Buriani Rosemary Kambarage Nyerere

Buriani Rosemary Kambarage Nyerere

Hapana sikutaja suala la ada tulikuwa tunasoma bure, bure kabisa hadi nauli ya kwenda na kurudi (return ticketi) tulikuwatunapewa tena wenzetu toka mikoa ya kusini hasa Mtwara (lindi haikuwepo) walikuwa wanakatiwa ticketi za ndege . Ilizoeleka ukipewa single warrant umefukuzwa kwa hiyo waliokuwa wana-disco walikuwa wanapewa single warrant.

Tabu ya wanafunzi wakati huo ilikuwa ni pamba kali, mavazi yalikuwa hakuna, hakuna kabisa so, mwanafunzi akivaa jeans au cordrray alikuwa anaheshimika kuliko mhazili, kama nilivyosema mwanzo watoto wa mameneja ndo walikuwa tishio. walikuwa wanakuja na pamba kali, mameneja wa RTC, NMC , BAT n,k watoto wao walikuwa wanakuja na ukwasi balaa. Mtoto wa Rais hakufua dafu kwa watoto wa mameneja hao.

Kwa mkutadha huo wewe kama wazazi wako ni hohehae inabidi uwe mpole NA USOME SANA ila upande wa pili watoto wa mameneja ndo walikuwa wanaongoza kwa ku-disco pengine ilichangiwa na chuki iliyotokana na makidai yao.

Ada ilikuwa hakuna wakati huo tabu ni hiyo tu. Kuanzia mwaka 1979 baada vita ya uganda lilitokea agizo la miezi 18 ya hali ngumu, nchi iliishiwa nguo zikawa hamna kabisa watu wakusini walivaa hadi mifuko ya mbolea,hata mwanachuo wa kusini utamwona vaa yake seruali waliweka vilaka.
Shukrani mkuu kwa kunikosoa.
 
Kwa wale tulioingia Chuo Kikuu cha Dar-es –Salaam faculty of Medicine enzi hizo intake ya mwaka 1982 tutamkumbuka ndugu yetu huyu mcheshi sana Rosemery Nyerere.

Miaka hiyo intake moja ilikuwa inachukua wadahiliwa 50 na majina yote tulikuwa tunayakuta kwenye gazeti la daily news gazeti la serikali. Basi mwenzetu huyu alifanikiwa kuwa mojawapo wa wateule wachache waliofanikiwa kuingia katika intake ya mwaka 1982 July. Katika intake hiyo tuliofanikiwa kumaliza tulikuwa 24, wengine either walidsco, waliacha tu au walibadilisha course jukwaku.

Rosemary Nyerere hakufanikiwa kumaliza kwani walimdiscontinue mwaka wa pili. Baada ya hapo aliajiriwa Print park kama sikosei.

Wakati huo Dean of faculty alikuwa ni Professor Honnoli sijui kama yuko hai , siyo kwamba Rosemary Nyerere alidisco hivihivi bali figisu zilitaka kufanyika ili aendelee lakini nakumbuka kuna Lecturer mmoja toka Jamaica alisimama kidedea mpaka Rosemary aling`oka, nakumbuka kama alikamatwa masomo mawili.

Timu wa walimu wetu enzi hizo ninaowakumbuka ni Professor Massawe, Mwaluko, Makene, Karashani, Kimati, Hiza, Msele na Shaba hawa ndo ninawakumbuka.

Tulikuwa tukiishi Muhimbili na kula cafeteria chakula kizuri kweli ambacho kwa sasa hata mkurugenzi hali, Mfano wali kwa kuku na saa nyingine kuku wa kukaanga,ugali na mbogamboga n.k

Rosemary hakuwa kabisa na mbwembwe zozote kama watoto wa Ma-rais wa sasa kama Yule wa Chalinze, alikuwa ni mwanafunzi wa kawaida kabisa na wala usingemdhania ni mototo wa Rais. Cha kushangaza watoto wa mameneja wakati huo ndo walikuwa wanatisha mfano kuna mtoto alikuwa ni wa meneja wa RTC akuwa anakuja na gari Peugeot 504.

