Bunge laazimia Serikali inunue ndege nyingine kwa ajili ya kuhudumia viongozi

Huyu jamaa hata upadre ulimshinda mpaka askofu mkuu Norbert Mtega alimrudisha nchini sasa kichwa kama hicho mlitegemea kiseme nini.Huyo jamaa no fisadi sana ana ka NGO kake kanaitwa Ruccodia ndo anakatumia kufanyia ufisadi na kuwatisha wananchi pale jimboni kwake Madaba.
 
Yeah. It makes sense... Wanunue Pilatus Pc-24 moja na Pilatus Pc-12 moja.

Pc -12 (Next generation)is superior in its class! Its a turboprop on jet fuselage (pressurized cabin)! Can land on all airstrips and with five blades on a propeller, it offers a speed of 'super jet'.

Pc-24 has a strength of a regional jets! Can land on all major runways and has a long range allowing it to travel across African continent.

 
Viongozi wa ki-taifa akina Makonda
 

Wanaweza kusafiri na Air Tanzania First or business class au mashirika mengine ya usafiri.

Viongozi wa juu wa Uingereza mara nyingi tu wanatumia commercial flight au hata helkopta za jeshi kusafiri.
 
Lucas anasemaje?
 
Hawa watu hawajali kabisa maisha ya wananchi wanajiangalia wao tu! Magari yao ya kutembelea wanataka ya milioni 500 na sasa wanataka wanunuliwe ndege nyingine mpya lakini tujue wazi hawa jamaa wanafanya yote hayo kwa sababu wameshajiridhisha kwamba Watanzania ni mazuzu hata wafanye nini hatuna cha kuwafanya na watatutesa sana hadi tukome.
 

Yaani tunahangaika na umeme…badala kuwekeza kwenye umeme tupate wa uhakika wanawaza kununua ndege!?

Kwakweli sitakuja piga kura tena.
 
Hamna njia nyingine ya kula keki ya nchi kama hautapambana na kuinuka kiuchumi. Tutalia weeeeeeeee na kutukana lakini hiyo ndio suluhisho. Angalao unabiashara na wewe una enjoy kukwepa na Kodi angalao maumivu yatapungua lakini kuendelea kulalama tutabakia kulalama na ubaya zaidi hata kudai haki tunadai mitandaoni
 
Hakuna bunge hapo ni genge la wahuni tu
 
Dah badala wapambane jinsi ya kupunguza mfumko wa bei, wao wanajiwazia wao tu. Wanahudumiwa kila kitu, hizo ndege za nini.
 
Madhara ya bunge kuhodhiwa na Chama kimoja ndio haya.

Yule aliyevuruga uchaguzi wa 2020 alitukosea sana.
 
Kuna mtu anasemaga CCM ni kansa sijui kwanini hatumuelewagi
 
Yaani tunahangaika na umeme…badala kuwekeza kwenye umeme tupate wa uhakika wanawaza kununua ndege!?

Kwakweli sitakuja piga kura tena.
Piga kura ya kuwaondoa wahuni. Pigania kipatikane chama kipya cha kuwatetea Wananchi.
 
Tatizo sio nchi, ila walioidhibiti wameshachoka hawana jipya tena.
Kuna ukweli, ila shida inaanzia kwetu, sisi tushajivika unyonge, tuliowakabidhi madaraka wanajiona wao ni maMAMBA.
Wameshatuona sisi ni mazumbukuku ndio maana wanatuletea mambo ya kiFALA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…