Bungeni Dodoma: Rais Magufuli avunja Bunge la 11. Asema ajira 6,032,299 zimetengenezwa, Viwanda vipya 8,477 vimeanzishwa

Ajira 6 m in 5yrs ni ajira 1.2m per year ambayo ni ajira 100,000 per month ambazo ni ajira 3,333 per day.
Hizi ajira 3,000 kila siku zinatangazwa wapi jamani maana leo tu utumishi ajira mpya hazifiki ata 100
 
Sawa, usalama wa raia umeongezeka kwa kiwango ambacho kimetajwa, Je kuhusu hizi issue zinazosikika za utekaji na utekwaji hazionekani kama dosari zinazochafua usalama wa raia?

Au usalama tunaouzungumzia tu, ni ule wa mipakani? Tukumbuke neno usalama halitumiki kimwili tu bali hata kiroho.

Endapo kama raia watadhulumiwa haki zao, kesi hazisikilizwi kwa wakati, kesi za kubambikiwa raia, kudhihakiwa na kudharauliwa, hivi vyote vinahatarisha usalama wa mtu. Kuna haja ya kuelewa usalama wa mtu/watu kwa mapana zaidi ili tuzungumzie hili jambo.


Sent from my TECNO B1 using JamiiForums mobile app
 
Viwanda 8,000 labda pamoja na vyerehani.
 
Hivi bado huwa mnawaamini wanasiasa,jamaa anakwambia maelfu ya viwanda vimeanzishwa katika awamu yake....mi nasubiri tu iyo siku watakayotoa iyo list ya viwanda wanavyodai vimeanzishwa
Wewe kila siku upo hapo buza kwa lulenge, utayajuaje ya vijijini?
 
Ajira mil6 haya ni matusi.
Au zipo chato? Inabidi wat twende chato
 

Neno Usalama ni pana sana halafu pia ni Mtambuka mno katika Maisha yetu na Nchi yetu ila Kikubwa kama Wewe huna tatizo basi jua uko Salama.
 
Kutoka vijiji 2000 mwaka 2015 vyenye umeme hadi vijiji 9000 hii ni speed kubwa, huyu jamaa ukiachilia mambo mengine ila utendaji kazi wake ni mzuri, hotuba yake kagusa kila mahali.
Una uhakika na ulichoandika?
 
Eti viwanda 8,477 na ajira 6,032, 299 huyu dikteta amekubuhu kwa uongo! Duh!
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…