Bunge lajadili juu ya adhabu ya Mbunge Luhaga Mpina. Laamua kumfungia vikao 15

baada ya kubuni uongo na uzushi, kana kwamba ni kweli na kuufanya kama tuhuma dhidi ya waziri kijana wa kilimo, mchapakazi hodari na anaeaminika sana, Hussein Bashe, na kujaribu kuwahadaa wananchi na kutaka kulidanganya bunge..

Mbunge huyo mzushi, atawajibika kutokukanyaga kabisa eneo la bunge katika muda usiopungua vikao15, hiyo maana yake atakanyaga tu, tana kwa bahati sana vikao vya bunge la November 2024.

Je,
CCM itavumilia Kuishi na mtu muongo na mzushi kama huyu?

au ni suala la muda tu tutapata taarifa ya Tume Huru Ya Uchaguzi ikiliarifu bunge hatua za CCM dhidi ya mbunge wake huyo muongo 🐒

uzushi, uongo, kiburi na jeuri vyamtokea puani, aweka ubunge wake rehani na uko mashakani kumponyoka 🐒
Chawa katika ubora wako
 
Sema machawa wamefanya naiona JF kwa upande wa habari na mijadala ya siasa kama inashuka hadhi yake ile ya kuwa platform ya great thinkers. Inakuwa sasa kama ni uwanja wa comedy au matani ya kulazimisha. Anyway, najua machawa watakaza mafuvu tu.
 
H
baada ya kubuni uongo na uzushi, kana kwamba ni kweli na kuufanya kama tuhuma dhidi ya waziri kijana wa kilimo, mchapakazi hodari na anaeaminika sana, Hussein Bashe, na kujaribu kuwahadaa wananchi na kutaka kulidanganya bunge..

Mbunge huyo mzushi, atawajibika kutokukanyaga kabisa eneo la bunge katika muda usiopungua vikao15, hiyo maana yake atakanyaga tu, tana kwa bahati sana vikao vya bunge la November 2024.

Je,
CCM itavumilia Kuishi na mtu muongo na mzushi kama huyu?

au ni suala la muda tu tutapata taarifa ya Tume Huru Ya Uchaguzi ikiliarifu bunge hatua za CCM dhidi ya mbunge wake huyo muongo 🐒

uzushi, uongo, kiburi na jeuri vyamtokea puani, aweka ubunge wake rehani na uko mashakani kumponyoka 🐒
Ila huu mwandiko huu, mmmmh.. unafanana na wa jamaa flani ivi hapa hapa jukwaani 😂. Machawa wako busy sana aisee..
 
Kamati Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge imewasilisha bungeni taarifa ya kamati hiyo kuhusu tuhuma za Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, jijini Dodoma leo Juni 24, 2024

Mbunge wa Mtera, Livingstone Joseph Lusinde amesema kutokana na tuhuma zinazomkabili Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kuhusu kumtuhumu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kuwa alilidanganya Bunge kuhusu sakata la Uagizaji wa Sukari, anatakiwa kufungiwa kuhudhuria vikao 15 vya Bunge

Ameyasema hayo Bungeni baada ya Mwenyekiti wa Kamati Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge, Ally Makoa kuwasilisha Bungeni Taarifa ya Kamati kuhusu tuhuma hizo, leo Juni 24, 2024
---
"Mheshimiwa Luhaga Mpina (Mbunge wa Kisesa) alimtuhumu Mheshimiwa Waziri (Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo) kuwa amelidanganya Bunge kwa kusema wamebadili kanuni za Nation Food Reserve Agency (NFRA) kuruhusu NFRA kuwa na mandate ya kuingiza sukari wakati hakuna tangazo la serikali lililotangazwa kuipa NFRA mandate ya kuingiza sukari, Waziri (Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo) aliieleza kamati kuwa walitumia sheria ya usalama wa chakula sura ya 249 kukabiliana na uhaba wakati wa dharura kupitia NFRA ambapo alisema kuwa wameanza mchakato wa kubadilisha sheria ili NFRA waruhusiwe kuagiza, kuhifadhi na kusambaza sukari hata kwa kipindi kisicho cha dharura na mchakato huo ulianza kwa kutoa tangazo serikalini namba 225 (b) la tarehe 01 Aprili 2024" -Makoa

