Buriani Rosemary Kambarage Nyerere

Alidisco 1982 na akamaliza Advanced Diploma Mzumbe 1989!Miaka saba? Kwamba alikuwa anapiga vyombo Kama Bro Mako halafu na Mifeg! Kumbe alikuwa dada wa mineli.Bila shaka kwenye pochi ungekuta nali.RIP dada Rose.
 
Alikuwa na Boy friend baadae akawa baba mtoto wake. MR. JAMES MWAIPOPO.
 

..nimeona kwamba intake ya 1982 waliingia wanafunzi 50 lakini walio-graduate ni 24.

..hapo maana yake ni kwamba zaidi ya nusu ya wanafunzi walioanza masomo hawakufanikiwa kumaliza.

..kwa maoni yangu, hapo kuna failure rate kubwa ambayo waalimu wa Muhimbili walipaswa kujiuliza sababu yake ni nini.

..Je, tatizo ni wanafunzi? Au tatizo ni course work na wahadhiri? Tungekuwa kwenye nchi za wenzetu lazima watu wangedai majibu ya maswali hayo.

..Wakati UDSM wanataka kuanzisha Faculty of Engineering walitafuta ushauri toka kwa timu iliyoongozwa na Prof wa Kirusi. Suala moja waliloliangalia lilikuwa ni either course iwe ya miaka 3 au 4, na iliamuliwa iwe miaka 4 ili kuepuka wanafunzi wengi kushindwa masomo. Nadhani walijifunza kutoka Nairobi University ambako walipata tatizo hilo, au UDSM walianza na course ya miaka 3.

..La mwisho, kama wanafunzi wengi wanafeli na kuacha masomo, je wale wanaoendelea na kuhitimu ufaulu wao ni wa kiwango gani?
 
siyo kwamba Rosemery Nyerere alidisco hivihivi bali figisu zilitaka kufanyika ili aendelee lakini nakumbuka kuna Lecturer mmoja toka Jamaica alisimama kidedea mpaka Rosemery aling`oka, nakumbuka kama alikamatwa masomo mawili
Sasa hivi kuna mtoto wa mkuu mmoja anaitwa Jesca M

 

Kozi ya udaktari ilikuwa inachukua zaidi ya miaka minne. Sidhani ya 1982 ilikuwa ya miaka mitatu. Masomo ya high school kama yanaendeshwa vizuri, yanatosha sana kumpa nafasi ya kusoma engineering kwa miaka 3. Kuna baadhi ya watanzania waliojiunga na vyuo vikuu vya UK na kumaliza degree zao katika kipindi cha miaka mitatu. Miaka minne nadhani ilitumika kutoa exposure kwa mwanafunzi na vilevile kurudia fundamentals.

Kwa maoni yangu, wanafunzi wa Tanzania wangeweza kusoma kama wanafunzi wa UK. Kama kuongeza basi mwaka mmoja wa remedial ungetosha. Lakini hapo hapo ukumbuke, kulikuwa na mwaka mmoja wa jeshi. Na kuna kipindi mtu alitakiwa kwenda jeshini na baada kufanya kazi kwa miaka miwili kabla ya kwenda University.

Kuhusu Nairobi University sina taarifa zao ilikuwaje. Lakini na wao walibadili mfumo wa elimu na kufuta high school. Waliingia kwenye 8 ya primary-4 ya Secondary - 4 ya University.

Tukirudi kwenye Universities zetu, hao wanafunzi wali-fail kama wangesoma Marekani, wengeendelea vizuri sana. Mfumo wetu wa elimu una watu wenye roho mbaya tu. Sidhani maprofesa wetu wa miaka ya 1980 walikuwa mabingwa kuliko maprofesa wa second tier universities hapa Marekani....
 
Duuu
 

..asante kwa mchango wako.

..suala la miaka 3 vs 4 nilikuwa nazungumzia kuhusu Faculty of Engineering of Udsm.

..kabla ya kuanzisha kitivo hicho, walitafuta wataalam wa kuwashauri, na urefu wa muda wa masomo ni moja ya kipengele kilichojadiliwa.

..Nadhani timu hiyo ya wataalamu iliangalia Nairobi Univ na ikakuta wanafunzi wanafeli sana na kozi yao ni ya miaka 3, hivyo wakashauri kozi ya Engineering mlimani iwe ya miaka 4.

..ni kweli kama unavyosema wako waTz waliokwenda kusoma Eng Uingereza miaka ya 70 na walimaliza ndani ya miaka 3.
 

Nadhani walichofanya faculty of engineering kilikuwa kitu kizuri sana. Kwa sababu failure sio tatizo la mwanafunzi pekee yake. Sijuhi kuna mtu ambaye anajua failure rate ya miaka ya sasa.
 
Maprofesa wa Muhimbili ndio hao wanaopata uprofesa kwa utaratibu wa annual increment. Ni watu waliojipa utukufu au umungu-mtu toka siku nyingi. Soma cv zao. Mtu anaajiriwa akiwa na degree ya kwanza anaanza na cheo cha lecturer, ukiuliza utaambiwa MD ni zaidi ya digrii ya kwanza! Mtu mwenye masters degree anapewa uprofesa, ukiuliza utaambiwa "masters ya medicine ni zaidi ya PhD". Usitarajie maprofesa wenye arrogance ya aina hii wafurahie kuona mtu akikaribia kuwafikia kitaaluma, lazima wafanye figisu.
Nadhani mpaka sasa hivi ni Muhimbili pekee ndiko kwenye maprofesa wasiokuwa na PhD.
 
UDSM ya magenius kama KABUDI na MWAKYEMBE teh teh teh.

Yaani ninamuamini mbunge msukuma kuliko Prof au Dr wa hicho chuo cha JALALANI UNIVERSITY.
Kabudi alishastaafu halafu alijitoa ufahamu,udsm siyo jalalani.Miaka hiyo ya 1960s hadi 1990s udsm ilikuwa chimbuko la fikra na wanamapinduzi.Wakati wa Dar School pale kulikuwa kumenoga,John Garang,Emanuel Kivuitu,Walter Rodney ,Wanna Dia Wamba,Museven wa kipindi kile siyo huyu M7 mpenkoni,Kimambo,Haroub Othman Miraji,Kweka,Shivj nk walikuwa watu,ngoja nimwongeze na Matiko Matare na Gervas Mkili,hakika usingeweza kupaita Jalalani.
 
nlisikitika sana bodi ya mkopo iliyakataa matokeo ya wanafunzi wa faculty flani pale DIT kisa 3/4 ya wanafunzi walikua wamezingua..
 
nlisikitika sana bodi ya mkopo iliyakataa matokeo ya wanafunzi wa faculty flani pale DIT kisa 3/4 ya wanafunzi walikua wamezingua..
DIT ya 2004 kurudi nyuma ilikuwa balaa, hv yule raisi wa 2004 yuko wapi sasa hv.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…