Bunge liitishe kikao cha dharura kujadili kufungwa kwa ubalozi wa Denmark 2024

Mawazo ya kichadema. Ovyo sana..eti bunge lijadili kwa nini denmark wafunge ubolozi. Kwanza wamesema wanafunga ofisi ya ubalozi sio kuvunja uhusiano. Ni maamuzi yao sisi hatuwezi lazimisha. Bila shaka baada ya hapo watawakilishwa na nchi nyingine. Siku uingereza wakisema wanafunga ubalozi sijui hao vibaraka wa chadema watasemaje. Wanaweza hata kusema serikali ijiuzulu ufanyike uchaguzi upya 😂😂. Wakongwe watakumbuka nchi hii iliwahi kuvunja uhusiano na uingereza kwa kuwasaidia walowezi wa rhodesia kwa miaka karibu au zaidi ya kumi na nchi ikaendelea kuwepi bila shida. Kushikwa kiwewe kutokana na uwezekano wa kukosa misaada ndio kitu kinawapa shida vibaraka. Misaada ambayo wala haijaisaidia nchi kutoka kwenye umaskini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…