Buriani Mzee Ruksa: Ni Deng Xiaoping Wetu wa Mageuzi ya Kiuchumi, Demokrasia, Haki za Binadamu na Uhuru wa Habari. Asante kwa Ruksa Zako, Pumzika!

Buriani Mzee Ruksa: Ni Deng Xiaoping Wetu wa Mageuzi ya Kiuchumi, Demokrasia, Haki za Binadamu na Uhuru wa Habari. Asante kwa Ruksa Zako, Pumzika!

Nairobi palionekana kama Ulaya, mtu akitoka Nairobi anarudi na sabuni, dawa za kupigia mswaki na bidhaa nyingine za basic needs.

Mwinyi aliondoa habari hizo.
Aisee!

Kula ilikuwa changamto, sukari changamoto. Nguo za viraka. Haikutosha, hata sabuni na dawa ya kupigia mswaki?

Kama kitu kama sabuni na dawa ya kupigia mswaki vilionekana anasa nakosa cha kusema kiukweli! Mlipitia kipindi kigumu sana.
 
Kiranga

Mama yangu aliniambia baba yako alifuatwa na usalama wa taifa nyumbani na wakaondoka naye kisa anaonekana tu ana maendeleo fulani.

Na hicho kipindi mzee alitaka kununua gari, mama anasema na laiti angelikuwa ameshalinunua halafu usalama ndiyo wamemdaka hali ingekuwa mbaya kwa baba yenu.

Kwa sababu kuna ndugu yetu mmoja alifilisiwa na alikamatwa kabisa na aliwekwa ndani. Walichimbia hela nyengine chini ya ardhi ili wasionekane wana visenti angalau.
 
Mwalimu ana pande mbili za sarafu nzuri na mbaya.

Ubaya ni kwamba propaganda imepigwa zaidi katika upande mzuri ila mbaya umefichwa hivyo ni rahisi zaidi makosa ya Mwalimu kurejewa na walio mfuatia kwa sababu Watanzania wengi hawafahamu upande mbaya wa Mwalimu.

Ogopa sana mtu ambaye itikadi imemtawala kupindukia ni ngumu kuamini jambo fulani ana kosea au hayupo sahihi, siku zote yeye ata amini ana fanyiwa hujuma au hajaeleweka wakati sivyo.

Wakomunisti na wajamaa wengi wa mwanzo ukomunisti na ujamaa uliwalevya kupindukia na hili pia naliona kwa mataifa ya kibepari hawa watu huwa hawaoni wala hawasikii na wala huwa hawaamini kwamba nje ya mawazo na mfumo wao kuna mambo mengi bora unaweza kujifunza na kuyachukua.

Mwalimu ujamaa ulimlevya na kumpofusha mazima akawa haoni wala hasikii wala aamini kuwa kuna mazuri na mabaya ndani ya ujamaa na pia kuna mazuri na mabaya nje ya ujamaa.
 
Aisee!

Kula ilikuwa changamto, sukari changamoto. Nguo za viraka. Haikutosha, hata sabuni na dawa ya kupigia mswaki?

Kama kitu kama sabuni na dawa ya kupigia mswaki vilionekana anasa nakosa cha kusema kiukweli! Mlipitia kipindi kigumu sana.

Watu walikuwa wanatengeneza sabuni zao zinaitwa maganji, wanachanganya magadi, majivu, mafuta na vitu gani sijui, wanapata sabuni za kutengeneza wenyewe.

Wengine walikuwa wanafua kwa kutumia majani ya mpapai.

Chakula kilikuwa haba tulikula bulga, bulga ni kama uji fulani wa ngano kama nakumbuka vizuri. Kulikuwa hakuna mchele wala unga.

Ronald Reagan akatufanyia mpango tukapewa unga wa msaada kutoka Marekani, unga wenyewe wa njano, watu wakawa wanasema huu unga wa njano ni mahindi ya kula wanyama, ni unga wa mahindi ya kula farasi na ng'ombe, si ya kula watu.

Lakini kwa sababu tulikuwa na njaa, tukala tu ule ugali wa njano. Tuliuita ugali wa Yanga kwa sababu ya rangi ya njano.