"Kamati ilipitia kifungu cha 14 cha sheria ya tasnia ya sukari kuhusu wanaoruhusiwa kuingiza sukari na kupitia kifungu cha 15 cha sheria ya usalama wa chakula ya mwaka 1991 na kubaini kuwa wakati wa dharura kama ilivyojitokeza sheria ya usalama wa chakula inakuwa na nguvu zaidi kuliko sheria ya tasnia ya sukari" -Makoa

"Kamati ilipata nafasi ya kujiridhisha kuhusu GN namba 25 (b) ya tarehe 01 Aprili 2024 na kupitia muswada wa sheria ya fedha iliona mapendekezo ya marekebisho yaliyoelezwa na Waziri kupitia kumbukumbu za Bunge na maelezo ya Waziri kamati ilikuwa na maoni kuwa hakuna uwongo uliozungumzwa na kwamba hakuna ukiukwaji wowote wa sheria uliofanywa" -Makoa

Ni sehemu ya maelezo ya Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki, maadili na madaraka ya Bunge Ally Makoa akiwasilisha Bungeni kuhusu tuhuma zilizotolewa na Mbunge wa Kisesa (CCM) Luhaga Mpina dhidi ya Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.

WABUNGE WAKUBALIANA KUMFUNGIA MPINA VIKAO 15 VYA BUNGE
Luhaga Mpina, Mbunge wa Kisesa amefungiwa kuhudhuria vikao 15 vya Bunge kuanzia Juni 24, 2024 kwa kosa la kukiuka Kanuni za Bunge, kudharau Mamlaka ya Spika na mwenendo wa shughuli za Bunge, atarejea Bungeni katika kikao cha pili cha Novemba, 2024

Mpina ametiwa hatiani baada ya kuzungumza na Wanahabari kuhusu ushahidi aliouwasilisha kwa Spika kabla ushahidi huo haujawasilishwa mezani au kupewa idhini na Bunge kufanya hivyo

Awali, Mpina alidai Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alilidanganya Bunge kuhusu Uagizaji wa sukari Nchini

Spika wa Bunge, Tulia Ackson amesema Mpina hatakiwi kufika eneo la Bunge wala kujihusisha na shughuli zozote za Bunge wakati wa adhabu yake

PIA SOMA
- Spika Tulia amburuza Luhaga Mpina Kamati ya Maadili

- Luhanga Mpina apewa siku 10 na Spika kuleta ushahidi wa Bashe kulidanganya Bunge

- Luhaga Mpina: Usambazaji wa sukari haukuwa ukifanywa na mfanyabiashara mmoja wa Mwanza pekee, Waziri Bashe alidanganya

- Luhaga Mpina amshukia Waziri Bashe, adai amelidanganya Bunge, awataja Magufuli, Rais Samia

Walimpa mpina nafasi ya kujibu hoja za wabunge?

Ama ndiyo alishambuliwa kisha wakahukumu.
 
Kama Mpina kaadhibiwa na bunge basi alisema ukweli; Bashe alilidanganya bunge.
 
Luhaga hawezi kuhamia upande wa maumivu (upinzani), maana ana madhambi mengi sana. Akithubutu kutoka atasulibiwa vibaya sana.

Ana ranch ya mifugo yake yenye ukubwa wa vijiji 3 ,alipora ardhi yawatu wa Morogoro.....atanyang"anywa.

Mnakumbuka yaliyompata Sumaye?
Mnakumbuka yaliyompata Wema Sepetu.
Mnakumbuka yaliyompata Lowasa?
 
Hivi ushahidi kumbe unapaswa kuwa siri? Mtu kaamua kusema hiki ndicho nakiwasirisha sasa yeye spika alikuwa na hofu gani?
 
