Bunge likutane haraka kuondoa ukomo wa mgombea Urais Tanzania

Bunge likutane haraka kuondoa ukomo wa mgombea Urais Tanzania

Ni wakati mwafaka Bunge letu tukufu likutane ili lipitishe uondoaji wa kikomo kugombea urais, ile miaka kumi sasa isiwepo. Kama mtu anafaa na hali inamruhusu aendelee milele hadi kifo kitakapomuondoa.

Lakini hapa pia litayarishe Tume huru japo kutakuwa na jamaa wenye mkono mkono, ila ikubalike na Wapinzani wote.
fisadi anayenufaika na MFUMU HUUBWA SASA WA UONGOZI

HATUTAKI HATUTAKI NA HATUTAKI KABISA MAANA HATA YEYE TULIKUWA HATUMJUI ILA TUKAMPATA TUTAPATA MWINGINE TU
 
Ni wakati mwafaka Bunge letu tukufu likutane ili lipitishe uondoaji wa kikomo kugombea urais, ile miaka kumi sasa isiwepo. Kama mtu anafaa na hali inamruhusu aendelee milele hadi kifo kitakapomuondoa.

Lakini hapa pia litayarishe Tume huru japo kutakuwa na jamaa wenye mkono mkono, ila ikubalike na Wapinzani wote.
"Alisikika Mhe. Mkamia Maji akisema hivyo"
 
Naomba maoni yako kwenye hili mkuu
Nilishatoa maoni yangu hapo kabla labda nirudie tu kwa faida yako.

Maoni yangu ni kama ulivyokuwa msimamo wa Dr. Magufuli, hataongeza zaidi ya hapa.

Naamini hataongeza, na pia namshauri asisikilize ushauri wa namna hii, kabisa kabisa.
 
Ni wakati mwafaka Bunge letu tukufu likutane ili lipitishe uondoaji wa kikomo kugombea urais, ile miaka kumi sasa isiwepo. Kama mtu anafaa na hali inamruhusu aendelee milele hadi kifo kitakapomuondoa.

Lakini hapa pia litayarishe Tume huru japo kutakuwa na jamaa wenye mkono mkono, ila ikubalike na Wapinzani wote.

viva udikteta 😂😂
 
Vipi mheshimiwa akabadilika tena na akawa na msimamo wa kuendelea ?
 
Ni wakati mwafaka Bunge letu tukufu likutane ili lipitishe uondoaji wa kikomo kugombea urais, ile miaka kumi sasa isiwepo. Kama mtu anafaa na hali inamruhusu aendelee milele hadi kifo kitakapomuondoa.

Lakini hapa pia litayarishe Tume huru japo kutakuwa na jamaa wenye mkono mkono, ila ikubalike na Wapinzani wote.
Hakuna guarantee kwamba akiongoza muda mrefu Mafanikio yatakuwepo mengi. Tume Huru si kwa Tanzania pekee, bali ni tatizo la hapa Afrika,
 
Ni wakati mwafaka Bunge letu tukufu likutane ili lipitishe uondoaji wa kikomo kugombea urais, ile miaka kumi sasa isiwepo. Kama mtu anafaa na hali inamruhusu aendelee milele hadi kifo kitakapomuondoa.

Lakini hapa pia litayarishe Tume huru japo kutakuwa na jamaa wenye mkono mkono, ila ikubalike na Wapinzani wote.
Over our dead bodies!!
 
Yote ulioandika hilo la tume huru ndo lenye uhai. Hayo mengine ya kuondoa ukomo wa urais, mimi kama mtanzania siungi mkono mpaka naingia kaburini
 
Ni wakati mwafaka Bunge letu tukufu likutane ili lipitishe uondoaji wa kikomo kugombea urais, ile miaka kumi sasa isiwepo. Kama mtu anafaa na hali inamruhusu aendelee milele hadi kifo kitakapomuondoa.

Lakini hapa pia litayarishe Tume huru japo kutakuwa na jamaa wenye mkono mkono, ila ikubalike na Wapinzani wote.
Wewe ni mjinga na huo ujinga ukifanyika nchi hii kamwe haitakuwa na amani tena. Aliyepo amalize miaka yake kumi ampishe mwingine kwa amani.

Watanzania hatutokubali kuongozwa na malofa miaka nenda rudi. [emoji51][emoji51][emoji51]
 
Umeona eei, hata haya ya chama au vyama naona ni mzigo kama inawezekana ukoo wa Magufuli tukausimika Ufalme wa Tanzania, zipo nchi za kifalme hazijui shida kitu gani, yaani mpaka raia wanafaidi bata wa Taifa.
Wee ndezi kweli [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Ndipo pale inaposemwa wenye wivu wajinyonge,mnatoka povu aafu povu lenyewe la kangara,sasa maneno yasio na heshima ya nini ? Nyie watu wa ajabu yaani aondoke yeye mbaki nyie mnaojua kutunga matusi mitandaoni.