Nimekumbuka miaka ile mpaka machozi yamenitoka.

Mwinyi aliondoa dhiki ile.
 
Kama tunataka kujenga taifa bora tuna hitaji kuwa katikati ya ujamaa na ubepari kamwe tusiwe wajamaa wala wabepari.

Kuna madhara makubwa sana sisi kulevya na itikadi za kibepari au kijamaa.

Tunahitaji kujua yapi ni bora katika ubepari na yapi ni mabaya pia tunapaswa kujua yapi ni bora katika ujamaa na yapi ni mabaya.

Case study yetu ya mwanzo inapaswa kuwa China na Singapore.
 
Bila shaka mwinyi alipata shida Sana kuongoza huku nyerere akiwa pembeni akifanya interference ya Mara kwa Mara.

Namkumbuka hata sera za benjamini mkapa nyerere alikuwa anazikosoa waziwazi
 
Huna akili kwa hiyo ww kwako ufahari wako ni kuwa na noti ya sh 100 na 50 na sio ubora wa maisha ya watu?
Yaani Nyerere aliye wafanya watu wavae uchi ,wakose mpaka mahitaji muhimu kama sabuni,haka kumiliki redio ilikuwa ni anasa ndo bora ,kuliko mwinyi aliye kuja kufuta huo upuuzi?

Sasa kati ya ww unaye amini ya kuwa nchi ikiwa na noti yenye 0 chache ndo maendeleo na Mwinyi ni nani kilaza?

Pesa ya Kuwait na Oman ina thamani zaidi ya mara 3 ya $ya kimarekani ,sasa hivi ukiwekewa $ na pesa ya hizo nchi utachagua kipi?

Pesa ya Kenya ina thamani kuliko pesa ya Korea na Japan ,haya tuambie maendeleo ya Kenya na hizo nchi yakoje?
Pesa ya Tz ina thamani zaidi ya mara 4 ya pesa ya Iran vipi kuhusu maendeleo kati ya nchi hizo mbili?

Zambia hapo si wana noti ya 100 wana nn cha maana zaidi ya njaa?
Ww jamaa uminitoa tongo za macho
 
Watu walikuwa wanatengeneza sabuni zao zinaitwa maganji, wanachanganya magadi, majivu, mafuta na vitu gani sijui, wanapata sabuni za kutengeneza wenyewe.

Wengine walikuwa wanafua kwa kutumia majani ya mpapai.

Chakula kilikuwa haba tulikula bulga, bulga ni kama uji fulani wa ngano kama nakumbuka vizuri. Kulikuwa hakuna mchele wala unga.

Ronald Reagan akatufanyia mpango tukapewa unga wa msaada kutoka Marekani, unga wenyewe wa njano, watu wakawa wanasema huu unga wa njano ni mahindi ya kula wanyama, ni unga wa mahindi ya kula farasi na ng'ombe, si ya kula watu.

Lakini kwa sababu tulikuwa na njaa, tukala tu ule ugali wa njano. Tuliuita ugali wa Yanga kwa sababu ya rangi ya njano.

Nimekumbuka miaka ile mpaka machozi yamenitoka.

Mwinyi aliondoa dhiki ile.
Kwa kweli niwape pole sana ya dhati kabisa kutokea moyoni.

Kuna kitabu chochote naweza kuyapata haya Bw. Kiranga? Au hata pdf?

Kwa sababu kwa kizazi chetu yakizungumzwa haya yanaoenakana kama hadithi.

Kuna kipindi nilikuwa naongea na wenzangu walishangaa na wengine kubisha kwamba Tanzania kwa zaidi ya mara mbili imenusurika kupinduliwa kijeshi. Ajabu watu hawajui kama kuna kitu kama hiki! Na siliongelei kisiasa yani niliongela kihistoria.
 
Kama tunataka kujenga taifa bora tuna hitaji kuwa katikati ya ujamaa na ubepari kamwe tusiwe wajamaa wala wabepari.

Kuna madhara makubwa sana sisi kulevya na itikadi za kibepari au kijamaa.

