Busara kidogo inahitajika katika hili

Busara kidogo inahitajika katika hili

Hey guys..!
Huwa napenda kuja hapa na uchiinga' wa hapa na pale, ila naombeni Leo niwe serious kidogo, hii ni issue ya kweli kabisa ya maisha yangu..!!

Sijui kwanini nataka kushare kama ni ushauri nitaupokea, ila kama kuna la kujifunza mtu aweza lichukua pia likamsaidia..

Mimi ni kati ya watu wachache waliobahatika kulelewa na 'baba mlezi' kwa ule upendo ambao lije jua, ije mvua I am 100% sure siwezi upata popote pale, I hate to call it Him baba mlezi, ila huo ndiyo ukhalisia..!!

Na bahati nzuri nilipewa bahati ya kujua ukweli nikiwa mdogo, Baba hakupenda hili jambo lakini kama ningekuja kujua sasa nadhani ningedata kabisa kujua Huyu Mwanaume anayenipenda kuliko chochote kuwa He is not My Real Father...!

Nakumbuka nikiwa mdogo kabisa, nilikuwa natazama photo album ya Mama ya zamani, Nika point picha mojawapo ya mkaka ambaye alikuwa ananifanania sana sana, nikamuambia 'Mama, bila shaka huyu ndiye Fulani' (hapa nilimtaja baba mzazi kwa jina lake)..

Mama alicheka akauliza umejuaje.?? Nikamuambia nimeona tu tunavyofanana, akaniambia ni kweli ni yeye..! Hilo likaishia hapo na ni sura ya ujanani kabisa, hivyo nikabaki na wazo tu kuwa Me and that man we real look alike, maisha yakaendelea hivyo..!!

Baba mlezi ndiye Baba ambaye nimekua nikijua huyu ndiye dunia yangu, He is so proud ov Me na hivi tuko na lighting color wote, hivyo nikitembea naye natambulishwa almost everywhere like she is my first daughter, na watu wakiona hiyo rangi angavu wanajua kabisa ndiyo ni kweli na husema kabisa mmefanana hasa..!

Katika wanaume I can admit wameni spoil ni this Man, na ukubwa wangu huu imagine that man bado ananiita 'my happiness' 'totoo', 'my everything'..! ana watoto wengine wa kike kwa kiume lakini the whole family inajua kipenzi cha Baba ni nani..!

Katika watu naogopa kuumiza maishani mwangu ni huyu mwanaume, Imagine, alinambia 'binti yangu, usije kuniaibisha', hayo maneno huwa natembea nayo chochote nachofanya nawaza nisije m-dissapoint yule mwanaume, japo ni muda mrefu ila huwa yanaishi moyoni mwangu daima..!!

Baada ya yote hayo, nikiwa binti mkubwa kabisa mwaka Jana mwishoni, napokea simu ya mtu anajitambulisha kuwa Mimi ni mwanae, kwanza I was shocked sababu najua baba yangu nilishapiga naye story mchana, mpaka aliponitajia jina ndiyo nikaelewa..!!

Nikajikuta nalia machozi, sijui ni kwanini nililia vile, anyways, nilizungumza naye kwa nidhamu na utulivu mkubwa nikawa namsikiliza, akaniambia anaomba sana samahani kwa kuniacha miaka yote hiyo, na alikuwa akinitafuta sana bila mafanikio ila hivi sasa ndiyo kafanikiwa kunipata..!

Anaomba sana samahani, kwa kuniacha, kutokuwa pale kwa ajili yangu na pia kwa kumuumiza Mama, na kinachomuuma hakufanikiwa kupata mtoto wa kike huko alikokwenda Mimi ndiyo bintiye wa pekee, kapata watoto wa kiume woote..!!

