Bunge, Serikali na Mahakama, Sio Mungu, Sio Malaika, Zinaweza Kukosea!. Zinapokosea, Zina Wajibu Kurekebisha na Kutenda Haki, Vinginevyo Karma Will Do

Naunga mkono hoja,uitishwe mdahalo wa wazi wa pande zote mbili wa watu wenye akili nzuri,hoja ijibiwe kwa hoja hapo hapo.Mkuu Paschal ukifanikisha hilo nchi itakukumbuka.
 
Itisha Mdaharo wa wazi wa siku tatu pale Nkrumah UDSM, Waite wasomi wote magwiji wa sheria na sio wanasiasa, uwe mjadala wa wazi wasomi washeria na wasomi wengine watoe maoni yao.

Mjadala uende live na kusiwe na filter yeyote, kila mtu atoe maoni yake kwa uwazi kabisa. Taifa linapata picha.
 
Leo ndio umeandika hoja za maana nadhani ulikua unawatetea lakini umeona unaowatetea ni watu wenye dharau sana na wasio wasikivu,

Hata usishangae ndugu yangu…wapo watu ambao kwa unafiki wao ni wa kupuuzwa tu! Baada ya kuwagundua hawanihangaishi tena.
 
Mengine yote ni porojo tupu
 
Atazuiwa kuingia nane nane
 
Hakuna hoja zozote zitakazojibiwa, kubalini tu mmepigwa 'big time'.....Ccm imeonyesha dharau zake waziwazi kwa wenye nchi.

JokaKuu Nguruvi3 Kalamu
zitto junior
Mkuu 'Proved', kama nilivyowahi kueleza huko awali nilipoitwa kwenye mada za maandishi ya huyu mleta mada, binafsi huwa sina kinachonivuta nisome maandishi yake, kwa hiyo huwa sizisomi.

Chukulia kwa mfano kichwa cha habari ya mada hii hii uliyoniita nichangie.
Anasema "Bunge, Serikali, Mahakama sio mungu, sio malaika zinaweza kukosea...".

lakini mtu huyo huyo anajua wazi kwamba huku siyo "KUKOSEA"

Sasa kwa mtu wa namna hiyo utajibu nini kuhusu mawazo yake hayo?

Serikali na wote hao wengine, hakuna aliyekosea; ni mpango maalum waliopanga, kwa maksudi kabisa kuufanya wakijua ubovu wake, ndiyo maana wanang'ang'ania hata wanapoelezwa upungufu katika mpango wao huo.

Ingekuwa nchi hii wananchi wake wameshika madaraka na hatma ya nchi yao, hawa wote wakati huu wangekuwa magerezani kujibu tuhuma za uhujumu wa nchi kwa maksudi kabisa.
Huyo anayejiita mwandishi badala yake anataka wananchi wakawapigie magoti kwaomba wawaonee huruma.

Hovyo Kabisa.
 
Kidogo kidogo naanza kuelewa kwanini hayati aliishia kulifasiri jina lake kuwa ni 'njaa'
 
Angalau umewasemea wananchi nimefurahi. Yoyote anaekiuka HAKI na kuwadharau wananchi alaaniwe. Asante kwa kujaribu kuwasemea wananchi waliokosa utetezi
 
Hata akichagua kugombea,

HATOGOMBEA!!!
 
Narudia tena mdogo mdogo tu utarud kweny akili yako halis ya kukemea pale penye ukakasi. Ni suala la muda tu!!!
 

Nina maswali machache Kwenye hii sababu yako ya kiUhalisia, ambayo nadhani majibu yake unayo.

Maswali:
- Nini kinahitajika/ kifanyike ilituweze "kuimarisha" bandari "kiuwezo wa uendeshaji"?
-Nini kinahitajika ili "kuimarisha" bandari "kimtaji"?
- Kumeshawahi kufanyika utafiti wowote rasmi kujua ni nini kinahitajika "kuimarisha" bandari kwa namna uliyohitaja?
 
nyumbani kwako kwa mkeo, ukishindwa, ni lazima tuu utasaidiwa!. Hili nimelisema.

Inapotokea hali hiyo, baba mwenye nyumba amekosea, sio lazima akiri, makosa na kuomba msamaha, lakini anapobaini amekosea, ana wajibu wa kurekebisha makosa kwa kufanya the right thing and do it right!.
Baba au Mama?
 
Binadamu tunatatizo linaitwa mob psychology ukiaminishwa jambo unalibeba kwa nguvu zote kwa bahati nzuri Mungu alifanya hivyo kwa maksudi yake mfano wale walioamua kujenga Mnara wa Baberi kama Mungu asinge ingilia kati kuna kitu kibaya kingetokea.

Mfano Leo watu wote tungekuwa na Imani ya Dini moja lazima ingekuwa shida lakini Leo ukitaka watu waingie kwenye imani ya Dini au dhehebu ni lazima ufanyike ushawishi ambao wengine wataamini na wapo ambao hawataamini kamwe.

Kwenye Siasa nako kila mtu anao Uhuru wa kuchagua chama chake na kujiaminisha kwamba vyama vyote vilivyopo havifai ili chama chake.

Kimataifa ndiyo maana kukapitishwa Kukubali kuto kukubaliana ili Dunia isonge mbele.

Leo vijana wetu wanakamatwa wakiwa safarini kwenda kupata mafunzo ya kigaidi hii ni kutokana na wasiokubali kutokukubaliana kuwa radicalise vijana kwa nia ya kuja kupambana na wale wasiofuata misimamo yao.

Hakuna Siku hata moja watu wote wakakubaliana jambo la kitaifa kwa kauli moja mifano ni mingi sana kumbuka kuhama kutoka analogue kwenda digital,usajili wa simu, uwanja Mpira kwa Mkapa,ununuzi wa ndege,Muungano nk.

Ninavyoona ni kwamba Serikali inajukumu la kuhakikisha kila jambo zuri lenye manufaa kwa wananchi linapotakiwa kutekelezwa lazima ifanye utafiti wa kina na baada ya hapo itekeleze mradi bila kuruhusu mijadala isipokuwa mijadala iwe kabla ya utafiti na pale ambapo jambo halieleweki.
 

Kiwepo chombo cha kufanya hiyo mipango na tafiti za kitaifa. Serikali (ya chama tawala) iwe ni mtekelezaji tu. Chombo hichi kiwe na wabobezi katika kila nyanja/taaluma.

Tukiendelea kama ilivyo sasa, ndio utakuta chama tawala kimeshindwa kutekeleza wajibu wake, alafu kinasema nchi imeshindwa.
 
https://www.facebook.com/
View: https://fb.watch/mTLTQUYlL6/?mibextid=NnVzG8&startTimeMs=204921
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…