Tunahitaji kujua yapi ni bora katika ubepari na yapi ni mabaya pia tunapaswa kujua yapi ni bora katika ujamaa na yapi ni mabaya.

Case study yetu ya mwanzo inapaswa kuwa China na Singapore.
Ewaaa! Naungana na wewe kwenye hili! Lakini napata tabu kwa nchi yetu kwa maana safu ya uongozi bado sijamuona aliye na maono ya namna hii!
 
Siku ya leo, tunampunzisha Mzee wetu, Rais Mtaafu wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi, kwa jina maarufu la Mzee Rukhsa, kwenye nyumba yake ya malalo ya makao ya milele.

Mara ya Kwanza Kulisikia Jina la Ali Hassan Mwinyi.
Kwa mara ya kwanza jina la Ali Hassan Mwinyi, nililisikia mwaka 1977 nikiwa darasa la 3 shule ya msingi, wakati huo akiwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani wa serikali ya Nyerere, alipolazimika kujiuzulu kutokana na kashfa ya vifo vya watuhumiwa wawili wa mauaji ya vikongwe, huko Mwanza mwaka 1976.

Mwinyi hakuwa peke yake aliyejiuzulu kutokana na kashfa hiyo, bali Makamo wa pili wa rais na Waziri Mkuu, Rashidi Mfaume Kawawa, pia aliondolewa!, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, anyeshughulikia Usalama wa Taifa, Peter Siyovelwa aliondolewa!. Wakafuatiwa na watendaji wakuu wa vyombo vya usalama Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Emelio Mzena, akastaafishwa kwa manufaa ya umma!, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Samweli Pundugu akastaafishwa kwa manufaa ya umma, na Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza pia akapumzishwa.

Mwalimu Nyerere alikuwa sio mtu wa mchezo hata kidogo!, kwani baada ya kuwafagia kule juu, fagio la chuma, likatua mjini Mwanza, likaanzia kumfagia Mkuu wa Mkoa Peter Kisumo, akaenda na maji, RPC wa Mwanza, RSO, OCD, na DSO wa Mwanza, kwanza wote wakafutwa kazi, kisha wakarejeshwa vijijini kwao, kwa kusombwa na Land rover 109 usiku usiku na kurudishwa kwenye their places of domicile na mwisho wa siku walikuwa kushitakiwa kwenye ile kesi maarufu, "Kesi ya Mauaji Mwanza" ya mwaka 1976. Mtu pekee aliyesalimika kati ya hao washtakiwa ni mtu mmoja tuu, aliyeitwa Andrew Mayalla, na salama yake, mdogo wake anayetwa Mathew Kasanga, kumuwekea wakili mahiri wa wakati huo, Wakili Murtaza Lakha, kumtetea kaka yake, lakini wengine wote, walikwenda na maji na walikula mvua za kutosha!. Ni kupitia tukio hilo ndipo nilipoanza kulisikia jina la Ali Hassan Mwinyi. Hiki kisa cha Kesi ya Mauaji Mwanza pia nilikihadithia kwenye bandiko hili TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!
Sijui uwajibikaji wa aina hii ya enzi za Nyerere, ulikuja kupotelea wapi, siku hizi watuhumiwa wanakufa mikononi mwa polisi, and no body cares!.

Tukio hilo lilileta mageuzi makubwa nchini mwetu, kwanza Idara ya Usalama wa Taifa, ilifumuliwa na kusukwa upya kwa kufanyiwa mabadiliko makubwa, ikaletwa sheria ya usalama wa Taifa, ya 1976, Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 na katiba mpya ya mwaka 1977.

Jina la Ali Hassan Mwinyi, nikaja kukutana nalo tena shule ya msingi, jijini Dar es Salaam, tukisoma na mtoto wake Hussen Mwinyi (Dr)aliyenitangulia madarasa mawili. Baada ya shule ya Msingi nikajiunga shule ya sekondari ya Tambaza, ile mwaka 1985 Rais Mwinyi anakuwa Rais wa Tanzania, yule mtoto wake Hussein Mwinyi alikuwa anasoma PCB Tambaza! alikuwa darasa moja na mtoto wa Malecela, Seche. Kitendo cha mtoto wa rais na mtoto wa Makamo wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu John Malecela kusoma shule moja, na halikuwa jambo dogo!, sasa ndio nikazidi kumfahamu Ali Hassan Mwinyi kwa karibu, wakati huo hapo Tambaza pia tuko na mtoto wa Nyerere na Mtoto wa Mkapa, darasa moja.