Huruma ni kweli alikuwa anatia me nikamuambia Mimi sina tatizi lolote na wewe, ila kwa jinsi ulivyomuumiza yule Mama sijui ni kitu gani utafanya mpaka tu akuelewe na kukusamehe maneno uliyomtamkia na jinsi ulivyomuacha Mimi nikiwa tumboni na nikuambie tu ukweli hajawahi kusahau..!

Akawa anataka tuonane japo anione tu, nikamuambia ongea kwanza na Mama, ndiyo naweza nikakuona japo kwa sehemu tulizokuwepo tulikuwa jirani kiasi ila sikuweza tu kwenda kumuona bila ruhusa, na pia sikutaka kabisa kumshirikisha hili Baba nilihisi tu kama atajiskia vibaya, sijui ni kwanini nilifikiri hivyo, kama nilivyosema mwanzo sikutaka nimfanye ajiskie vibaya kwa ajili yangu kwa namna yoyote ile,

Mpaka Leo sikuwahi muambia Baba yangu chochote na yeye hakuwahi niuliza chochote japo Mama alishamuambia kuwa baba mzazi kanitafuta, Nadhani anasubiri kama nitamuambia chochote ila Mimi siwezi muambia kitu kiukweli..!!

Japo kiukweli niliwahi enda kumuona baba mzazi, I was just curious kumuona na ni kitu nilikuwa natamani sana, I can admit he is very charming person kama Mimi anapenda kufurahi mno pia.! Ila nimekaa naye na kuongea naye it's like talking to a stranger, ana maisha yake tu anajiweza lakini Ile furaha hupata nikiwa na Baba yangu mlezi it was never there.! tulifanikiwa kuongea mengi na kupiga story na akawa anajutia sana lakini on my side nilimuambia ni sawa tu nilishamsamehe..!

Tatizo linaanzia wapi, sahii analalamika anataka ule ukaribu na bond ya Baba na Mwanae, anahisi namtenga, anahisi sijamsamehe, lakini sina tatizo naye ni kuwa almost every day the only Man that came into my mind ni Baba Mlezi, the only Man niwe na siku nzuri ama mbaya lazima nimuambie na ni lazima anitafute ama nimtafute, na ukubwa huu lakini ni kawaida kuona 'Imethibitishwa' zake kwa simu yangu, huwa ananitreat bado kama vile Mimi ni kabinti kadogo, mpaka niliwahi muambia nikija olewa nitahakikisha naolewa na mwanaume anayenipenda at least nusu ya upendo wako, akacheka akaniambia tu Muombe Mungu sana na ulivyo tu huyo mwanaume kazi atakuwa nayo, nikamuambia wewe ndiyo umeniharibu lakini, akatabasamu akajibu, ipo siku nitakuja kuelewa..!

Kabla nisahau, Mama hataki ushirika naye kabisa anasema Baba anayemtambua yeye ni Baba Mlezi tu, japo yeye pia alimuambia ashamsamehe hivyo asijali aendelee na maisha yake kwa amani, Naomba nikazie hapa My Ma hajawahi nizuia Mimi kuwasiliana wala kumuona Baba sababu ni yeye ndiye alipambana nitumie jina la Baba mzazi alisema hataki nipoteze haki ya kumjua baba mzazi pia, na alikuwa anaimani sana kuwa ipo siku baba yako mzazi atarudi tu na utamuona, na kweli yakatimia..!!

tukirudi huku kwa baba mzazi, analalamika mpaka namuonea huruma lakini sipati ile feeling ya ubaba juu yake what am I supposed to do.? Na huwa ananitumia pesa za hapa na pale ananiambia vocha namuambia tu ahsante, hata ile kuita 'Baba' naona ugumu, me huwa naishi zangu kama vile he doesn't exist, nikikumbuka ni mara moja namjulia hali mpaka nikumbuke tena siyo Leo, most of the time yeye ndiye hunitafuta na malalamiko juu anahisi nafanya kusudi kumkomoa lakini hapana, moyo wangu unaishi huku kwingine toka utotoni..! anataka nikawajue ndugu zake lakini I don't feel like I do belong there, kawapa ndugu zake namba wananitafuta lakini siwafurahii all the same pia, na kumsamehe nishamsamehe lakini the bond ain't there, na malalamiko yake yananiumiza lakini nimeshindwa yafanyia kazi..!!