Kutohudhuria Vikao tu huku ukiendelea na majukumu Yako ya Kibunge Jimboni ni advantage wakati huu tunapoelekea Uchaguzi mkuu

Nakumbuka mbunge wa Rorya yule Lakairo aliwahi kusema kushinda bungeni wakati unahitajika jimboni ni kupoteza Muda

Aziz na Mkono ndio walikuwa hawahudhurii kabisa bungeni hata yule Mo Dewji wa Makolo

Hii Adhabu labda kwa Wabunge wa Upinzani wanaotegemea Posho kupeleka Watoto shule

Kanuni za Adhabu ziangaliwe upya

Mlale unono 😃😃😃

PIA SOMA

- News Alert: - Bunge lajadili juu ya adhabu ya Mbunge Luhaga Mpina. Laamua kumfungia vikao 15
 
Luhaga Mpina, Mbunge wa Kisesa amefungiwa kuhudhuria vikao 15 vya Bunge kuanzia Juni 24, 2024 kwa kosa la kukiuka Kanuni za Bunge, kudharau Mamlaka ya Spika na mwenendo wa shughuli za Bunge, atarejea Bungeni katika kikao cha pili cha Novemba, 2024
-
Mpina ametiwa hatiani baada ya kuzungumza na Wanahabari kuhusu ushahidi aliouwasilisha kwa Spika kabla ushahidi huo haujawasilishwa mezani au kupewa idhini na Bunge kufanya hivyo
-
Awali, Mpina alidai Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alilidanganya Bunge kuhusu Uagizaji wa sukari Nchini

-
 
Kwa mujibu wa Kanuni ya Bunge #84 (3) (a) ya mwaka 2023 amekutwa na hatia na Kamati ya Hadhi na Madaraka ya Bunge.

Tuendelee kufuatilia bunge
≈=====================

"Mheshimiwa Luhaga Mpina (Mbunge wa Kisesa) alimtuhumu Mheshimiwa Waziri (Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo) kuwa amelidanganya Bunge kwa kusema wamebadili kanuni za Nation Food Reserve Agency (NFRA) kuruhusu NFRA kuwa na mandate ya kuingiza sukari wakati hakuna tangazo la serikali lililotangazwa kuipa NFRA mandate ya kuingiza sukari, Waziri (Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo) aliieleza kamati kuwa walitumia sheria ya usalama wa chakula sura ya 249 kukabiliana na uhaba wakati wa dharura kupitia NFRA ambapo alisema kuwa wameanza mchakato wa kubadilisha sheria ili NFRA waruhusiwe kuagiza, kuhifadhi na kusambaza sukari hata kwa kipindi kisicho cha dharura na mchakato huo ulianza kwa kutoa tangazo serikalini namba 225 (b) la tarehe 01 Aprili 2024" -Makoa

"Kamati ilipitia kifungu cha 14 cha sheria ya tasnia ya sukari kuhusu wanaoruhusiwa kuingiza sukari na kupitia kifungu cha 15 cha sheria ya usalama wa chakula ya mwaka 1991 na kubaini kuwa wakati wa dharura kama ilivyojitokeza sheria ya usalama wa chakula inakuwa na nguvu zaidi kuliko sheria ya tasnia ya sukari" -Makoa

"Kamati ilipata nafasi ya kujiridhisha kuhusu GN namba 25 (b) ya tarehe 01 Aprili 2024 na kupitia muswada wa sheria ya fedha iliona mapendekezo ya marekebisho yaliyoelezwa na Waziri kupitia kumbukumbu za Bunge na maelezo ya Waziri kamati ilikuwa na maoni kuwa hakuna uwongo uliozungumzwa na kwamba hakuna ukiukwaji wowote wa sheria uliofanywa" -Makoa

