Buriani Rosemary Kambarage Nyerere

mleta mada kwanini unadhani mtu kuja chuo na gari ni mbwembwe ? unataka wote tufanane maisha ?
 

mkuu usimtetee huyo mjinga, nchi hii haitokuja kuendelea kama vyuo vikuu vina wajinga kama huyo Kumbuka elimu tumeitoa kwa wazungu ila wazungu wenyewe hawapo hivo, sisi tunachanganya elimu na roho mbaya
 

mkuu hukumuelewa uliyemjibu,msome tena utamuelewa
 
Maswali mazuri; mimi ninajua Engineering ya miaka ya 80 na mwanzoni wa 90. Tatizo kubwa lililokuwapo engineering ni kuwa course nyingi za Engineering zilikuwa zinahitaji link ya moja kwa moja kati yake na ya masomo ya high school. Kwa upande wake sheria na Commerce siyo hivyo; kwa maana nyingine scores za high school zinasaidia mwanafunzi kujiunga na masomo ya sheria au biashara, lakini hata asiyekuwa na score hizo bado anaweza kumudu kozi hizo kwa vile ni kama zinaanza fresh kuanzia mwanzo.

Kwa upande wa kozi za Engineering na nadhani hata Medicine na Science hizi zinaendelea kuanzia pale mwanafunzi alipoachia high school. Sasa ile link kati ya elimu ya high school na hizi kozi ndiyo ilikuwa hafifu kwa baadhi ya wanafunzi. Engineering inahitaji foundation nzuri ya Mathematics na Physics moja kwa moja kutoka high school; na hii haikuletwa na waalimu "weusi wenye roho mbaya" bali ni system iliyoletwa na waalimu wajerumani alioanzisha faculty ile. Waalimu wengi "weusi wenye roho mbaya" walikuwa ni matunda ya hao wajerumani.

Unaweza kukuta mwalimu anaingia darasani akitegemea kuwa mwanafunzi tayari ana misingi fulani ya Physics na Math halafu kumbe hali halisi haiko hivyo; kwa hiyo mwalimu anaweza kufundisha matumizi ya Maxwells laws za Electromagnetics kwenye design of electrical machines, kumbe mwanafunzi huyo haijui hiyo Maxwell's Law ikoje- nadhani unanielewa. "Cream nzuri" ni relative term, best student kutoka high school anaweza kuwa amepata 5/10 wakati engineering inahitaji mtu aneyapata 8/10; sasa iwapo high school hazitatoa 8/10, basi wale wa 5/10 ndio watakaochukuliwa, na ni lazima wakumbane na msukosuko huo.

Kuna wanafunzi kadhaa waliodisco engineering, wakajiunga na IDM Mumbe na kupasua sana huko.
 
Nimepata somo murua, na nimeona ukweli yote uliyosema, afu nahisi wee ni mhadhiri wa chuo, tena huko nje.
Sio kwa madini haya lol, [emoji120][emoji120][emoji120]
 
mkuu usimtetee huyo mjinga, nchi hii haitokuja kuendelea kama vyuo vikuu vina wajinga kama huyo Kumbuka elimu tumeitoa kwa wazungu ila wazungu wenyewe hawapo hivo, sisi tunachanganya elimu na roho mbaya
Hukufundishwa na waalimu wajerumani pale engineering UDSM wewe; tuliofundishwa nao hatusemi hayo unayosema wewe. In fact Mkolela alikuwa anafundisha katika style ya kijerumani kabisa; huwezi kupasi mtihani wa mwalimu wa kijerumani kama umekariri !
 

Asante Sana Kichuguu:

Toka nikiwa mtoto nilitamani kuwa injinia. Kwa bahati mbaya sikufaulu kwenye shule za ufundi au za sayansi. Lakini nilifanikiwa kuingia Dar Tech FTC electrical engineering. Wengi waliokuja walitoka Technical Secondary schools wakiwa division I na II. Na wengi walikuwa na pass nzuri za primary schools.