Mwanzo wa Mwinyi Kutwa Mzee Ruksa.

Wakati Mwinyi anachukua urais ile 1985, hali yetu ya Uchumi ili dhollfu bin taaban, baada ya vitavya Kager ana Mwalimu Nyerere kutangaza miezi 18 ya kufunga mikanda, mambo kiukweli yalikuwa magumu, tumekula unga wa Yanga, kutoka Marekani ambao kule kwao ni chakula cha mifugo!, Watu wamevaa magunia, sandarusi hadi sisi wanafunzi nchi nzima tumevaa uniforma ya kitambaa cha madurufu, ambacho nip amba chafu ya kutupa!.

Mahitaji muhimu yote ni kwa resheni kupitia maduka ya kaya, tulikuwa tunapanga foleni siku nzima kusubiria kuuziwa kilo mbili mbili za sukari, hivyo Watoto wote mnatumwa, ili kuwahi foleni, watu walidamka asubuhi na kupanga mawe, gari linaweza kuja saa 10 jioni au siku nyingine kutoka bila bila, haliji kabisa.

Nchi za mabeberu zilimpa Mwalimu Nyerere masherti magumu ya kutupa misaada, ndipo Mwalimu akaamua kuliko kukubali misaada ya masherti na kugeuka nyuma akageuka jiwe, bora aachie ngazi, kwa mtindo wa kung’atuka na kumpisha Ali Hassan Mwinyi. Hivyo Mwinyi aliipokea nchi ikiwa kwenye dhiki kubwa!.

Baada ya ya kuingia rais Muislamu, kukaibuka vikundi vya Waislamu wenye siasa kali, kwanza waligomea Nguruwe wasichinjiwe mahali pamoja, na wanyama wengine kwasababu nguruwe ni haramu kwa Waislamu,
na isiuzwe bucha zile zile za nyama ya kawaida.

Vikundi hivyo vikaleta vurugu za kulazimisha nyama ya nguruwe ipigwe marufuku kwasababu ni haramu, na kuanzishwa mihadhara ya kashfa, kwa wanazuoni wa Kiislamu kuikosoa Biblia na kusema nguruwe hata kwenye Biblia ni Haramu. Vurugu hizo zikapelekea kuvamia mabucha ya nguruwe na kuvunja kisha kukimbilia kujificha misikitini kulikopelekea vurugu za Msikiti wa Mwembecha miaka kadhaa baadae.

Rais Mwinyi akatangaza rukhsa mtu yoyote kula kitu chochote, hakuna ruhusa ya mtu mwingine yeyote kuingilia uhuru wa mtu wa dini nyingine yoyote kula chochote, “Ruksa” na huo ukawa ndio mwanzo wa kuitwa Mzee wa Ruksa, wale wahuni kwa kisingizio cha dini walishughulikiwa kikamilifu, ikiwemo Msikiti wa Mwembechai Kuvamiwa, tena ikatokea mmoja wa wana vuguvugu hawa ni mshikaji wangu sana wa deski moja sekondari ya Tambaza, akiitwa Hassan.

Baada ya kuzifungulia hizo ruksa, alikuja kufungulia ruksa nyingine nyingi za biashara, Uchumi, akaruhusu mitumba, akaruhusu Chai Maharage, akalipindua Azimio la Arusha lililoweka miiko ya uongozi na kuleta Azimio la Zanzibar ambalo liliruhusu viongozi kufanya biashara na kumiliki mali na hapa sasa ndio viongozi wa umma wakaanza kuwa matajiri na kuupindua uchumi wetu kutoka uchumi wa kijamaa na kuingia kwenye uchumi wa kibepari wa nguvu ya soko, market economy.