Nashindwa hata nimfanye nini maskiini..!!
Utopolo...!
 
Natumaini unaona hizo sehemu nilizoBold na kuweka strikethrough
-
Kwa tamaduni zetu za kiafrika mtu ambae unamuheshimu kama mzazi hutakiwi kumu-Address kama ulivyofanya hapa, kwa muono wangu sidhani kama inaleta picha nzuri kumuita baba yako mzazi au mlezi "Huyu Mwanaume" hilo ni jina analoweza kuita mama yako pekee. Otherwise Ukifanya kama ulivyofanya hapa wengine wanaweza kuhisi kuna hali ya incest kati yenu. Maybe ndio maana nae inakua rahisi kukuita "Toto langu"

I'm so sorry for saying this to you I might be wrong too but my point is pinned to the fact that the way you address your father figure is not Healthy. Change!!!!
______
Rolling to the main topic!!

Kuna Father na Daddy, Father anatia mimba hajali Mtoto atakua vipi na kuishi vipi...Daddy anatia mimba na kujali kiumbe hicho alicholeta duniani kwa "Kuwepo" pembeni ya kiumbe huyo siku zote. Kwa maelezo ulivyoeleza huyo aliyekuzaa he was your father but wasn't your Daddy. Anachokifanya ni kutaka kula mavuno ya shamba ambalo hakulipalilia, jambo hili Hata Mungu kakataza. Maana anasema...

Mathayo 25:24,28,30
[24]Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya;
[26]Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;
[27]basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.
[28]Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.
[30]Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Btw Kwakua hatujajua kisa cha mzazi halisi kukutelekeza basi Siwezi mlaumu. Ila cha msingi ongea na mama yako akupe kisa chote cha baba yako kukuacha kisha msikilize na baba yako pia upande wako then wewe mwenyewe utaamua cha kufanya. Choose wisely

Obvious naamini baba yako anachotaka ni kupata recognition ya kua wewe ni mtoto wake if so basi mpatie. Mjulie hali hata kwa simu mara moja moja mtembelee, ila mapenzi kwa baba mlezi usipunguze kamwe.
WOW
You have made my day.
It is very rare to read a wonderful and fantastic comments like this in a JF.
Nice counselling
Love of God be with you mate.
Good Day.
 
Pole sanaa lakini kikubwa shukuru Mungu umepata upendo wa baba mlezi. Hakuna kitu kinachompa mtoto ujasiri,,,akili nk. Kama upendo. Bond ya familia inatokana na upendo na si vingine.

Hata kwenye familia ya baba na mama watoto wengi wanawapenda mama ,,sababu ya bond muda mwingi mama anakuwa na watoto,,,atawajulia hali atawapikia chakula,,,lkn utakuta wababa wengi wapo busy na kutafuta hela. Shule anaenda mama,,mambo madogo madogo ndo yanaleta bond. Mwisho wa siku wanakuja jilaumu na kusingizia kuwa mama anawalisha sumu. Kama mtoto ulimwonyesha upendo toka mdogo amekua anauona na kuuishi hata mama amlishe sumu kiasi gani. Upendo utaishi moyoni mwa mtoto. Tofauti na hapo ni lawama zisizo na msingi.
 