Kwa sababu sikuwa na msingi mzuri wa kuchukua masomo ya ufundi na kwa sababu nilikuwa nataka kwenda Mlimani, ilibidi nifanye kazi ya ziada kujiandaa na kuwa mbunifu. Nilipoangalia matokeo ya wanafunzi waliotutangulia, niliona kuwa wanafunzi wengi waliopata F kwenye mathematics, walipata F kwenye electrical machines na Transmission. Hivyo tulipomaliza calculus ilibidi nifanye revision ya masomo kama basic electricity au circuit theory ambayo tulifundishwa kwa kutumia formulas. Hii ilisaidia sana kufanya mitihani yangu ya mwisho vizuri.
 


Failure rate ilikuwa kubwa sana. Wanafunzi wa mwanzo waliojiunga UDSM kutoka Dar Tech. waliboronga mpaka zikawekwa conditions kuwa mtu wa kutoka Technical college ni lazima awe na B ya Math na average ya B ya masomo yote. Lakini wengine waliokwenda nje walifanikiwa.
 
Vyuo vingi vya nje hufundisha Calculus na Linear Algebra chuoni, siyo high school; kwa hiyo unapokwenda huko, utarudishwa tena kwenye ile math uliyopitia high school Tanzania kabla hawajaanza kukupika katika engineering. Kwa vile Tanzania tulikuwa na term tatu za PT na sehemu kubwa ya muda wa first year kwa Workshop Technology, mambo ambayo vyuo vingi vya nje haviweki kwenye mitaala yao, tulihitaji sana ile foundation ya high school ili kukamilisha kozi ya engineering kwa miaka minne!
 

Ni kweli unayosema. Tanzania nilisoma engineering math...na ilikuwa na topics zote na waalimu walikuwa sio wazuri kabisa. Nilipotoka nje nilisoma calculus tatu kama kozi za kujitegemea, linear algebra, discreet math, probabilities kama masomo yaliyojitegemea. Na Physics ilibidi isubiri mpaka calculus 1 imalizike kwanza. Mwaka wa pili ndipo tulipoanza kuchukua specialization.
 
Exactly! mambo ndivyo yalivyo huko nje; kumbe wewe umeshapitia tanuru hilo utakuwa unalielewa vizuri sana.

Wanafunzi wenye misingi mizuri niliowahi kuleta marekani kutoka Tanzania walikuwa wanakuwa tishio sana madarasani kwao, lakini hata wale ambao hawakuwa na misingi mizuri bado walifanikiwa pia baada ya kujijenga upya kwa kurudia masomo hayo ya Math na Physics college level.
 

Nilipitia na kuona tofauti kubwa sana. Hila nilifanya uzembe na kukwepa probability. Miaka ya mwisho nili-struggle kidogo kwa sababu masomo mengi mapya yalianza kutoka kwenye classic math. Hivyo ilibidi nitumie misuli.
 
Moja kati ya mawazo ya kimasikini sana tuliyonayo watu wengi weusi; wivu; hatupendi wengine wafikie tulipo; halafu wakikamatwa wanafunzi wengi hivyo mwenyewe anasikia RAHA, umasikini wetu ni wa kujitakia kwa sehemu kubwa.
Ni kweli mkuu, ila kiuhalisia saivi tuna wasomi wengi ambao walikariri elimu lakini hawakuelimika.. pia wengi wao wanategemea janja janja nyingi katika kufaulu, sasa unapowaondolea uwezekano wa janja janja na ukiwapiga fair kabisa unadaka wengi!.. sasa hapo niambie tatizo ni la nani??
 
wakiwa huko nje walikua wanajishughulisha kama walivyokua hapa bongo!?.. sikatai kua kuna tatizo, ila naamini tatizo kubwa linakua kwa wanafunzi kupenda mteremko na baadae wakifeli kutafuta mtu wa kumpa lawama.. ma lectuters pia hua hawapendi hicho kitu maana kiuhalisia kina-wa discredit!
 
