Bungeni: Mbunge wa CHADEMA amtimua mpangaji wake ambaye ni Askari Polisi, adai haoni maana ya kushirikiana nae, Waziri Lugola amtisha

Haitoshi kuwafukuza mapolisi hayo matendaji lazima yatimuliwe yakalale CCM.
Halafu huyo mkata viuno si awapangishe nyumbani kwake?
 
Hii midada ya viti maalumu chadema sio wa kulaumu sana maana sera kichwani hamna na jinsi ya upatikanaji wao huwa ni aibu kuelezea humu.
 
Kampangishe wewe huyo Askari.
 
😁😁😁😁😁🙂😁 huyo MBUNGE noma maana sio kwa ukauzu huo.
 
Najaribu kutafakari ni sheria ipi itamtia hatiani huyo mbunge
 
Mama nakuonea huruma sana. Je umejiandaa vyema kupambana na Hilo kundi? Wanaweza kukutengenezea fitina makusudi sijui utakuja Tena hadharani kuwalalamikia hawafanyi kazi.
 
Ovyo kweli kweli kiongozi ni kioo cha jamii hivi sasa mtu kama huyu anafundisha nini wananchi.

Hii ni ‘hate crime’ na hatua za kisheria lazima zichukue mkondo wake.
 
Hata mimi ningemuondoa ila nisingemtangaza bungeni

Ishu sio kumuondoa polisi, ishu ni kuutarifu umma juu ya mpasuko uliopo hapa nchini. Upendo, udugu na amani ya moyoni haipo tena. Hili ndilo jambo alilotaka kuelezea umma. Ujumbe umefika
 
Najaribu kutafakari ni sheria ipi itamtia hatiani huyo mbunge
TRA kama alikuwa kodi halipi na TRA ikishamtia hatiani haruhisiwi.kugombea Tena milele udiwani ,ubunge ,uraisi au uongozi wa serikali ya mtaa sababu kukwepq Kodi ni moja us kosa ambalo ukidakwa haruhusiwi kugombea

Pia Kuna huo.mkataba wa kupanga nyumba Kama kakiuka imekula kwake
Tatu kosa la kimaadili.la kibunge ,bunge lenyewe Lina uwezo wa kula naye sahani moja
 
Ovyo kweli kweli kiongozi ni kioo cha jamii hivi sasa mtu kama huyu anafundisha nini wananchi.

Hii ni ‘hate crime’ na hatua za kisheria lazima zichukue mkondo wake.
Hiyo ni hate speech .Nchi za wenzetu saa hii angekuwa na pingu
 
Mama nakuonea huruma sana. Je umejiandaa vyema kupambana na Hilo kundi? Wanaweza kukutengenezea fitina makusudi sijui utakuja Tena hadharani kuwalalamikia hawafanyi kazi.
Tena aelezwe wazi traffic polisi wanasubiria magari yake barabarani hakuna atakayekuwa tayari kumpa ushirikiano Kama yeye asivyotaka ushirikiano
 
Ndo kusema ile kinga ya wabunge wakiwa mjengoni nayo ndo haina maana tena?
Aliyemsema na kumtimua hayuko bungeni kamnyanyasa mtu nje ya bunge hakuna Cha Kinga hapo.Huwezi niibia ukakimbilia bungeni ukasema uliniibia halafu ujifanye una Kinga ya bunge.Kitendo kiovu ulichofanya nje ya bunge lazima uwajibike
 
Uovu ni upi?
Kumkataa mpangaji au kutangaza bungeni nimemkataa mpangaji?
 
hata mimi ningemtimuwa au hata kumwitia mwizi apewe kichapo maana ndio wanao wapa kiburi hao mashetani wa kijani.
 
Huyo hawajui polisi wa nchi hii ni heri angekaa tu kimya kwa kuwa tayari ameshamtimua na nafsi yake imesuuzika badala ya kuendekeza huo upayukaji.

Atalengeshwa kwa wahuni wampore halafu wasikilizie ataenda ku-report wapi!

Akijipeleka huko atakutana na yaliyomkuta Magdalena Sakaya miaka ile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…