TANZIA Buriani Abbas Kleist Sykes


Kudos [emoji1548]
 
Kuandika ni sanaa na siku zote sanaa haina kanuni

Hii ni kwa sababu sanaa ni ubunifu wa kuunda/kutengeneza/kutunga/kuanzisha mtindo/mpango/utaratibu/muonekano/mpangilio/mnasibu wa kitu/jambo/umbo/mtindo/mchezo/habari au taarifa

Usikariri usomi wa elimu za kizamani za KIHAFIDHINA ulimwengu wa leo upo very flexible kuakisi maendeleo ya kila kitu kutokana na ubunifu wa mambo mablimbali katika nyanja tofauti tofauti ili kuleta furaha katika maisha ya kila siku na kuupamba ulimwengu uvutie kuishi na maisha yawe mazuri

Usichanganye mambo hakuna SHERIA au KANUNI ya KUFANYA sanaa ila kuna SHERIA na KANUNI za kuendesha UFANYAJI wa sanaa kwa hiyo sanaa kama sanaa inaweza kufanywa vyovyote ili mradi ipendeze na kuvutia kutegemeana na lengo la Msanii

Ungetuandikia wewe basi uliesoma haswaa na ukaelimika kikwelikweli acha dharau wakati hujui lolote Mxieusssszzzz!!! HOVYOOO !!!

Kongole Mohamed Saidi

Umesanifu vizuri taarifa yako na imevutia sana kiasi cha kumfanya mtu arudishe fikra na kujaribu kutengeneza picha na mandhari kichwani mwake kana kwamba anashuhudia hali ilivyokua katika miaka hiyo ya hamsini

Hujagusa tu watu husika lakini pia umesanifu maelezo yako yamegusa mpaka Jiografia ya maendeleo ya mitaa na mipango miji ilivyokua na ilivyo sasa kiasi mtu anajenga picha kichwani mwake ya hali ilivyokuwa katika miaka hiyo ya kuanza kwa TANU

Hongera Mkuu hizi ni hazina kwa sisi vizazi vilivyofuata baadae
 
Inna lillah wainna ilaih rajiuun bw.Abbas Sykes
 
Ubaguzi unatoka kwa nani kwenda kwa nani.
Maana serikali ya sasa ni ya Mzee wetu ......, sasa ni juu yetu sisi wajukuu zake kuandika kwenye hayo magazeti
 
Si uandike wewe ujuavyo? Unataka kila aandikae aandike utakavyo wewe? Unanshangaza!
 

Ustadhi wa gas haitoki nakuona unakuja kwa kasi kama moto wa mabua.Tulia soma taratibu utaelewa bahati mbaya leo nimeanza kufunga sita.
 
Sio wakimbilia Ubelgiji,hawa hakukimbia kuchumia tumbo,walimkabili mkoloni hapahapa
Mkoloni mweupe hakuwa anawapiga Risasi kwenye Viwanja vya Bunge Mkoloni mweusi ndio Hatari zaidi lakini atang'oka tu
 
Huyu ndo babake Abdul Sykes aka Dully Sykes?
Nilikuwa Dubai, nilipigiwa simu na BBC kutaka kunihoji hapohapo nilikuwa Tanga nikifuatilia katika TV......


Visa vya kutunga tunga vina shida zake
Kishindo,
Hapana ndugu yangu sina sababu ya kusema uongo.

Bahati mbaya wewe unadhani hayo ni makubwa si yangu naamua kutunga.

Mie si mgeni wa yote hayo nikae kitako kuyatamani na kuyatunga katika fikra.

Angalia picha niko BBC Glasgow mwaka wa 1991.

Jitulize nisome upya.

BBC walikuwa wanataka kunihoji ugonjwa wa Mwalimu yuko London.

Tanga sasa Mwalimu kesha fariki mimi nafuatilia matangazo ya mapokezi ya mwili wake katika radio siko tena Dubai.

Ukipenda kunifahamu ingia hapa: mohamedsaidsalum.blogspot.com

 
Aah, wapi! Huyo Mohamed Said huwa anajua historia ya watu wasiozidi kumi; Abbas na Abdul Sykes, Dosa Aziz, Bibi Titi, Rupia na wengine wachache. Na hao wote ni wa Kariakoo mitaa ya Aggrey na Tandamti! Hajui kingine chochote zaidi ya hiyo mitaa!!!
 
Kwameh,
Kughitilafiana ni silka yetu binadamu.

Ningekuwa naandika kama unavyoona wewe kuwa ndiyo sawa nisingekuwa hivi nilivyo leo.

Ila hili la uungwana sijui kwa nini umelileta.

Nakushukuru.
 
Aah, wapi! Huyo Mohamed Said huwa anajua historian ya watu wasizidi kumi; Abbas na Abdul Sykes, Dosa Aziz, Bibi Titi, Rupia na wengine wachache. Na hao wote ni wa Kariakoo mitaa ya Aggrey na Tandamti! Hajui kingine chochote zaidi ya hiyo mitaa!!!
Sweet tablet,
Niko Washington DC VoA wananihoji mie mbumbumbu wa Tandamti.

Nijue nini Mswahili mimi.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…