Hahahaa...
Mmenichangamsha mpaka nimecheka tena..!
kale ka Uzi niliwahi ku comment mwanzoni kabisa lakini nilivyoona kananipeleka jehanum peku peku nikafuta na ile comment kabisa..!
Wapi tena? But please forgive and forget. I have also forgiven so many people who have wronged me here. Forgive, let go and move on.
Let's concentrate on your issue, I really need to talk to u privately. U really need someone special, caring and my words of encouragement will help u
 
Natumaini unaona hizo sehemu nilizoBold na kuweka strikethrough
-
Kwa tamaduni zetu za kiafrika mtu ambae unamuheshimu kama mzazi hutakiwi kumu-Address kama ulivyofanya hapa, kwa muono wangu sidhani kama inaleta picha nzuri kumuita baba yako mzazi au mlezi "Huyu Mwanaume" hilo ni jina analoweza kuita mama yako pekee. Otherwise Ukifanya kama ulivyofanya hapa wengine wanaweza kuhisi kuna hali ya incest kati yenu. Maybe ndio maana nae inakua rahisi kukuita "Toto langu"

I'm so sorry for saying this to you I might be wrong too but my point is pinned to the fact that the way you address your father figure is not Healthy. Change!!!!
______
Rolling to the main topic!!

Kuna Father na Daddy, Father anatia mimba hajali Mtoto atakua vipi na kuishi vipi...Daddy anatia mimba na kujali kiumbe hicho alicholeta duniani kwa "Kuwepo" pembeni ya kiumbe huyo siku zote. Kwa maelezo ulivyoeleza huyo aliyekuzaa he was your father but wasn't your Daddy. Anachokifanya ni kutaka kula mavuno ya shamba ambalo hakulipalilia, jambo hili Hata Mungu kakataza. Maana anasema...

Mathayo 25:24,28,30
[24]Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya;
[26]Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;
[27]basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.
[28]Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.
[30]Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Btw Kwakua hatujajua kisa cha mzazi halisi kukutelekeza basi Siwezi mlaumu. Ila cha msingi ongea na mama yako akupe kisa chote cha baba yako kukuacha kisha msikilize na baba yako pia upande wako then wewe mwenyewe utaamua cha kufanya. Choose wisely

Obvious naamini baba yako anachotaka ni kupata recognition ya kua wewe ni mtoto wake if so basi mpatie. Mjulie hali hata kwa simu mara moja moja mtembelee, ila mapenzi kwa baba mlezi usipunguze kamwe.
Umetoa ushauri mzuri.
 
Kabisaa baada ya kukosa mtoto wa kike ndo kakumbuka kuna sehemu alipanda mbegu ila sio kwa mapenzi maana angekua na binti kwa mkewe nako asingekumbukwa kabisaa!!huyo amerudi tu purposely ila hana mapenzi

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
Na hapo anaumia sana kuona baba mlezi anapendwa na kuthaminiwa
 
Wakati mwingine kukubali Mimba sio rahisi kihivyo!!mnajikuta mpo watatu KWA dem mmoja wakati huo huo Hadi unafanya kusitisha MAHUSIANO!!sasabaadae unaambiwa mimba unashtuka!!
Sasa kinachofanya umtafute akiwa kashakua mkubwa ni nini?

Ukishikilia kukana mkane hadi kufa kwako
 
Sasa kinachofanya umtafute akiwa kashakua mkubwa ni nini?

Ukishikilia kukana mkane hadi kufa kwako
Nilikuja kujua badae nimekausha Hadi leo!!japo anateseka Sana KWA taarifa ;!wameshaachana na jamaa ni teja hana makazi maalumu anatelekeza watoto hawana hats chakula!!nilishindwa cha kufanya na mama mtu watoto walitoroshwa hawajulikani walipo!!
 
Hata story yako na hii hazifanani
 
Mbegu za uzazi haziwezi kutengenezwa maabara wacha kutushika maskio MUHENGA feki

Kama hukuzaliwa mazingira hayo huwezi kijua, waswahili wanasema anayekulisha ndo anayekumiliki, why do you respect your parents Kama unao, simply because they you came in this world through them, their responsibility was to feed, raise you and take care of you: kukulisha , kukutunza na kukulea ndo utimilifu wa uzazi wao kwako: Haijalishi what happened between baba na huyo binti, lakin absence ya biological father Kwa huyu binti, it disqualifies him automatically as a father: period:
 
Hey guys..!
Huwa napenda kuja hapa na uchiinga' wa hapa na pale, ila naombeni Leo niwe serious kidogo, hii ni issue ya kweli kabisa
Naona wewe,mama yako na babako mzazi mnamuandalia huyo baba mlezi maumivu yakumtosha na majuto juu.

