Busara kidogo inahitajika katika hili

Baba mwenyewe alisema ulikuwa ni ujana na anajutia, hivyo it was never My Ma's fault..!
Kumbe...basi asikusumbue. Nachukia wanaume wa hivi alijua kabisa ana mtoto mahali kilichomkimbiza ni kipi na kilichomrudisha ni kipi?? apambane na hali yake. Msamehe ndio lakini hakuna namna nafasi aliyoipoteza muda wote huo aje aipate kirahis rahis tu.Nina dada yangu nae ana kesi kama hii mwanae yupo chuo sasa et baba mtu ndio anakuja alafu sasa anamtafuta mtoto kwa kuibia ibia.

Wanaume wanaokimbia watoto jaman mkikimbia msirudi mnaumiza sana watoto wenu hata kama mama mtu ndio alikosea mtoto/watoto wanahusika vipi? Yaani mtu unakua na sababu gani hasa usilee mwanao?? Mambo yakiwa magumu huko ndio mnarud ooh mwanangu nisamehe hii kitu inaudhi mno.
 
Aiseh nilimpoteza mtoto wangy wa kiume kisa mama yake alituchanganya watatu nikakataa nikisema tupo watatu nitaaminije ni mimi!!leo dogo ana miaka tisa kapewa ubin Mwingine!!!hayo ndio maisha aiseh!!!heshimu baba yako tu!!ili upate haki yako!!!
 
Aiseh nilimpoteza mtoto wangy wa kiume kisa mama yake alituchanganya watatu nikakataa nikisema tupo watatu nitaaminije ni mimi!!leo dogo ana miaka tisa kapewa ubin Mwingine!!!hayo ndio maisha aiseh!!!heshimu baba yako tu!!ili upate haki yako!!!
Dah!...pole aisee japo wewe pia ni chanzo kwa kukataa kuwajibika.......na wewe umekubali kabisa dogo apotee kirahisi hivyo ?.....chukua hatua mapema.

Fight for your 'blood' man
 
Hii mada waisome sperm donor wote waliopo humu jf, inasikitisha sana mtu kujifanya anakupenda sasa ilhali alikukana na kukutelekeza tangu mimba🤤🤤, baba mlezi kamsitiri mama yako na wewe pasipo kusita, mthamini na ongea nae juu ya hilo mpe heshima na nafasi yake maana anastahili hilo na abarikiwe sana

Anajipendekeza baada ya kukosa mtoto wa kike tu
 
Ni ngumu kidogo kutoa ushauri wa jumla pasipo kujua haswa kisa kilichofanya baba yako wa kibaiolojia kutengana na mama yako na hatimaye 'kutelekeza' ujauzito/mtoto...

Baba anayekulea ambaye kiuhalisia ndiyo baba yako ana nafasi kubwa ya kushirikishwa hali halisi kuliko kuendelea kumficha...
 
Binti,
Kama ni haki yako ya kumjua baba mama yako ameshakupatia.Kama ni upendo wa kibaba,Umeupata kwa baba yako mlezi.Baba yako mzazi hana haki yoyote ya kujaribu au kukulazimisha umpe nafasi katika maisha yako kama wewe hauko tayari.Maadam ameshakupa contact zake na umeshampa nafasi ya kukuona nafikiri inatosha.

Wewe kwa sasa ni mtu mzima.Unayo haki ya kuamua kiwango cha muingiliano unachohitaji kutoka kwake na kumwambia stop iwapo unahisi anakukera au kukubughudhi.Heshima aliyopewa na mama yako pamoja na baba yako wa kufikia ya kuweka jina lake kwako inatosha kwa sasa.Mengine yanategemea hisia zako na uamuzi wako.

Zingatia kwamba kila uamuzi utaofanya una weza ama kukupa furaha au kukupa huzuni na ushauri wangu kwako ni huu.Usikubali akufanye mateka wa kihisia bali tanguliza furaha yako kwanza.Mpe heshima yake na nafasi yake kwa kadiri ya nafsi yako.

Nakutakie kila la heri na unao moyo mzuri sana kuweza kusamehe.
 
Huwa nawaambiaga Sana wanaume wenzangu kuhusu matukio kama haya, unaishi na mtu mpaka unampa ujauzito then either unamfukuza au unamtafutia sababu uachane nae...later unakuja kudai haki yako uliyokuwa huna mpango nayo na kuona si kitu.

Carleen Una haki kusema chochote juu ya huyo Biological father mpaka ulipo sasa, don't hurt that Baba Mlezi hata iweje muombe Mungu akujaalie katika hilo, najua you make wise decision on this.
 
Kabisaa baada ya kukosa mtoto wa kike ndo kakumbuka kuna sehemu alipanda mbegu ila sio kwa mapenzi maana angekua na binti kwa mkewe nako asingekumbukwa kabisaa!!huyo amerudi tu purposely ila hana mapenzi

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Just like you said, "nidhamu" could be relative too. Kile ambacho kwako hakifai, kwa mwingine kinaweza kuwa ni cha kawaida kabisa. Na pia, mila zako sio lazima zifanane na mila za mleta mada.

Jifunze kuchukulia poa mambo mengine. Too much imagination inakupunguzia uwezo wa kupuuza mambo ambayo yanastahili kupuuzwa. Nakubaliana na wewe, hili liishie hapa.

I rest my case!
 
