Bunge laazimia Serikali inunue ndege nyingine kwa ajili ya kuhudumia viongozi

Hawa wabunge wapo hapo kuwakisha shida za wananchi au Mano wanayotaka wao?
Ununuzi wa ndege kwa matumizi yao je ni kipaumbele wakati wananchi wanalia na ugumu wa maisha?
 
“Hali hii husababisha Wakala [wa Ndege za Serikali] kutekeleza jukumu la kuwahudumia viongozi kwa kuchelewa pindi zinapotokea safari za viongozi wote kwa wakati mmoja,” Mhagama anasema.

Hizi sababu hazina mashiko kabisa, kwanini wote wasafiri kwa wakati mmoja ?
 
Bunge la Tanzania limeazimia kuwa Serikali iangalie umuhimu wa kununua ndege nyingine mpya kwa ajili ya kuwahudumia viongozi wakuu wa kitaifa...​
Dah Kweli?

Hii ndo kupunguza maisha kwa Watanzania au Kuongeza mzigo..

Watanzania kwa sasa Hawaitaji ndege za viongozi wanahitaji maisha yao kupungua
 

Kamati ya Bunge yataka Serikali kuongeza ununuzi ndege za viongozi​

Jumanne, Februari 13, 2024


Picha maktaba: Dr. Joseph Kizito Mhagama

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Dk Joseph Mhagama akizungumza wakati akiwasilisha taarifa ya shughuli za kamati hiyo kwa mwaka 2023, leo Jumanne, Februari 13, 2024.
 
Wahuni Hata Serikalini Wapo Hawana Aibu Yaani Wakipanga Lazima
Baadaye Eti Hao Ndiyo Wasomi Wetu Wana Vyeti Tu Ila ....Akili....
Ndege kwa viongozi ni muhimu,imagine mpya kabisa ni ile aliyonunua mkapa,hizo zingine tangu Nyerere,ipo siku watabinuka angani
 
Kwanini Mtanzania ulipe kodi?what for!

Uu mzalendo sana au kitu gani?huduma za afya mbovu,maji hakuna yakitoka yana vumbi umeme ndiyo huo halafu uje uniambie ”Lipa kodi kwa maendeleo ya taifa lako”

Hiyo kodi utalipa wewe mimi silipi.
 
Wanaongeza moja tu zitatosha? Kuongeza moja tu ni uduanzi wa hali ya juu. Ndege za viongozi wakuu zinatakiwa ziwepo nane ili kukidhi mahitaji yao.
 
Hili sio bunge la wananchi bali kundi la vibaka waliookotezwa mitaani na mwendawazimu mwendazake. Hawana uchungu na wananchi wanaoteseka mitaani
 
Huyu Joseph Mhagama ni wajimbo Gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…