Business Class ina raha yake - tafuteni pesa

Endelea kusafiri. Vijana wanaruka na mkeo. Wewe tafuta pesa tuuuu
 
Mkuu nifanyie liteni nile mchana
 
Mie kwa mara ya kwanza nilisafiri daraja la kawaida na Qatar baadaye nikarudi na uae nilifurahi mno nikasema kumbe ndio mana kikwete alikuwa hakatiki angani yaani hao wadada wachangamfu Ile mbaya. Unauliziwa chicken or beef ,watu wanalewa ,wananyonyana mate yaani unaona uko dunia nyingine
 
Safi sana
 
Endelea kubarikiwa kama Id yako isemavyo!
 
Sijui hii ndiyo wanaitaga kuokota dodo chini ya mlimao?

Hukutamani wakosee tena siku nyingine?

Ulifaidi sana!
 
Mambo hayo ๐Ÿ˜
Halafu wanawake wanalaumiwa kupenda pesa๐Ÿ˜€
Pesa inaraha yake jamani
Hakuna maanamke aliyelaumiwa kupenda pesa aliyoitolea jasho la halali.

Lawama ni zile pesa za kitapeli kwa kulegeza mimacho na kutegemea "kitumbua" kama mtaji ukijua kabisa hapa na-cheat. Mbaya zaidi unakamua hadi damu bila huruma.
 
Kitu kimoja ambacho hua mnasahau...

Kupata au kukosa ni majaaliwa yake Muumba.

The way mnavyosema "Tafuteni pesa" mnaifanya ionekane kama sisi tusio na pesa ni kama hatupambani, au tumebweteka, au labda hatuna akili.

Kumbe unakuta sisi tunapambana kuliko nyie sema tu labda bahati haijatuangukia, au hatujakamata izo channel kama zakwenu, au hatujapata mtu wa kutushika mkono nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