Ni sehemu ya maelezo ya Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki, maadili na madaraka ya Bunge Ally Makoa akiwasilisha Bungeni kuhusu tuhuma zilizotolewa na Mbunge wa Kisesa (CCM) Luhaga Mpina dhidi ya Waziri wa Kilimo Hussein Bashe

PIA SOMA
- LIVE - Bunge lajadili juu ya adhabu ya Mbunge Luhaga Mpina

View attachment 3024970
Baseline hapa ni;.. Je sukari baada ya kuagizwa kwa vibali (kwa maana ya wafanyibiashara kusamehewa mabilioni ushuru) ilipatikana kwa bei nafuu kwa wananchi au la? tuache details zingine hizo hadi kumgeuza mtuhumu kua mtuhumiwa nakumuadhibu yeye.
Kwa hakika sasa nchi imegeuka mwanasesere wa maslahi ya mabepari uchwara wa nchini au tuseme wafanyibiashara wakubwa.
 
Kwa mujibu wa Kanuni ya Bunge #84 (3) (a) ya mwaka 2023 amekutwa na hatia na Kamati ya Hadhi na Madaraka ya Bunge.

Tuendelee kufuatilia bunge
≈=====================

"Mheshimiwa Luhaga Mpina (Mbunge wa Kisesa) alimtuhumu Mheshimiwa Waziri (Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo) kuwa amelidanganya Bunge kwa kusema wamebadili kanuni za Nation Food Reserve Agency (NFRA) kuruhusu NFRA kuwa na mandate ya kuingiza sukari wakati hakuna tangazo la serikali lililotangazwa kuipa NFRA mandate ya kuingiza sukari, Waziri (Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo) aliieleza kamati kuwa walitumia sheria ya usalama wa chakula sura ya 249 kukabiliana na uhaba wakati wa dharura kupitia NFRA ambapo alisema kuwa wameanza mchakato wa kubadilisha sheria ili NFRA waruhusiwe kuagiza, kuhifadhi na kusambaza sukari hata kwa kipindi kisicho cha dharura na mchakato huo ulianza kwa kutoa tangazo serikalini namba 225 (b) la tarehe 01 Aprili 2024" -Makoa

"Kamati ilipitia kifungu cha 14 cha sheria ya tasnia ya sukari kuhusu wanaoruhusiwa kuingiza sukari na kupitia kifungu cha 15 cha sheria ya usalama wa chakula ya mwaka 1991 na kubaini kuwa wakati wa dharura kama ilivyojitokeza sheria ya usalama wa chakula inakuwa na nguvu zaidi kuliko sheria ya tasnia ya sukari" -Makoa

"Kamati ilipata nafasi ya kujiridhisha kuhusu GN namba 25 (b) ya tarehe 01 Aprili 2024 na kupitia muswada wa sheria ya fedha iliona mapendekezo ya marekebisho yaliyoelezwa na Waziri kupitia kumbukumbu za Bunge na maelezo ya Waziri kamati ilikuwa na maoni kuwa hakuna uwongo uliozungumzwa na kwamba hakuna ukiukwaji wowote wa sheria uliofanywa" -Makoa

Ni sehemu ya maelezo ya Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki, maadili na madaraka ya Bunge Ally Makoa akiwasilisha Bungeni kuhusu tuhuma zilizotolewa na Mbunge wa Kisesa (CCM) Luhaga Mpina dhidi ya Waziri wa Kilimo Hussein Bashe

PIA SOMA
- LIVE - Bunge lajadili juu ya adhabu ya Mbunge Luhaga Mpina

View attachment 3024970
Hukum za bunge hazitoi mda wa mtuhumiwa kujitetea?

Kwanin hawajaamua kuzifatilia taarifa zake ili mtuhumiwa nae apewe adhabu yake?
 
Vp na wale kwenye ripoti ya mkaguzi
Ripoti ya uchunguzi wa kamati umebainisha kwamba gentleman wa Kisesa ni mzushi na muongo amelidanganya bunge na kumdharau spika 🐒

ripoti gani tena unauliza gentleman 🐒
 
Back
Top Bottom