Kwanza, amesema katika 50 wamegraduate 24, na hao 26 walishindwa kwasababu mbalimbali ikiwemo ada kuhama course na baadhi disco! ila sio wote ni disco.
Pili, faculty ya Engineering na ya medicine sio kama faculty za business n.k, hizo faculty ni ngumu sana sio TZ tu bali kote duniani, sasa mwanafunzi anapo-trip mara nyingi inakua ni buriani..
Tatu, wanafunzi wengi wakifika ngazi ya chuo kikuu mambo mengi nje ya kusoma huongezeka ikiwemo starehe na kubweteka ambayo naamini hua yanaathiri hata weledi wa masomo.
Nne, wanafunzi wengi chuo wanadumbukia kwenye dimbwi la kufanya uhuni na janja janja ili kufaulu wakikamatwa hawa hua ni disco mkuu.. mfano, nilipata kuwa msimamizi msaidizi katika chuo flani, imagine katika wanafunzi 86, wa5 walikamatwa na simu katika siku 2 za mtihani na karibu 18 kama sikosei walikamatwa na vibuti/precursor/nondo.. hao ni waliokamatwa mkuu, naamini kuna ambao hawakukamatwa, sasa niambie hawa wote ukiwa disco tatizo ni la nani!?.
Mwisho, ni kua chuo kikuu asilimia 65 ya maarifa mtu anatakiwa awe na uwezo wa kuyatafuta yy mwenyewe, na 35 atapewa na muhadhiri na anaposhindwa kitu amfuate muhadhiri.
Sikatai kua kuna wanaofelishwa makusudi mkuu, wapo wengi ila hawafiki hata ¼ ya darasa husika.