Hali iliyopelekea kuuwawa kwa viongozi mbalimbali waandamizi wa Iran wa serikali,kijeshi hadi Raia wa kawaida wasio na hatia.

Lakini pia vita hiyo imepelekea kulipuliwa kwa visima vya mafuta ,maghala ya kuhifadhia mafuta lakini pia kufungwa kwa njia za kusafirisha mafuta kwenda maeneo mbalimbali Duniani.

Ikumbukwe ya kuwa sisi kama Taifa kwa kama zilivyo nchi zingine tumekuwa tukitegemea na kuagiza mafuta kutoka Mashariki ya kati ambako ndiko kulikotokea Vita. Hivyo kama ambavyo sisi ni sehemu ya Watumiaji wa mafuta kutoka kanda hiyo tumejikuta tukipata athari kama ambavyo wengine wameathiriwa kila mmoja kwa kiwango chake.

Hivyo Spika wa Bunge ameagiza kupitia kiti cha Spika kufanyika kwa kikao cha Dharura kati ya Kamati ya Nishati pamoja na wizara ya nishati ili kufanya Tathmini juu ya mambo hayo niliyoyaeleza hapo juu.

Ikumbukwe na kufahamika vyema ya kuwa mafuta Nchini hayajapandishwa na CCM ama serikali ya CCM bali ni soko la Dunia ndio limesababisha hali hiyo. Lakini pia ifahamike ya kuwa sisi hatuna visima vya mafuta wala maghala ya mafuta . Jambo ambalo siyo jinai maana huwezi kuwa na kila kitu hapa Duniani. Na ndio maana tunaishi kwa kutegemeana. Mimi nakupa na kukuletea hiki nawe unanipa na kuniuzia kile ambacho mimi sina ama ninacho kwa kuwango kisicho tosheleza mahitaji yangu.

Kwa hiyo hilo ni suala ambalo lipo nje ya uwezo wetu juu ya upandaji wa mafuta. Lililo ndani ya uwezo wetu katika kukabiliana na hali hiyo ni kuchukua hatua nyingine tu kama vile serikali kuweka Ruzuku katika mafuta kama ambavyo Jemedari wetu hodari na kipenzi chetu Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan alifanya miaka kadhaa iliyopita kwa kutoa Bilioni Mia moja kila Mwezi.

Lakini pia Serikali inaweza kutoa ama kupunguza baadhi ya kodi fulani fulani kwa kipindi fulani cha mpito mpaka pale hali ya bei ya mafuta itakaporejea katika hali yake ya kawaida katika soko la Dunia.

Kikubwa ni kuwa tuwe wavumilivu,watulivu na wenye subira wakati huu huku macho na maskio tukielekeza kwa serikali yetu chini ya uongozi shupavu na madhumuni wa shujaa wetu Mpendwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka, chuma cha reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia na nuru ya Wanyonge.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Kikao cha kwenda kujadili namna ya kuikwamua nchiinaenda kugeuka dili kwa wahusika kuanza kukaa vikao kadha wa kadha huku wakitandika ma-allowances. Siku muafaka unapatikana tayari mafuta yatakuwa yameshuka kwenye soko la dunia mwezi wa 5 katikati
 
Haipo nchi yenye uwezo wa kudeal na soko huria la dunia hususan kwenye soko la mafuta,
hata hivyo, serikali kali sikivu ya CCM, imejipanga kukabiliana kindakindaki na changmoto hiyo, lakini pia kudeal na gharama za maisha ya wananchi wake.

changamoto ya mafuta duniani ni fursa muhimu sana sasa kwa Tanzania kujikita kwenye matumizi ya hazina ya gesi asilia tulionayo kuendesha shughuli za kiuchumi bila kutegemea mafuta pekee.

Yaani miaka yote ya uwepo wa NG hatujaweza kuweka LNG plant, sasa wakati ambapo kuna mzozo wa Mid East ndio tuwe tumebadilika na kujenga faster plant ya LNG?

Kwanza sijui kama unajua kwamba hiyo gesi inayochimbwa sisi kama nchi tunanunua kwa hao hao wazungu wanaoichimba huko baharini pamoja na kwamba inachimbwa kwenye mipaka ya Tanzania...

Namna pekee ya kudeal na mafuta ilikuwa ni kujenga uwezo wa kuhifadhi mafuta kama ambavyo wengine wanafanya kwa sababu suala la mizozo mashariki ya kati na kudestabilize bei za mafuta kunajulikana kwani karibu kila baada ya miaka kadhaa huwa kunachafuka hapo kati...
 
Mbona zungu lenyewe ukilitazama usoni kwa picha kama vile lina stroke? Tutazamie safari ingine karibu nini? My dirty mind
 
IMG-20260403-WA0040.jpg
 
Back
Top Bottom