Kama Rosemary Nyerere ametangulia mbele za haki basi Mungu amlaze mahala pema na ninakumbuka kama aliwahi kuwa Mbunge wa kuteuliwa au Viti Maalumu mwaka 2000-2005.
Dah basi wazeya na wakongwe tumo wengi humu, halafu huyu prof mwaluko kumbe wa Kitambo sana, kanifundisha na baadae kamfundisha mwanangu.
 
Ila sasa hivi ukileta swaga hizo za mavazi nk na cigarette pensi Fupi nini utaishia kuitwa mhuni tu na kufungiwa
Namkumbuka Rosemary Nyerere. Alipenda uhuru wake na kuvaa anachotaka, including zile pensi fupi sana za jeans. Na sigara yake aliipenda sana. Na ulabu. Na kujichanganya na masela.
Sikuwahi kusikia wala kumwona mtu yeyote akitajwa kama boyfriend wake. Hakushobokea kabisa hizo vitu
 
Kwa wale tulioingia Chuo Kikuu cha Dar-es –Salaam faculty of Medicine enzi hizo intake ya mwaka 1982 tutamkumbuka ndugu yetu huyu mcheshi sana Rosemery Nyerere.

Miaka hiyo intake moja ilikuwa inachukua wadahiliwa 50 na majina yote tulikuwa tunayakuta kwenye gazeti la daily news gazeti la serikali. Basi mwenzetu huyu alifanikiwa kuwa mojawapo wa wateule wachache waliofanikiwa kuingia katika intake ya mwaka 1982 July. Katika intake hiyo tuliofanikiwa kumaliza tulikuwa 24, wengine either walidsco, waliacha tu au walibadilisha course jukwaku.

Rosemary Nyerere hakufanikiwa kumaliza kwani walimdiscontinue mwaka wa pili. Baada ya hapo aliajiriwa Print park kama sikosei.

Wakati huo Dean of faculty alikuwa ni Professor Honnoli sijui kama yuko hai , siyo kwamba Rosemary Nyerere alidisco hivihivi bali figisu zilitaka kufanyika ili aendelee lakini nakumbuka kuna Lecturer mmoja toka Jamaica alisimama kidedea mpaka Rosemary aling`oka, nakumbuka kama alikamatwa masomo mawili.

Timu wa walimu wetu enzi hizo ninaowakumbuka ni Professor Massawe, Mwaluko, Makene, Karashani, Kimati, Hiza, Msele na Shaba hawa ndo ninawakumbuka.

Tulikuwa tukiishi Muhimbili na kula cafeteria chakula kizuri kweli ambacho kwa sasa hata mkurugenzi hali, Mfano wali kwa kuku na saa nyingine kuku wa kukaanga,ugali na mbogamboga n.k

Rosemary hakuwa kabisa na mbwembwe zozote kama watoto wa Ma-rais wa sasa kama Yule wa Chalinze, alikuwa ni mwanafunzi wa kawaida kabisa na wala usingemdhania ni mototo wa Rais. Cha kushangaza watoto wa mameneja wakati huo ndo walikuwa wanatisha mfano kuna mtoto alikuwa ni wa meneja wa RTC akuwa anakuja na gari Peugeot 504.

Kama Rosemary Nyerere ametangulia mbele za haki basi Mungu amlaze mahala pema na ninakumbuka kama aliwahi kuwa Mbunge wa kuteuliwa au Viti Maalumu mwaka 2000-2005.
Kama ni Me wewe ni kaka yangu kama Ke wewe ni dada mkubwa wa kwetu 1982? Ndiyo namaliza Std VII!! Shikamoo kaka!
 
