Bunge lapitisha Muswada unaotaka wake wa Marais na Maspika wastaafu kulipwa kiinua mgongo

Pamoja na maudhi yote haya ya serikali ya ccm...watu wapo usingizini huku wakiota ndoto za kutisha(mabomu ya machozi, kupigwa na polisi, n.k)

Watanzania ni kama mazombi....waboreshee tu SIMBA na YANGA wahangaike nazo, mengine yaliyobaki utajua mwenyewe!
 
Kwenye kipindi hiki kigumu,ni kweli kuna ulazima wa kuongeza gharama za kuendesha serikali!?
Ma CCM, yanamuonea huruma mke wa waziri mkuu! Ambaye kwanza anabiashara zake, harali na haramu, watoto wapo sekta nyeti,
Akaunti imenona! Kwanini hii huruma wasipewe vijana wanaomaliza vyuo na kukosa ajira, vijana wapewe hata 400K, kwa mwezi! Ili kukidhi, mahitaji Yao, mpaka watakapo pata ajira,
 
Hii ndo Tanzania,watu wake bado wamelala usingizi wa mzito!Eti tunaogopa mabadiliko ya utawala kwamba kutatokea vita,aisee
 
Wanazolipwa waume zao haziwatoshi??
Ikiwa hivyo basi iwe kwa Watumishi wote Nchi nzima,tuache kuwa biased.
What are the so special??
 
hapa anatafutwa Mume wa Spika (Tulia) apigwe Chini Ewura maana Afu afarijiwe na mafao ya Mwenza
 
Ni jambo jema saaana, ila lingekuwa jema zaidi na zaidi kama wangepeleka na mswaada wa kuwashitaki pindi wanapomaliza mda wao na wakawa wameenda kinyume na matakwa ya katiba pindi wawapo madarakani.

Ila kwa kwa kuwa kazi ya bunge ni kutunga sheria na ili uwe mbunge sifa moja wapo ujue tu kusoma nakuandika basi sawa wacha tuendelee hivi hivi mpaka watakapoamka waliolala.
 
Kutokana na kuwa suala ni wenza na kiinua mgongo, nadhani kila mwenza wa mtumishi anastahili gawana hii keki ya taifa mfano waalimu, maaskari, mesenja, mhudumu nk. Lakini kwa kutumia busara na hali ya uchumi na nchi kutegemea mikopo kujiendesha hata katika matumizi ya msingi sidhani ni muda muafaka kwa jambo hili kutekelezeka kwa sasa labda kama ni kutojali uhalisia na kodi za wananchi wenye kipato kidogo ambacho hakitoshi hata milo mitatu.
 
...Uzuri ni Kwamba Wataziacha hapa hapa Duniani !! Kama itavyokuwa Kwa Masikini...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…