Ruksa nyingine kubwa Rais Mwinyi aliyotuachia ni ruksa ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini Tanzania kiasi kwamba sifa ya Baba wa demokrasia Tanzania inamstahili kabisa!, Mwinyi ndie Deng Xioping wetu!.

Japo Rais Mstaafu, Ali Haasan Mwinyi, Mzee wa Rukhsa, ametutoka kwa kutangulia mbele ya haki, huku nyuma Watanzania tunaendelea kuzifaidi rukhsa zake, tutanzienzi milele, na tena sio tuu ametuachia Rukhsa, pia ametuachia na kale ka copy pale Zanzibar!, cha mtu rahimu kama yeye!.

Akina sisi, tayari tumeisha mshauri Mama, kama hoja Hivyo kama HII sauti ni sauti ya kweli, na kama vipi 2025, ataona ni parefu, hakuna ubaya, akikapisha kale ka Copy kule kaje huku kutufungulia ruksa nyingine zote zilizobakia!.

Buriani Ali Hassan Mwinyi, Mwendo Umeumaliza.

inna lillahi wa inna ilayhi rajiun
(إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّ إِلَيْهِ رَاجِعُونَ‎)

Paskali.
My always wish ni kumuona Hussein Mwinyi akishika Uraisi wa Jamhuri. I see him kufanya makubwa sana ila sasa ndio sijui kama itakuw hivyo. Nadhani Magufuli alikuwa anamuandaa kuwa Mrithi wake baada yake.
 
Kuna kipindi alipwaya mpaka Nyerere aliamua kumsaidia.

Alishindwa kabisa kucontrol bunge , serikali ilikua inaanguka.

Anyways nitamkumbuka kwa kuuza Loliondo kwa waarabu.

Familia yake ina bahati sana ya Uongozi ila ni vilaza.
sio alishindwa ku control Bunge, aliridhia Demokrasia ichukue nafasi yake

Wabunge wengi kupitia G55 walipiga kura kuridhia kurejeshwa serikali ya Tanganyika ambayo hadi leo inaliliwa, Mwinyi akajadiliana na PM wake Malecela na Katibu Mkuu wa Chama Horace Kolimba wakaona bora waridhie kilio cha wengi

kuna Machawa wakamjulisha Mwl Nyerere ndio mbio mbio akaomba iitishwe Kikao cha Wabunge cha CCM walati huo Wabunge wote ni CCM akaomba awahutubie kwa kuwa kule Bungeni hatambuliki kisheria

ndio akawaibukia akatibua mpango akawaambia mkitaka Serikali 3 kwanza mjitoe CCM kwa kuwa sio sera ya Chama , wakati huo ukijitoa CCM kama vile umejitoa uhai na mchezo ukaishia hapo wa Serikali 3


Unaemwita Kilaza hakuwa na lugha za kukera wala kufedhehesha ila naamini kama kwny familia yako wangepewa fursa ya kuchagua Baba kati yako na Yeye kwa kura za siri angepita kwa kura za ushindi wa Tsunami
 
My always wish ni kumuona Hussein Mwinyi akishika Uraisi wa Jamhuri. I see him kufanya makubwa sana ila sasa ndio sijui kama itakuw hivyo. Nadhani Magufuli alikuwa anamuandaa kuwa Mrithi wake baada yake.
JPM alimtaka ndio awe Samia wake na aliwahi kulisema hadharan JPM mwenyewe, sema yule Mzee akiekuwa na jina la Mgombea kwny mfuko wa koti pia alikuwa na jina la Makamu wa Rais na akafanikiwa kumshawishi Mgombea urais kubadiki jina la Makamu wake kwa mujibu wa hayati Mwamba mwenyewe
 
Azimio la Zanzibar lilileta mageuzi,yakiwemo ya upatikanaji wa bidhaa muhimu,ambazo kipindi Cha bwana haambiliki zilikuwa kama anasa.

RIP Baba wa demokrasia,licha kwamba kule Kigoma kwenye Kura za ndio idadi ya Kura ilizidi idadi ya wapiga kura.
 
Back
Top Bottom