Kwa mujibu wa Kanuni ya # Bunge 84 (3) (a) za mwaka 2023 amekutwa na hatia na Kamati ya Hadhi na Madaraka ya Bunge.
Tuendelee kufuatilia bunge
≈=====================
"Mheshimiwa Luhaga Mpina (Mbunge wa Kisesa) alimtuhumu Mheshimiwa Waziri (Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo) kuwa amelidanganya Bunge kwa kusema wamebadili kanuni za Nation Food Reserve Agency (NFRA) kuruhusu NFRA kuwa na mandate ya kuingiza sukari wakati hakuna tangazo la serikali lililotangazwa kuipa NFRA mandate ya kuingiza sukari, Waziri (Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo) aliieleza kamati kuwa walitumia sheria ya usalama wa chakula sura ya 249 kukabiliana na uhaba wakati wa dharura kupitia NFRA ambapo alisema kuwa wameanza mchakato wa kubadilisha sheria ili NFRA waruhusiwe kuagiza, kuhifadhi na kusambaza sukari hata kwa kipindi kisicho cha dharura na mchakato huo ulianza kwa kutoa tangazo serikalini namba 225 (b) la tarehe 01 Aprili 2024" -Makoa
"Kamati ilipitia kifungu cha 14 cha sheria ya tasnia ya sukari kuhusu wanaoruhusiwa kuingiza sukari na kupitia kifungu cha 15 cha sheria ya usalama wa chakula ya mwaka 1991 na kubaini kuwa wakati wa dharura kama ilivyojitokeza sheria ya usalama wa chakula inakuwa na nguvu zaidi kuliko sheria ya tasnia ya sukari" -Makoa
"Kamati ilipata nafasi ya kujiridhisha kuhusu GN namba 25 (b) ya tarehe 01 Aprili 2024 na kupitia muswada wa sheria ya fedha iliona mapendekezo ya marekebisho yaliyoelezwa na Waziri kupitia kumbukumbu za Bunge na maelezo ya Waziri kamati ilikuwa na maoni kuwa hakuna uwongo uliozungumzwa na kwamba hakuna ukiukwaji wowote wa sheria uliofanywa" -Makoa
Ni sehemu ya maelezo ya Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki, maadili na madaraka ya Bunge Ally Makoa akiwasilisha Bungeni kuhusu tuhuma zilizotolewa na Mbunge wa Kisesa (CCM) Luhaga Mpina dhidi ya Waziri wa Kilimo Hussein Bashe
View attachment 3024970