Vijana.. ngoja niwaache....
Lakini maisha ni zaidi ya ngono, starehe na mengineyo. Kwanza naona wengi wenu mmechanganya kati ya Nguvu za Kiume na Uhanithi. Sasa kuchanganya huko kumewatoa kabisa nje ya Mada.
Zaidi ya yote, tafuteni pesa. Haya majigambo ya nguvu za kiume mkifikia umri wetu, mtagundua hakuna kitu mmepata kwa kuwa na nguvu za kiume.
Hebu fikirieni kwa mfano. Mtu Mwenye nguvu za kiume anapopata tatizo la kumaliza hiyo nguvu ya kiume na yeye hana pesa, anabakiwa na nini? Kwenye ulimwengu huu ili maisha yaende unatakiwa uwe na uwezo wa kuyaendesha ni lazima uwe na rasirimali na kwa ulimwengu wa sasa, ni PESA.
Zamani mababu zetu waliokuwa na wake wengi walikuwa na mashamba makubwa pia, leo huna hela hizo nguvu zako atazitaka nani? Mwanamke anakuja kwako unashindwa kumlisha, kumvisha na kumtimizia mahitaji yake mengine, unadhani utaweza kummiliki kwa kuwa tu unamfurahisha kitandani?