Hapana sikutaja suala la ada tulikuwa tunasoma bure, bure kabisa hadi nauli ya kwenda na kurudi (return ticketi) tulikuwatunapewa tena wenzetu toka mikoa ya kusini hasa Mtwara (lindi haikuwepo) walikuwa wanakatiwa ticketi za ndege . Ilizoeleka ukipewa single warrant umefukuzwa kwa hiyo waliokuwa wana-disco walikuwa wanapewa single warrant.

Tabu ya wanafunzi wakati huo ilikuwa ni pamba kali, mavazi yalikuwa hakuna, hakuna kabisa so, mwanafunzi akivaa jeans au cordrray alikuwa anaheshimika kuliko mhazili, kama nilivyosema mwanzo watoto wa mameneja ndo walikuwa tishio. walikuwa wanakuja na pamba kali, mameneja wa RTC, NMC , BAT n,k watoto wao walikuwa wanakuja na ukwasi balaa. Mtoto wa Rais hakufua dafu kwa watoto wa mameneja hao.

Kwa mkutadha huo wewe kama wazazi wako ni hohehae inabidi uwe mpole NA USOME SANA ila upande wa pili watoto wa mameneja ndo walikuwa wanaongoza kwa ku-disco pengine ilichangiwa na chuki iliyotokana na makidai yao.

Ada ilikuwa hakuna wakati huo tabu ni hiyo tu. Kuanzia mwaka 1979 baada vita ya uganda lilitokea agizo la miezi 18 ya hali ngumu, nchi iliishiwa nguo zikawa hamna kabisa watu wakusini walivaa hadi mifuko ya mbolea,hata mwanachuo wa kusini utamwona vaa yake seruali waliweka vilaka.

Asante kwa kurudi na kutoa mchango wako. Kilichonistua mimi ni rate of failure ya wanafunzi wa medicine wakati nchi ilikuwa na watu karibu ya 20 milioni na hospitali zingine za wilaya zilikuwa hazina daktari mwenye digrii. Pili walitoka na kwenda kusoma nje, walirudi na digrii zao. Something was amiss.
 
Kwanza, amesema katika 50 wamegraduate 24, na hao 26 walishindwa kwasababu mbalimbali ikiwemo ada kuhama course na baadhi disco! ila sio wote ni disco.

Pili, faculty ya Engineering na ya medicine sio kama faculty za business n.k, hizo faculty ni ngumu sana sio TZ tu bali kote duniani, sasa mwanafunzi anapo-trip mara nyingi inakua ni buriani..

Tatu, wanafunzi wengi wakifika ngazi ya chuo kikuu mambo mengi nje ya kusoma huongezeka ikiwemo starehe na kubweteka ambayo naamini hua yanaathiri hata weledi wa masomo.

Nne, wanafunzi wengi chuo wanadumbukia kwenye dimbwi la kufanya uhuni na janja janja ili kufaulu wakikamatwa hawa hua ni disco mkuu.. mfano, nilipata kuwa msimamizi msaidizi katika chuo flani, imagine katika wanafunzi 86, wa5 walikamatwa na simu katika siku 2 za mtihani na karibu 18 kama sikosei walikamatwa na vibuti/precursor/nondo.. hao ni waliokamatwa mkuu, naamini kuna ambao hawakukamatwa, sasa niambie hawa wote ukiwa disco tatizo ni la nani!?.

Mwisho, ni kua chuo kikuu asilimia 65 ya maarifa mtu anatakiwa awe na uwezo wa kuyatafuta yy mwenyewe, na 35 atapewa na muhadhiri na anaposhindwa kitu amfuate muhadhiri.

Sikatai kua kuna wanaofelishwa makusudi mkuu, wapo wengi ila hawafiki hata ¼ ya darasa husika.

..asante kwa mchango wako.

..mimi niko hapa kuongeza wigo wa mjadala wetu na kujifunza.
 
dah basi wazeya na wakongwe tumo wengi humu, halafu huyu prof mwaluko kumbe wa Kitambo sana, kanifundisha na baadae kamfundisha mwanangu

R.I.P Prof. MWALUKO

It pains us deeply to inform you of the loss today of our University Vice Chancellor, Professor Gabriel Paul Mwaluko, who passed away on Tuesday 19th November, 2013 in Apollo Hydrabad India where he had been undergoing medical treatment.