Mi nakumbuka tuliomba sana tupate kiongozi mchapa kazi asieogopa na anaeweza kupambana asiemuonea haya mtu ,anampa mtu makavu mbele ya kadamnasi,umeona yule waziri aliekuwa hajui kuunganisha herufi , kilio kimesikika mbinguni na tumeletewa kiongozi anaeongoza watu na kuwasimamia ,nchi sasa inasimamiwa vizuri mno kuliko tulivyozoea.

Bunge la serikali kwa vile lipo na asilimia kubwa ni wachama cha Magufuli na hawatashindwa wacha kuondoa ukomo hata wakiamua sasa hivi nchi iwe na Mfalme ,linapita kwa asilimia miamoja.

Mbona Lesotho wana Mfalme na hatusikii haya makelele ya upinzani pinzani,hili nalo neno tulifikirie ,Sasa Mheshimiwa Magufuli ni Mfalme mtarajiwa,hivi la ajabu litakuwa lipi ? Lesotho haipo mbali ni mfano hai,haya ya kuwa na vyama vya wapinzani wengine wanapika pilau,wengine wanachemsha bata wengine wanapandisha tanga wengine wanavaa makoti kama madaktari wa wanyama pori. Ni balaa tu.

Na nchi yetu ilivyo tajiri chini ya Mfalme Magufuli tutaondoka hapa tulipo na kupiga hatua za mwendo kasi kuelekea maendeleo kamili kwa kila mwananchi,mpaka asie na kazi atalipwa.
Daaah, kweli mitazamo yetu haiwezi kuwa sawa, Kama Kuna mtu angebaki madarakani milele basi alikuwa hayati baba wa taifa hili, Mwl.J.K NYERERE!

Alikuwa na nyenzo zote za kulifanya hilo lakini hakuthubutu, akaasisi mfumo wa vyama vingi (HAKUWA MJINGA)

Wengine ambao wangeweza kubaki madarakani kwa msingi wa hoja zako ni mzee Benjamin Mkapa, alifanya kazi kubwa zaidi ya hata mzee Magufuli, kwani vision yake kubwa katika kuanzisha taasisi zinazoishi mpaka sasa haikuwa ya kitoto, imelisaidia sana taifa letu...(lakini aliondoka, hakuwa MJINGA)

Ili kuendelea kustawisha nchi yetu, acha tuendelee na utamaduni na desturi ya kuachiana madaraka kama ilivyo sasa, kwani bila huo utaratibu hata Magufuli asingepatikana, tuacheni kufikiria kuinajisi katiba.

Katika kuhitimisha hili, tukumbuke kwamba hakuna kiongozi aliyewahi kuwa mzuri kwa kila kitu, kila kiongozi ana mazuri na mabaya yake, tuwe na utamaduni wa kuendeleza mazuri na mabaya tumuachie aondoke nayo...

Nitatoa mfano mdogo tu, Rais Magufuli amekuwa mzuri kwenye kusimamia mambo na kusukuma maendeleo, lakini amekuwa mzuri pia kwenye kunyonga haki za wengine, mfano, kasome sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii ya 2019, kasome sheria ya utumishi wa umma 2004, halafu tazama anachokifanya, angazia biashara za mazao ya kilimo,n.k utanielewa namaanisha nini.

Tuheshimu mfumo tuliokubaliana,hakuna sababu ya kuubadili kwa sababu hizi mnazozitoa, ni sababu dhaifu mnooo!

Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
 
Ni wakati mwafaka Bunge letu tukufu likutane ili lipitishe uondoaji wa kikomo kugombea urais, ile miaka kumi sasa isiwepo. Kama mtu anafaa na hali inamruhusu aendelee milele hadi kifo kitakapomuondoa.

Lakini hapa pia litayarishe Tume huru japo kutakuwa na jamaa wenye mkono mkono, ila ikubalike na Wapinzani wote.
Usitunyime raha ya kuona bimbwanga na mbwembwe za viongozi:

Mchonga: haambiliki, lakini tulipata huduma bure na tuliheshimiana.

Mzee ruksa: wakatokea miungu watu, tanzania ikawa jalala kwelikweli. Tukanywa bia za Stella Artois zilizoisha muda wake, tukanunua magari mpaka ya laki saba(Jaba), mishahara ikawa taaabu, tukahimizwa kujishughulisha kwakuwa mishahara haitoshi, tz ikawa home of drug trafficking, name them.

Mzee wa ukweli na uwazi: nchi ikawa na akiba, heshma ya mtumishi ea umma ikarudi.

Vasco da Gama; sitii neno, maana tulioneshwa kuwa tupo tisiostahiki kupata hata vumbi la keki.

Wacha tuinjoyi hii substitution😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀
 
Back
Top Bottom