Bunge lakanusha Kauli ya Mbowe kuwa Mshahara wa Wabunge umepanda kutoka Tsh Milioni 13 hadi 18

Bunge lakanusha Kauli ya Mbowe kuwa Mshahara wa Wabunge umepanda kutoka Tsh Milioni 13 hadi 18

Maneno ya kukana hoja Hizo yametolewa na Kitengo cha mawasiliano na uhusiano wa kimataifa Bungeni..

Jana Ijumaa tarehe 22 Machi, 2024 alipokuwa anahutubia mkutano wa hadhara Mjini Babati Mkoa wa Manyara na kisha Video yake kusambaa kwenye Mitandao ya Kijamii Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe amedai kwamba mishahara ya Waheshimiwa Wabunge imeongezwa mwaka 2023 kutoka shilingi milioni kumi na tatu (sh.13,000,000/=)
hadi shilingi milioni kumi na nane (sh.18,000,000/=)

View attachment 2942304
Bunge limetudanganya. Mbowe hajawahi kusema nyongeza ya mshahara bali alisema kuhusu nyongeza ya marupurupu na posho za wabunge. Siku zote wabunge wamekuwa wakilipwa mshahara kidogo sana na kujilipa maposho na marupurupu kufuru. Na hapa ndipo serikali ya kifisadi ya CCM inapopiga fedha za umma. Nchi hii ina mijitu ya ajabu sana. Ni bora hata ife ili nchi ipate kupona. Mipuuzi mikubwa!
 
Salary sio milion 13,

Ila maokoto Yao yote ukichanganya ni 13 Kwa mwezi
Vyovyote ilivyo kwa hela hiyo na wanachokifanya hao watu hiyo ni hela nyingi haiwastahili,kugonga gonga meza na kujifanya wanasema shida za wananchi ambazo in reality huwa hazitekelezwi kwa sababu ni wao wamezisema huo ni mshahara mkubwa mno.

Hii nchi siku tukiwa na akili tutagundua kwamba hatukuhitaji wabunge wapiga makofi bungeni ila kama kulikuwa na umuhimu wa watu kulipwa vizuri ilibidi wawe wenyeviti wa vijiji,madiwani na viongozi wa serikali za mitaa kwa sababu wao ndiyo wanakutana moja na wananchi then wao wanawasilisha kero zetu kwa wakuu wa wilaya na mikoa ambao ni wateule wa raisi wanaoripoti kwake moja kwa moja tofauti na sasa wapo watu wanalipwa hela nyingi na hata kusema hizo kero za wananchi hawazisemi na hata zikisemwa siyo kwa undani ule kama angeulizwa diwani au viongozi wengine wa vijiji.
 
Maneno ya kukana hoja Hizo yametolewa na Kitengo cha mawasiliano na uhusiano wa kimataifa Bungeni..

Jana Ijumaa tarehe 22 Machi, 2024 alipokuwa anahutubia mkutano wa hadhara Mjini Babati Mkoa wa Manyara na kisha Video yake kusambaa kwenye Mitandao ya Kijamii Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe amedai kwamba mishahara ya Waheshimiwa Wabunge imeongezwa mwaka 2023 kutoka shilingi milioni kumi na tatu (sh.13,000,000/=)
hadi shilingi milioni kumi na nane (sh.18,000,000/=)

View attachment 2942304
Taarifa za kupanda Kwa mishahara ya wabunge zimeletwa Chadema na wabunge wa CCM.
Mnajikaanga wenyewe
 
Hii taarifa ya kijinga kwenda kwa wajinga.
Taarifa yenye weledi inatakiwa ioneshe mshahara sahihi kwa wakati huu (Mbowe alisema 18m ambapo ukweli ni .......).
Hata hivyo, kwa sababu ya mabadliko ya fikra na teknolojia, siku si nyingi mambo kama haya hayatakuwa siri tena.
Waseme wananchi wahamaki 😅😅
Na bungeni kusikalike?
 
Lying is just taking advantage of present time(s), situation and circumstances to hide the truth. However, at the same time, it is taking risk when those times, circumstances and situation have changed or no longer exist.

Tusubiri.
Yeah
 
Wanajionaga wao ndo wanaakili nasisi ni wakudanganywa kipuuzi??! Mbowe ashindwe kumuuliza hata Mdee walivyo washkaji!!
Hii nchi Maviongozi hawana huruma ndomana wakianza kumsifu mkuu wao wanatumika nguvu zao zooote!! Unashangaa kunamaskini nao husifu hovyo
Milioni 18 huku watoto na walimu wao wanaanguka njaa kwakukosa chakula shuleni alafu mpuuzi anakwambia mama anaupigia mwingi
 
Hata kama ni milioni kumi na tatu jumla na marupurupu ni fedha nyingi mnoooo mnooo!Kwa kazi gani hasa wanayoifanya?Nchi ya ajabu mnooo.Kuna watu tukiwaangalia mule bungeni hawapaswi kuwemo.Kwa mfano yule na huyu na hata wale(...?) ingawa tunaita ni haki na demokrasia bila ubaguzi.
 
Fedha za wabunge ni nyingi sana hata kama bunge limekanusha. Ili kupunguza gharama za kukaa Dodoma muda mwingine vikao vingekuwa vinafanyika kwa 'Zoom' tu. Huwezi ukasema una Mbunge darasa la Saba eti yupo Dodoma anatunga sheria huo ni utapeli.
 
Bunge.jpg

Jana ljumaa tarehe 22 Machi, 2024 alipokuwa anahutubia mkutano wa hadhara Mjini Babati Mkoa wa Manyara na kisha Video yake kusambaa kwenye Mitandao ya Kijamii Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe amedai kwamba mishahara ya Waheshimiwa Wabunge imeongezwa mwaka 2023 kutoka shilingi milioni kumi na tatu (sh.13,000,000/=) hadi shilingi milioni kumi na nane (sh.18,000,000/=).

Tunapenda kuujulisha umma kwamba madai hayo ni uzushi na upotoshaji kwa kuwa hakuna Mbunge aliyeongezewa mshahara kama alivyodai. Hivyo, tunapenda kuwashauri na kuwasihi wananchi kupuuza madai hayo ambayo lengo lake ni kuleta taharuki pamoja na kuwagombanisha wananchi na wawakilishi wao.

Nyongeza ya mshahara ni suala linalozingatia bajeti na hakuna utaratibu wa aina yoyote kama huo ambao umefanyika kwa ajili ya kuwaongezea Waheshimiwa Wabunge mishahara.

Imetolewa na:-
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa
Ofisi ya Bunge, 10 Barabara ya Morogoro
S.L.P 941, 40490
Tambukareli, DODOMA.

23 Machi, 2024

Kauli ya Mbowe soma hapa - Mbowe: Wabunge wamejiongezea Mishahara Kutoka Tsh milioni 13 za awali na sasa wanalipwa Tsh milioni 18 kwa mwezi mbali na posho
 
Jtatu wampeleke mahakamani kwa kosa la kupotosha umma, ili ukweli ukajulikane.
 
Hata kama ni milioni kumi na tatu jumla na marupurupu ni fedha nyingi mnoooo mnooo!Kwa kazi gani hasa wanayoifanya?Nchi ya ajabu mnooo.Kuna watu tukiwaangalia mule bungeni hawapaswi kuwemo.Kwa mfano yule na huyu na hata wale(...?) ingawa tunaita ni haki na demokrasia bila ubaguzi.
Hela za wajinga lazima ziliwe mkuu, unashangaa hizo ndogo hivyo tukikuambia zingine si utazimia.
 
Back
Top Bottom