Mwambie baba mlezi ukweli and make sure unawakutanisha

Na unamweka baba mzazi wkenye nafasi yake na kumweleza sifa zote ulizotuambia hapa za baba mlezi

Hiyo itampa mlezi heshima na amani na mzazi atajua nafasi yake

Hakuna kitu kibaya Kwa mwamaume kama akijua unamficha vitu

Na hasa kama amesacrifice maisha yake Kwa ajili yako

Btw…. Mbona hii story inajurudia sana humu jf?

Mbona kama hii issue ilishakua solved na member mmoja veteran humu?
 
Nitazungumza na Baba this Pasaka, nitaona kile atasema..!
Unajua huyo baba mlezi anaweza akaacha uamue lakini ikamuumiza sana.
Natamani huyu baba mzazi abaki tu kama mgeni mualikwa ktk maisha yako yote!
Ili uwe na amani pia,kwanza ht hao ndugu zako na mkewe kwa baba mzazi sidhani kama wanaupendo nawe maana hapo ukute wanawaza umefata Materials things!achana nao
Situation yako ilimtokea mdogo wangu kwa mamdogo 34yrs back ,mbaba alikataaga mimba!
Yule mzee anajiweza sanaa kimaisha ni mkulima mkubwa anauza mpk nje huko ila hanaga mtoto mpk Leo.
Mamdogo alifariki mda mrefu sana dogo anatumia jina La huyo mzee na la mwisho ni ukoo wa kina mama...
Sasa miaka ya hivi karibuni akaanza kumtafuta mwanawe aliyemkataaga kipindi hiko ,akaanza kumtafuta mamdogo mwingine mpenda hela akampanga vzr wakamfata binti kumueleza kua baba ake Mara sijui vipi na vipi kabla hajamaliza akasema "stop mamamdogo,sina baba ktk hii dunia,na staki kwa namna yoyote mumtaje huyo mtu nimekubali sina baba na ntaishi bila baba,kwa maisha niliyopitia ya kuishi bila baba mzazi Leo sihitaji mwingine baada ya kupata shida zote aseme Mimi ni mwanawe na akamuambia odo ukitaka tukosane ongelea huyo mzee,simjui na sihitaji kumjua mpk naingia kaburini na sina deni kwa Mungu"
Vikamshuka mpenda hela yule na yule mzee hata alipokuja na pesa zake Dogo amekaza wajomba wakasema maamuzi tunamuachia yeye aamue sisi hatuna usemi maana mama ake amefariki 1994 toka kipindi hajajitokeza na bad enough walikua wote mkoa hukoo baada ya mamdogo kufariki walienda kuzika kina mama wakarudi wakamuacha mtoto wakiamini baba ake atamfata kumbe alivyofata huku nyuma na baadhi ya watu akasema sio mwanangu simtaki,na enzi zile hakuna simu aliishi maisha ya kichokoraa km miezi miwili mama angu mzazi Mimi siku moja akasema ngoja niende nikaangalie dogo anaishije ,mkoa anauliza pale home anaambiwa hawajui alipo ikabidi aanze kumsaka kesho yake anamkuta maeneo ya stendi anaomba omba mama akamchukua wakaja nae Dar akasomeshwa na wajomba na sasa ana ajira yake na ameolewa na mume mzuri tu.
Sio story Carleen ni uhalisia upo ktk familia yetu kabisaa!

Kuna mwanaume waselfish Sana'a mwishowe wanaambulia majuto makubwa na wewe pia usiwe selfish acha baba mlezi afaidi matunda yake
Be wise in ur decision kuhusu hilo jambo

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Thank you!

Well said

Yaani huyo mzee anawez hata kujuta na kupata msongo

But he won’t say because he doesn’t want to hurt the girl
 
Pole sana , ukirudi kwenye psychology ni dhahiri kuwa mtoto wa kike upendwa sana na baba na pia binti umpenda baba sana , sasa hapa ndiyo tatizo lilipoanzia ulishaathirika na upendo wa baba mlezi since ukiwa mdogo na hivyo ni vigumu huo upendo kuugeuza.

Sasa si shida ila jua kumtenga baba yako mlezi itakuchukua mda sana na inahitaji njia za kisaikolojia sasa usifike huko kaa na baba mzazi , mueleze scenario nzima ila mjulishe haumtengi ila mko wote , baada ya hapo jitaidi kuongeza mawasiliano naye kupunguza lawama .

Kwa hivyo nahisi itakuwa Sawa na maisha yataendele .after all he is your real father

Pole sana ni ugonjwa wa saikolojia ila tiba yake ni hiyo.
 
Hii dunia inazunguka kwa kasi sana, nampa pole baba mzazi.

Off the topic:

Nina kaka yangu yeye alikua na mwanamke akaambiwa ana mimba ya huyo mwanamke jamaa kapambana akalea mimba hadi kujifungua. Picha ikaanza mtoto wa kiume kazaliwa mweupe pee na jamaa ni mweusi tii na binti ni mweusi tii.

Sasa rumours zikaanza mtoto si wajamaa, jamaa akaanza upelelezi mwanamke akakaza kuwa mtoto ni wake. Baada ya mwaka mtoto anazidi kubadilika, weupe unakolea hana sura ya mama wala ya baba. Ndipo jamaa akakomaa kua wakapime DNA mwanamke akaruka maili mia.

Jamaa akasema kama umegoma kupima DNA ya mtoto mie sitatoa na wala sitajihangaisha na gharama za mtoto. Kumbuka Hayo walifikiana wakiwa dawati la jinsia.

NB. Huyo bro ana familia yake na huyo mwanamke alikua ni mchepuko wanafanya wote kazi. Jamaa likawa funzo kwake hapigipigi hovyo tena saivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…