..nimeona kwamba intake ya 1982 waliingia wanafunzi 50 lakini walio-graduate ni 24.
..hapo maana yake ni kwamba zaidi ya nusu ya wanafunzi walioanza masomo hawakufanikiwa kumaliza.
..kwa maoni yangu, hapo kuna failure rate kubwa ambayo waalimu wa Muhimbili walipaswa kujiuliza sababu yake ni nini.
..Je, tatizo ni wanafunzi? Au tatizo ni course work na wahadhiri? Tungekuwa kwenye nchi za wenzetu lazima watu wangedai majibu ya maswali hayo.
..Wakati UDSM wanataka kuanzisha Faculty of Engineering walitafuta ushauri toka kwa timu iliyoongozwa na Prof wa Kirusi. Suala moja waliloliangalia lilikuwa ni either course iwe ya miaka 3 au 4, na iliamuliwa iwe miaka 4 ili kuepuka wanafunzi wengi kushindwa masomo. Nadhani walijifunza kutoka Nairobi University ambako walipata tatizo hilo, au UDSM walianza na course ya miaka 3.
..La mwisho, kama wanafunzi wengi wanafeli na kuacha masomo, je wale wanaoendelea na kuhitimu ufaulu wao ni wa kiwango gani?