Bunge lapitisha Muswada unaotaka wake wa Marais na Maspika wastaafu kulipwa kiinua mgongo

Hii nchi aliyenacho huongezewa asienacho hupokwa zaidi.
Bunge limepokea msaada na kuupitisha ili wenza wa viongozi wastaafu walipwe mafao ya kustaafu. Sio vibaya kwa kuwa hoja ina mashiko kwa wahusika na ilitolewa na mmoja wa wanufaika aliomo bungeni.
Wananchi wa kawaida waliofanya kazi na kustaafu hadi leo wanapigania haki zao za madai ya kustaafu lakini hawajalipwa na bunge inalijua hili. Serikali inalijua lakini wazee hawa wanyonge hawana mtu wa kuwasimania na kuhakikisha wanalipwa. Hivi kweli hii ndio Tanzania waliyoiacha mwl. Nyerere na Karume. Mbona wenye sauti hawa wajali wanyonge.
Bunge na Serikali simamieni haki wazee wastaafu na wasio na wakuwasimania walipwe haki zao za madai ya kustaafu.

Sent from my Infinix X657C using JamiiForums mobile app
 
Wanasema hao tayari washachukua chao mapema kwenye mikopo ya elimu yajuu hivyo ukiwapa tena nchi itaingia hasara
 
Upumbavu wa Bunge na Watawala unaenda kuwabebesha mzigo mzito walipakodi ambao hawana maji na umeme wa uhakika wala huduma bora za afya.


Hii ndiyo CCM ambayo imeamua kufanya itakavyo kwa sababu inaamini inaongoza mazuzu.

Haya ndo yanayoenda kuiangusha muda si mrefu kwenye sanduku la kura
 
Watu wanalipa tozo mbalimbali, wanalipa kodi mbalimbali, hali ni ngumu, maisha yamewapiga Watanzania.

Badala ya Serikali kuleta muswada wa kubana matumizi yasiyo ya lazima ili kuwapa unafuu Watanzania, yenyewe inaleta muswada wa kuzigawa fedha za Watanzania kwa kikundi kidogo cha watu ambacho hata hivyo kimekuwa kikifaidi mema ya Nchi kwa muda mrefu kabisa.

Mungu mwenye enzi, nguvu na uweza wa ajabu aingilie kati suala hili. Tunaodhani wangekuwa msaada kwa Wananchi, hao ndo wanakuwa GENGE la majizi na mafisadi.

Wabunge nao wakiamua tu, wanajiongezea posho na marupurupu ya kila aina.

Allah Akbar.
 
Wanapeana tu ulaji ****nina zao.
 
Luka 19:26
“Akawajibu, ‘Nawaambia kwamba kila aliye na kitu, ataongezewa. Lakini yule asiye na kitu, hata alicho nacho atanyangʼanywa.
 
Hii ingelitufanya wtanxania tuasi nchi, lkn tumelala ndiyo maana wanafanya watakavyo
 
Mtu akiwa kiongozi Tanzania huamini yeye ana akili kuliko yeyote yule na ndio mwenye haki kuliko raia yeyote yule na mali asili yeyote ile ambayo iko chini yake hiyo ni mali yake.
 
Taifa la Tanzania halihitaji hawa wanasiasa kukomboa watu bali linahitaji sasa nguvu ya umma itakayowapiga ambush maharamia waliojitwalia Taifa hili na kulifanya mali yao binafsi.

Ukombozi utakaofanyika ndio utaleta tija na heshima tuitakayo wote kama watanzania,
 
Andika vizuri kwamba sio sawa kutoa mafao Kwa wenzao wa Viongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…