Mhadhiri au mwalimu akifundisha halafu wanafunzi wengi wakafeli huyo mwalimu ndiye hajui kufundisha na si tatizo la wanafunzi.
Hapana, kama ni wanafunzi kutoelewa si wanafaa kuuliza!?.. mi naona ni tatizo la wanafunzi mkuu!.. hawajishughulishi
 
Kwanza, amesema katika 50 wamegraduate 24, na hao 26 walishindwa kwasababu mbalimbali ikiwemo ada kuhama course na baadhi disco! ila sio wote ni disco.

Pili, faculty ya Engineering na ya medicine sio kama faculty za business n.k, hizo faculty ni ngumu sana sio TZ tu bali kote duniani, sasa mwanafunzi anapo-trip mara nyingi inakua ni buriani..

Tatu, wanafunzi wengi wakifika ngazi ya chuo kikuu mambo mengi nje ya kusoma huongezeka ikiwemo starehe na kubweteka ambayo naamini hua yanaathiri hata weledi wa masomo.

Nne, wanafunzi wengi chuo wanadumbukia kwenye dimbwi la kufanya uhuni na janja janja ili kufaulu wakikamatwa hawa hua ni disco mkuu.. mfano, nilipata kuwa msimamizi msaidizi katika chuo flani, imagine katika wanafunzi 86, wa5 walikamatwa na simu katika siku 2 za mtihani na karibu 18 kama sikosei walikamatwa na vibuti/precursor/nondo.. hao ni waliokamatwa mkuu, naamini kuna ambao hawakukamatwa, sasa niambie hawa wote ukiwa disco tatizo ni la nani!?.

Mwisho, ni kua chuo kikuu asilimia 65 ya maarifa mtu anatakiwa awe na uwezo wa kuyatafuta yy mwenyewe, na 35 atapewa na muhadhiri na anaposhindwa kitu amfuate muhadhiri.


Sikatai kua kuna wanaofelishwa makusudi mkuu, wapo wengi ila hawafiki hata ¼ ya darasa husika.
 
Kwanza, amesema katika 50 wamegraduate 24, na hao 26 walishindwa kwasababu mbalimbali ikiwemo ada kuhama course na baadhi disco! ila sio wote ni disco.
Hapana sikutaja suala la ada tulikuwa tunasoma bure, bure kabisa hadi nauli ya kwenda na kurudi (return ticketi) tulikuwatunapewa tena wenzetu toka mikoa ya kusini hasa Mtwara (lindi haikuwepo) walikuwa wanakatiwa ticketi za ndege . Ilizoeleka ukipewa single warrant umefukuzwa kwa hiyo waliokuwa wana-disco walikuwa wanapewa single warrant.

Tabu ya wanafunzi wakati huo ilikuwa ni pamba kali, mavazi yalikuwa hakuna, hakuna kabisa so, mwanafunzi akivaa jeans au cordrray alikuwa anaheshimika kuliko mhazili, kama nilivyosema mwanzo watoto wa mameneja ndo walikuwa tishio. walikuwa wanakuja na pamba kali, mameneja wa RTC, NMC , BAT n,k watoto wao walikuwa wanakuja na ukwasi balaa. Mtoto wa Rais hakufua dafu kwa watoto wa mameneja hao.

Kwa mkutadha huo wewe kama wazazi wako ni hohehae inabidi uwe mpole NA USOME SANA ila upande wa pili watoto wa mameneja ndo walikuwa wanaongoza kwa ku-disco pengine ilichangiwa na chuki iliyotokana na makidai yao.

Ada ilikuwa hakuna wakati huo tabu ni hiyo tu. Kuanzia mwaka 1979 baada vita ya uganda lilitokea agizo la miezi 18 ya hali ngumu, nchi iliishiwa nguo zikawa hamna kabisa watu wakusini walivaa hadi mifuko ya mbolea,hata mwanachuo wa kusini utamwona vaa yake seruali waliweka vilaka.
 
duh......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…