Bus kuwa VIP linatakiwa kuwaje maana kuna moja nimepanda hakuna tofauti kubwa na la kawaida

Bus halikuwepo wakati nakata tiketi , lilikuja baadae muda wa kusafiri ulipokaribia
Ungeanzisha timbwili yani umeshapanda unaanza kuwauliza choo kiko wapi..?
kama hakipo unawaambia unamwaga inya kuanzia mwisho wa bus mpk kwa dereva!.
unang'aka haswa kama hakuna na AC unawaambia unavunja dirisha!.
yani unahakikisha hukamatiki hivyo vi juice na biscuit unakataa unapiga zogo unataka ugali nyama!..🤣
 
[/QUOTE]
Na mie leo najiunga na wa CHAI hii

Sababu haujataja Jina la kampuni na ukisafiri kutoka wapi kwenda wapi.

Unajua JF ipoje? 😉
Wanajijua wenye hizo huduma . Wajirekebisha wataje huduma za kweli na sio kuongezea za uongo ambazo hazipo.
 
Kwa nchi hii ya watawala Wagagagigikoko na wachumiatumbo. basi likishaandikwa "VIP BUS" ubavuni mwake, tayari linakuwa VIP mkuu. Nchi ya kipuuzi sana hii.
 
Nilikata VIP ya Kigoma-Saratoga ili nishukie Tabora.
Wakati wa kusubiria gari nikaingia KB Lounge Mbezi nikagonga vyombo nikijua sitapata shida ya kuchimba dawa. Nilijuta na siipandi tena.

Juzi nimetoka Masasi na VIP-Mining Nice. Hakuna cha internet wala refreshments. Choo kipo ila abiria wamejaa hadi wamekaa mlango wa chooni. Nimewadharau sana wenye gari.
Jana nimepanda BM VIP ya Arusha ya saa tatu. Hawa nawaa maua yao. Kila kitu walichoandika kipo. Huduma nzuri sana.
Kesho nitapanda Nacharo ya Tanga. Nitaleta mrejesho.
Angalizo. Sipo hapa kuaribu biashara ya mtu ili hii iwe iama changamoto na ifanyiwe kazi
 
Kwa nchi hii ya watawala Wagagagigikoko na wachumiatumbo. basi likishaandikwa "VIP BUS" ubavuni mwake, tayari linakuwa VIP mkuu. Nchi ya kipuuzi sana hii.
Oyaaa! kitambo my mom used to call me mgagagigikoko hii ina maana gani?
 
VIP

2 x 2

Huduma:
Bites
Vinywaji
AC
TV
Jamaa alitaka agonge ugali nyama mboga saba km kwa shilole.
Huwa najikazasana kutokula njiani.
Siku tunaenda Dom enzi za BM Chalinze pale pembeni tulifakamia ile mibata maji, huku tuliambiwa ni kuku kienyeji, mpaja km mguu wa mtoto, nikala chipsi yai kuku kienyeji hata sikumbuki km lilikua la mbuni lile.
Ila hataakuumwa tumbo, msosi ndo ulikua hadithi.
 
Bus halikuwepo wakati nakata tiketi , lilikuja baadae muda wa kusafiri ulipokaribia
Mkuu pole sana,mi nilikua mbio nirudi dar na mishe zangu niko mbeya kwanza tukuyu huko.
Nafika mbeya stand nikakamatishwa Abood ya kutoka tunduma sa tatu inaingia na siti nikapewa.
Ile kuingia ndani hamna siti.
Nilikalia kiroba cha mchele mpk bongo.
na tulipita pale moro saa nzima+ garage kwao.
Nilijuta.
Sijawai kupanda tena mabus.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…