Butiku: Viongozi watambue wanaongoza watu siyo kuku au mbuzi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Akizungumzia haki na uhuru wa watu kuzungumza, Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amesema viongozi wanatakiwa kuthamini utu wa watu, hivyo wana haki ya kulinda uhuru na haki ya kila mtu.

“Kwangu mimi viongozi anatakiwa kutamba kuwa anaongoza watu na siyo Mbuzi, Ng’ombe au kuku,” anasema Butiku na kuongeza kuwa kiongozi ambaye natambui hilo basi huyo si kiongozi.

Amesema “Lazima wakumbuke wanaongoza watu wanaopenda utu, unaweza kulewa kidogo madaraka ukasahau kama unaongoza watu, lakini pia hata wananchi nao wanaweza kuwa na tabia mbaya kama wanamchagua kiongozi na kisha hawamsikilizi.

Chanzo: ITV
 
Huyu babu naye ni mnafiki tu hana lolote
 
Bahati mbaya baadhi ya hao watu wanaona sifa kuwa mbuzi na kuku.

Afadhali hawa wazee wanabaki na misimamo yao, japo ni aibu sana kuona vijana wanaowategemea kusogeza taifa letu mbele, wakiona sifa kuishi kwa kusifia kwa ajili ya matumbo yao.

Kifupi ni kwamba hawa wazee walitutoa kwenye ukoloni, bahati mbaya sasa wanashuhudia kwa macho yao hawa vijana wanalirudisha taifa letu kwenye ukoloni mamboleo, utumwa wa kifikra.
 
Nilijua tu Bashiru Ali hayuko peke yake! Ngoja tuone mwisho wa huu mtifuano.
You might be very right. It seems bashiru ana kundi kubwa nyuma yake maana hawa wazee akina Butiku, Warioba unaona kabisa wanamtetea. Na akina Butiku na warioba, wana kundi lao...ambalo it seems liko against Samia

Definitely alichosema Bashiru ni ukweli, kweli mtupu, LAKINI yeye katika historia ya Tanzania, ndiye amekuwa mtu katili , muuaji, mfungaji watu, mbambikia makosa/kesi watu akitimiza maagizo ya Magufuli. Alimuona magufuli kama Mungu na alimpamba kama wa sasa wanavyompmba Samia anayewawezesha kupata mlo wao.

Likewise, Bashiru alimuabudu magufuli kwa vile alikuwa anapata mkate wake toka kwa Magufuli. Kwahiyo ni mnafiki, siyo kuwa anawaonea huruma wakulima, bali ni kwa vile amekosa mlo aliokuwa anaupata toka kwa Magufduli.
 
Akizungumzia haki na uhuru wa watu kuzungumza, Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amesema viongozi wanatakiwa kuthamini utu wa watu, hivyo wana haki ya kulinda uhuru na haki ya kila mtu.

“Kwangu mimi viongozi anatakiwa kutamba kuwa anaongoza watu na siyo Mbuzi, Ng’ombe au kuku,” anasema Butiku na kuongeza kuwa kiongozi ambaye natambui hilo basi huyo si kiongozi.

Amesema “Lazima wakumbuke wanaongoza watu wanaopenda utu, unaweza kulewa kidogo madaraka ukasahau kama unaongoza watu, lakini pia hata wananchi nao wanaweza kuwa na tabia mbaya kama wanamchagua kiongozi na kisha hawamsikilizi.

Chanzo: ITV
Mungu amlinde Rais Samia. Wabaya wake hawalali kuhakikisha wanamharibia ili aonekane kiongozi dhaifu. Ukweli wateule wake kwa sehemu fulani wamemuangusha ingawa inahitajika saikolojia kukabiliana na ukweli wa mambo ulipo. Mfano tu akimfukuza kazi Nape, Makamba na Mwigulu na Riziwani na Waziri wa Maji basi mambo yanaweza kugeuka fasta na watu wakaanza kumuamini.
 
Kwangu mimi kiongozi anatakiwa kutamba kuwa anaongoza watu na siyo Mbuzi, Ng’ombe au kuku
 
You might be very right. It seems bashiru ana kundi kubwa nyuma yake maana hawa wazee akina Butiku, Warioba unaona kabisa wanamtetea. Na akina Butiku na warioba, wana kundi lao...ambalo it seems liko against Samia
Definitely alichosema Bashiru ni ukweli, kweli mtupu, LAKINI yeye katika historia ya Tanzania, ndiye amekuwa mtu katili , muuaji, mfungaji watu, mbambikia makosa/kesi watu akitimiza maagizo ya Magufuli. Alimuona magufuli kama Mungu na alimpamba kama wa sasa wanavyompmba Sami anayewawezesha kupata mlo wao. Likewise, Bashiru alimuabudu magufuli kwa vile alikuwa anapata mkate wake toka kwa Magufuli. Kwahiyo ni mnafiki, siyo kuwa anawaonea huruma wakulima, bali ni kwa vile amekosa mlo aliokuwa anaupata toka kwa Magufduli.
Dr.Bashiru ni mbunge nashangaa unaandika anakosa mlo, hakuna kitu kama hicho.

Unaposema kwenye historia ya Tanzania Dr. Bashiru amekuwa mtu katili, muuaji watu... kwa ushahidi upi ulionao? hii yako ni mihemko tu.

Dr. Bashiru ameongea pointi ya msingi sana, na hata kama aliwajaza ujinga wakati ule, kama wakati huu anawaambia ujinga aliowajaza haufai muuache, lakini kuendelea kukomalia ule ujinga naona ndio ujinga zaidi.
 
Mungu amlinde Rais Samia. Wabaya wake hawalali kuhakikisha wanamharibia ili aonekane kiongozi dhaifu. Ukweli wateule wake kwa sehemu fulani wamemuangusha ingawa inahitajika saikolojia kukabiliana na ukweli wa mambo ulipo. Mfano tu akimfukuza kazi Nape, Makamba na Mwigulu na Riziwani na Waziri wa Maji basi mambo yanaweza kugeuka fasta na watu wakaanza kumuamini.
Alijichagulia maisha yeye mwenyewe na alipopata madaraka akawa na mihemko ya kumfunika Magufuli! Upumbavu huu utamtafuna mpaka 202 5 na kama anaakili bora asigombee ata pata tabu haijawahi tokea!
 
Mungu amlinde Rais Samia. Wabaya wake hawalali kuhakikisha wanamharibia ili aonekane kiongozi dhaifu. Ukweli wateule wake kwa sehemu fulani wamemuangusha ingawa inahitajika saikolojia kukabiliana na ukweli wa mambo ulipo. Mfano tu akimfukuza kazi Nape, Makamba na Mwigulu na Riziwani na Waziri wa Maji basi mambo yanaweza kugeuka fasta na watu wakaanza kumuamini.
Samia ni dhaifu, kwasababu kama ana wateule wasiojielewa kwanini asiwaondoe?

Nyie waimba mapambio ndio mnazidi kumuharibu Samia, mwambieni ukweli abadilike, sio kumsifia azidi kuwa mjinga.
 
Back
Top Bottom