Bungeni Dodoma: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akosa Mbunge wa kumuuliza swali la papo hapo

Bungeni Dodoma: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akosa Mbunge wa kumuuliza swali la papo hapo

Sasa unajiandikishaje kuuliza swali kwa Mtu ambaye hayupo? Hii nchi ngumu sana wallah, yaani PM yupo zake kwenye kampeni huko kwa Mpango na ameacha majukumi yake ya Kiserikali pale Bungeni!

CCM, sasa hivi watanzania tutaanza kumuomba MUNGU na tutamuachia yeye afanye kwa niaba yetu hasa wabunge wanaokula Posho za makalio.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Nadhani ndio maana PM akaamua kwenda zake kwenye kampeni maana aliona hakuna cha Maana.. Sema CCM wanauchu wa madaraka sana, yaani kuna sababu gani PM kwenda kupiga kampeni kwenye Jimbo moja ilihali wana majimbo zaidi ya 360 yanakero za kutosha?😆😆
 
Nikikumbuka Bunge lililopita, nilikuwa naisubiria kwa hamu sana siku ya Alhamisi kumuona kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe wakati huo, kupata wasaa wa kumuuliza Waziri Mkuu juu ya sensitive essues
Wabunge wa CCM ni wabobezi katika kuomba miongozo, huwa walikuwa wanasubiri nondo za wapinzani ndipo nao wapate mwanya wa kuomba miongozo
 
Ina maana hata wale Covid-19 na wao wamewekewa operating system ya maccm
 
Kusema ni rahisi sana kuliko kutenda,hata wale waliounga mkono juhudi wamekosa la kuuliza kwakweli inashangaza sana.
Kwakuwa wote ni wakupitisha ilani ya Chama tusitegemee kuona maswalai ya kuikataa au kukinzana na ilani ya Chama, aibu, mshangao,kutokujua mwelekeo vyote ni toka ndani ya Chama tawala.
 
Kuwa makini sana na groupthink katika mikutano ambayo haina maswali.
 
Leo hii ikiwa ni Alhamisi kama tulivyozoea kuwa ni siku ya wabunge kumuuliza kiongozi wa shughuli za bunge mh Waziri Mkuu.

Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson amesema, leo Alhamisi kulikuwa na kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, lakini "hakuna mbunge aliyejiandikisha kwa ajili ya kumuuliza Waziri Mkuu."

Ktk hali ya kuangaza hakuna mbunge aliyekuwa tayari kujiandikisha ili amuulize mwaswali ya papo kwa papo mh waziri mkuu.

Bunge kukosa wabunge wa upinzani kunalifanya kulala usingizi wa pono.

Haya ndiyo madhara ambayo waliyo panga huu mpango wa kuwakwamisha wapinzani wasishinde basi yatawatafuna maishani mwao milele.

bunge dhaifu huzaa wabunge goigoi
 
Back
Top Bottom