Prof. Mwaluko who was born in 3rd August, 1945 was a holder of MB. Ch.B Degree of the University of East Africa at Makerere obtained in 1969, Msc (Clinical Pharmacology) and PhD (Pharmacology) from Manchester University obtained in 1972 and 1975, respectively.
 
Ni kweli kabisa Rosemary Nyerere baada ya discontinuation ya medicine pale Muhimbili baade alikwenda kusoma IDM Mzumbe na ali - graduate May 1989 with Advance Diploma in Professional Accountancy (ADPA) with honor akiwa "Ameua" - amepiga A's course zote. July 1989 Alipangiwa kazi kama Assistant Lecturer pale IFM (now a days IFM University) na kuanza kufundisha course za Accountancy mwaka wa kwanza na na wa pili.

Nakumbuka alikuwa rafiki na mcheshi na mtu wa kujichanganya kwa wote na hata wanafunzi wake. Pale IFM (kule nyuma ya jengo) siku hizo kulikuwa na mgahawa unaendeshwa na serikali ya Wanafunzi (almaarufu kama "MUWATA") ulikuwa ukiuza supu, chips kuku, mishakaki, bia, soda. Nakumbuka pale ilikuwa ni kijiwe alichokuwa akikipenda sana ambapo utamkuta akifurahi baada ya classes zake akipiga bia yake na sigara yake mkononi. Kwa hakika bado namuona akiwa kwenye tabasamu yake, upole na ustaarabu wake na sauti yake nyororo.

Nakumbuka alikuwa ni dada mmoja aliyekuwa akishughulishwa zaidi na mambo yake mwenyewe na ya watu aliyatazama tu na kuyaacha kama yalivyo. Na pia namkumbuka siku hizo kama mdada aliyekuwa akipenda kujichanganya kwenye vijiwe vya wanaume zaidi kuliko wanawake wenzie.

Bwana akutangulie katika safari yako.

RIP Rosemary Nyerere.
Sigaraaa????[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
 
Bro, sijakujibu wewe; nazungumzia hayo mawazo na mipango ya hao walimu wa chuo kikuu. Wewe umeandika kile kilichokua kinafanyika vyuoni, ukweli ni maeneo mengi. Ukiingia hata ofisi za serikali nyingi hata sasa, sio watu wa kutatua shida bali wanatengeneza ugumu wa wewe kupata solution ya tatizo, mfano hata TRA leo hi, the way wanavyo kusanya KODI is as if hawataki biashara ziendelee. Unajua hadi mwaka 1998 idadi ya wahasibu walikua na CPA (T) nchi nzima walikua hawafiki 3000? Sasa hiyo kama sio roho mbaya ni kitu gani?

Siamini kwamba wote wale walikua wanafeli eti hawakua na uwezo, sio kweli; baadhi yao hao walio disco vyuo vyetu wamekwenda nje ya nchi na wakawa the bet students, shida sio KUKARIRI; tunalo tatizo period
Mtu anaweza feli lakini akipata second chance akijitambua anatoboa .Kwamba walifeli hapa wakaenda kutoboa nje haiondoi uwezekano wa wao kufeli kihalali.
 
Umenijibu kama vile mimi ni mtoto mdogo wa mtaani. Naomba usinionehivyo; mimi ni mwalimu wa vyuo vikuu kwa takriban miaka 34 sasa. Nimeshafundisha siyo Tanzania tu, bali hata New Zealand, na sasa Marekani, kwa hiyo haya maoni yako ya mawazo ya kimaskini weusi wenye wivu siyo kweli kabisa. Nimeshasidia vijana wa watanzania wengi sana kusoma marekani, na wengine wao leo ni maprofesa hukuhuku marekani. Kwa hiyo jua kuwa mimi siyo maskini, na vile vile ninafurahi sana kusaidia wengine wafikie hapa nilipo.

