Umenijibu kama vile mimi ni mtoto mdogo wa mtaani. Naomba usinionehivyo; mimi ni mwalimu wa vyuo vikuu kwa takriban miaka 34 sasa. Nimeshafundisha siyo Tanzania tu, bali hata New Zealand, na sasa Marekani, kwa hiyo haya maoni yako ya mawazo ya kimaskini weusi wenye wivu siyo kweli kabisa. Nimeshasidia vijana wa watanzania wengi sana kusoma marekani, na wengine wao leo ni maprofesa hukuhuku marekani. Kwa hiyo jua kuwa mimi siyo maskini, na vile vile ninafurahi sana kusaidia wengine wafikie hapa nilipo.
Napenda uelewe tena kuwa katika elimu usitegemee kupewa maksi za kushinda kwa mambo ya kukariri ukadhani kuwa hiyo ndiyo elimu, kazi ya elimu kukujenga skills za kutafsiri unayofundishwa darasani ili kuyafanya yatatue matatizo halisi ya maisha. Kama nilikufundisha kuwa mashine moja ya 240V: 250kW utatumia transformer yenye current capacity kiasi gani, ninategemea pia kuwa nikuuliza mashine tano za namna hiyo utatumia transformer ya namna gani. Siyo ukariri jibu la mashine moja tu. Iwapo ungekuwa mwanafunzi wangu na una attitude hii, ni kweli ningekukamata na kuchekelea sana. Chuo kikuu siyo choo ambacho hata inzi anaweza kuingia na kutoka!