Lil sis don't stress yourself; Wala hata usiwaze huyo baba yako anajisikiaje; sio shida zako hata kama umemsamehe.
Baba yako ni mtu selfish; wakati wewe unamuhitaji kwenye maisha yako; yeye hakuwa tayari. Muda huu yeye anakuhitaji wewe na anakulazimishia; sio sawa.
Ukweli ni kwamba sio kila mwanaume ni baba. Kuna watu wengi waliolelewa na baba zao; lakini hicho alicho/anachokupa baba yako mlezi; kuna millions of people hawajawahi kuki_experience. Mshukuru huyo baba yako mlezi sanaaaaa. Hujapata ombwe/ trauma kwa sababu ya kutokulelewa na baba; kwa sababu yeye aliamua kuwa baba ambaye hukuwa naye. Mimi ninajua umuhimu wa uwepo wa baba kwenye maisha ya mtoto wa kike; kwa kukukubali wewe na kukufanya mtoto wake uuuh; kitu kikubwa mnoooo, ni neema.
Tena mama yako mmmh basi tu; mimi binafsi ningekupa na surname ya huyo baba mlezi period; ingebaki tu damu yake kwako maana haiwezi kutolewa. Ubaba sio tu kumwaga mbegu; ubaba ni malezi. Baba ni yule anayejua umekula nini, umevaa nini, umelala wapi; anakupenda, anakujali, anakufundisha, anakuoyna, anakuwa concerned na wewe kwa Kila hali. Ukiumwa, ukiwa na changamoto yoyote; he is always there you. Huyo ndiyo baba na hicho kinacho-form bond kati ya mtoto na mzazi. You are an absentee parent; don't expect any bond with your child
Huyo baba yako mzazi; kaa naye kwa kina mwambie tu you are at peace with him, unamtambua kama baba yako mzazi; ila huwezi kuwa karibu naye kama anavyotamani. Ni mtoto wake kwa kukuzaa; but alishauza hiyo haki kwa mwanaume mwingine.
Nenda kamwambie baba yako mlezi ukweli wote; asije akakuona you are an ingrate. Naamini amefanya Kila kitu kwenye maisha yako kwa sababu ya upendo na sio kungoja shukrani. But kiubinadamu tu; mpe tu shukrani zake; una deni juu yake. Mpe na msimamo wako juu ya huyo baba yako mzazi. Hakikisha baba yako mlezi ana amani juu yako. Don't lose than man, don't hurt him, don't disappoint him. Make him proud; isije siku akasema "mtoto wa watu ni wa watu tu".