Endeleeni muda utaongea.
Mnawasiliana naye wa nini sasa?
Mmekosa nini kwa huyo baba mlezi aliyejitoa kwa ajili yenu?
Inashangaza sana na ndio maana singo maza hawaaminiki kabisa huyo mamaako ajiangalie sana angekuwa anathamini upendo wa mume wake angekupiga stop kuwasiliana na huyo wakuitwa baba mzazi kudumisha amani nyumbani kwenu msimuone huyo mlezi wenu mjinga anausoma mchezo
 
Mungu akupunguzie uchungu na maumivu whiterose,
Ahsante..!!
 
UR VERY LUCKY!! Hongera kwa kupata malezi ya baba japo sio baba mzazi. Mimi hapa nimeanza kuishi na baba mzazi nikiwa form one kiukweli paka leo I don’t feel km nina baba yaani ni 0 bond btn Us, sometime tunakaa hata mwaka mzima bila kuonana wala simu mi nahisi labda anasubiri akizeeka hajiwezi ndo aanze kunitafuta.

Please usimuumize huyo baba bora, how I wish yani hayo mapenzi ningeyapata mimi.

All the best dear
 
Relax mkuu. Kuna vitu sio vya kuchukulia serious namna hii. Umewaza mpaka habari za incest, that's too much imagination for such an ordinary storyline!

Back to the topic, nimeona vitu kadhaa:

- Baba mzazi hakufanikiwa kupata mtoto wa kike huko aliko. Ndugu mleta mada, do you really think the old man angekutafuta kama huko aliko angepata mabinti kadhaa? Hata usinijibu hili swali.

- Baba mlezi hajui kama unawasiliana na baba mzazi. You're about to hurt that old man. Sisi wanaume tunakuaga very territorial. Once we have what we consider to be family, haturuhusu another man aingilie chain of command and how we're running the show. Mlezi akigundua baba mzazi is back, and you're sneaking behind his back, ataumia kinoma. Ni either umwambie mwenyewe, au uache ku-hangout na upande wa baba mzazi.

- Hakuna bond kati yako na baba mzazi, zaidi ya baiolojia iliyokuleta duniani. Umekua na undugu na upande wa baba mlezi. Brothers, sisters na wengineo, they all consider you one of their very own. Huko kwa baba mzazi hautaweza kutengeneza bond mpya, na kama ukiweza kuna mahala utavunja kwa ndugu zako wa upande wa baba mlezi. Pick your side wisely sweetheart!

Kwa upande wangu, undugu sio kushare damu. Undugu ni nani yuko na wewe through thick and thin. Nani anaguswa na shida zako? nani anaumia ukipitia magumu? Binafsi, kuna washkaji tu nawathamini kuliko "ndugu". It's because they've got my back when shit goes down!

Nashauri ukae na baba mzazi, umpe ukweli. Mwambie nakutambua mzee, and I do respect you. Ila hatuwezi kua na bond like family. I already belong somewhere else. Kuna watu wamenikuza like one of their own, itakua ngumu kuswitch sides kwa sasa. Tuendelee tu hivihivi.

Ukimaliza hapo, rudi kwa Baba mlezi umpe picha nzima. And maybe, muulize anashauri nini. It will make him feel better, kuliko kukaa kimya huku akiwa anajua kinachoendelea.

NB: kumbe mleta mada uko na light skin sio? Uko na kapicha tuone?
I heart your contribution
Bila shaka hicho kichwa chako ni madini.
 
Back
Top Bottom