Napenda uelewe tena kuwa katika elimu usitegemee kupewa maksi za kushinda kwa mambo ya kukariri ukadhani kuwa hiyo ndiyo elimu, kazi ya elimu kukujenga skills za kutafsiri unayofundishwa darasani ili kuyafanya yatatue matatizo halisi ya maisha. Kama nilikufundisha kuwa mashine moja ya 240V: 250kW utatumia transformer yenye current capacity kiasi gani, ninategemea pia kuwa nikuuliza mashine tano za namna hiyo utatumia transformer ya namna gani. Siyo ukariri jibu la mashine moja tu. Iwapo ungekuwa mwanafunzi wangu na una attitude hii, ni kweli ningekukamata na kuchekelea sana. Chuo kikuu siyo choo ambacho hata inzi anaweza kuingia na kutoka!
Huyu mzee anaujima mwingi....... Class ina watu 150, unafelisha wote wanafaulu 15, na unajisifu ety unafundisha si bora uache tuu hiyo kazi... Kwahiyo wote hao hawana akili isipokuwa ww tu.... Acheni roho mbaya

Sent from my 5023F using JamiiForums mobile app
 
Umerudia lawama ambazo nimeshajibu huko nyuma; halafu madarasa ya enzi zile yalikuwa na watoto 20 hadi 35 tu siyo hii ya 150 ambayo hata mwalimu hawezi kuwa na contactna wanafunzi wake ( student.
 
Sio tu akiwa hai bali akiwa Rais wa nchi

Kuna Mkuu wa Shule alimpiga barua ya kumwita Mzazi mtoto wa Nyerere…alipofuatwa kuulizwa akajibu nimemuita Julius Nyerere Mzazi wa Mwanafunzi sio Rais

Huyo ni Mama Siwale alikuja kupata Uwaziri wa Elimu

Baadae nae akaja kutumbuliwa kwa kosa la kupeleka Uwaziri chumbani akiwa na Mumewe

The rest is history
Huyu mama alikuwa ngangari kwelikweli, alimpelekea waziri mkware "mwanae" ili alale nae maana yule wazir rip alikuwa anawalazimisha wakuu wa shule kutoa binti alale nae wakati akitembelea shule. Waziri akahamaki akataka kumtisha huyu mama yeye thabita akapiga simu ikulu waziri akapigwa chini.
 
Daah

Siku hizi kina Halima Mdee ndio Iron lady wa uchumi wa Kati

Huyu Siwale na Bibi Titi Mohamed ndio ma Iron Lady nlowahi kuwashuhudia hapa Bongo

Huyu mama alikuwa ngangari kwelikweli, alimpelekea waziri mkware "mwanae" ili alale nae maana yule wazir rip alikuwa anawalazimisha wakuu wa shule kutoa binti alale nae wakati akitembelea shule. Waziri akahamaki akataka kumtisha huyu mama yeye thabita akapiga simu ikulu waziri akapigwa chini.
 
Umerudia lawama ambazo nimeshajibu huko nyuma; halafu madarasa ya enzi zile yalikuwa na watoto 20 hadi 35 tu siyo hii ya 150 ambayo hata mwalimu hawezi kuwa na contactna wanafunzi wake ( student.
Ni kweli madarasa yalikuwa ni level seat wanachuo si zaidi ya 40, lakini letu lilikuwa na watu 49 mmoja toka Kigoma hakufika chuoni na nyumbani hakurudi inasemekana amepotea hadi leo. Madarasa ya sasa vyuo vikuu siyo madarasa bali ni mikutano wa hadhara.
 
Hata Isack Newton alipopewa Ubunge hakuwahi kuongea Bungen zaid ya kumuomba Jiran yake afunge dirisha kuna baridi kali nje

Mie kwangu huo ndio uthibitisho kuwa alikuwa na akili kubwa
Na wakat anamwambia jirani yake afunge dirisha alikuwa anafanya verification if air resistance is an effect to periodic time of a pendulum clock
 
Back
Top Bottom