Busara kidogo inahitajika katika hili

Busara kidogo inahitajika katika hili

Sio kila stori ina pande mbili. Jamaa kamtelekeza mwanamke na mimba. Halafu akaja kumtafuta mtoto baada ya miaka zaidi ya 20.

Hakuna sababu zitakazokua na mashiko, just lame excuses.
duh! haya mambo yapo sana kwa sisi tunaoishi na masingle mother, ila pia unatakiwa kuelewa kuwa huyo baba ako mzazi aliachana na ur mumy kwa7bu zipi! usukute labda alifumaniwa, au usikute labda huyo baba ako mzazi ndiye aliyeharibu mahusiano yake kayi ya baba mlezi na mama ako
Btw Kwakua hatujajua kisa cha mzazi halisi kukutelekeza basi Siwezi mlaumu. Ila cha msingi ongea na mama yako akupe kisa chote cha baba yako kukuacha kisha msikilize na baba yako pia upande wako then wewe mwenyewe utaamua cha kufanya. Choose wisely
 
Lil sis don't stress yourself; Wala hata usiwaze huyo baba yako anajisikiaje; sio shida zako hata kama umemsamehe.

Baba yako ni mtu selfish; wakati wewe unamuhitaji kwenye maisha yako; yeye hakuwa tayari. Muda huu yeye anakuhitaji wewe na anakulazimishia; sio sawa.

Ukweli ni kwamba sio kila mwanaume ni baba. Kuna watu wengi waliolelewa na baba zao; lakini hicho alicho/anachokupa baba yako mlezi; kuna millions of people hawajawahi kuki_experience. Mshukuru huyo baba yako mlezi sanaaaaa. Hujapata ombwe/ trauma kwa sababu ya kutokulelewa na baba; kwa sababu yeye aliamua kuwa baba ambaye hukuwa naye. Mimi ninajua umuhimu wa uwepo wa baba kwenye maisha ya mtoto wa kike; kwa kukukubali wewe na kukufanya mtoto wake uuuh; kitu kikubwa mnoooo, ni neema.

Tena mama yako mmmh basi tu; mimi binafsi ningekupa na surname ya huyo baba mlezi period; ingebaki tu damu yake kwako maana haiwezi kutolewa. Ubaba sio tu kumwaga mbegu; ubaba ni malezi. Baba ni yule anayejua umekula nini, umevaa nini, umelala wapi; anakupenda, anakujali, anakufundisha, anakuoyna, anakuwa concerned na wewe kwa Kila hali. Ukiumwa, ukiwa na changamoto yoyote; he is always there you. Huyo ndiyo baba na hicho kinacho-form bond kati ya mtoto na mzazi. You are an absentee parent; don't expect any bond with your child

Huyo baba yako mzazi; kaa naye kwa kina mwambie tu you are at peace with him, unamtambua kama baba yako mzazi; ila huwezi kuwa karibu naye kama anavyotamani. Ni mtoto wake kwa kukuzaa; but alishauza hiyo haki kwa mwanaume mwingine.

Nenda kamwambie baba yako mlezi ukweli wote; asije akakuona you are an ingrate. Naamini amefanya Kila kitu kwenye maisha yako kwa sababu ya upendo na sio kungoja shukrani. But kiubinadamu tu; mpe tu shukrani zake; una deni juu yake. Mpe na msimamo wako juu ya huyo baba yako mzazi. Hakikisha baba yako mlezi ana amani juu yako. Don't lose than man, don't hurt him, don't disappoint him. Make him proud; isije siku akasema "mtoto wa watu ni wa watu tu".
Mama malezi umetoa risala hadi imenigusa mie [emoji25][emoji25][emoji25]
Ubarikiwe sana.
 
Baba mzazi hana nafasi kabisa kwenye moyo wako maana imeshazibwa tayari, huenda analipia gharama za kutelekeza majukumu.

Je ukifika wakati wa kuolewa, baba yako mzazi utamshirikisha?, Kama jibu ni ndio je mahari yako (kama ikiwepo) atapokea nani kati ya hao 'baba' wawili ?...au atakayepokea 'ukwe' kati ya pande hizo mbili ?, Na familia ya mumeo, je imtambue nani kama baba mkwe ?

Ni vizuri kuweka haya mambo sawa mapema ili isilete sintofahamu huko mbeleni.
 
Baba mzazi hana nafasi kabisa kwenye moyo wako maana imeshazibwa tayari, huenda analipia gharama za kutelekeza majukumu.

Je ukifika wakati wa kuolewa mahari yako atapokea nani kati ya hao 'baba' wawili ?...au atakayepokea 'ukwe' kati ya pande hizo mbili ?

Ni vizuri kuweka haya mambo sawa mapema ili isilete sintofahamu huko mbeleni.
Hiyo inaeleweka ni haki ya mlezi na huyo ndiye baba, yule mwingine ni mzazi.

Baba ni mlezi, mlinzi, mbeba majukumu na mtoa upendo.

Mzazi ni yule aliyesababisha uzaliwe.
 
Hiyo inaeleweka ni haki ya mlezi na huyo ndiye baba, yule mwingine ni mzazi.

Baba ni mlezi, mlinzi, mbeba majukumu na mtoa upendo.

Mzazi ni yule aliyesababisha uzaliwe.
Haki ya mzazi ni ipi Sasa ?
 
Achana na maugovi yao hao wazazi wewe stick na huyo mlezi mengine mtajua mkifika kwa sir God
 
Back
Top Bottom