Butiku: Viongozi watambue wanaongoza watu siyo kuku au mbuzi

Butiku: Viongozi watambue wanaongoza watu siyo kuku au mbuzi

Butiku nA warioba hawajahi kukubali moyoni kuwa nje ya ruling system,, ndo maana tangu awamu ya nne wao wako against serikali,, waliopoa kidogo enzi za JPM maana yule hakuwa na cha msalie mtume,, WANGEPOTEA😂
Wajanja wajanja sn
 
alafu nilichoshangaa kumbe madaraka matamu,msimchukulie poa shangazi angu
 
1671114131652.jpeg
 
Mbuzi na kuku wanafugwa,hawa hawana Uhuru juu ya bwana wao.

Sisi ni raia ambao tunao wajibu Kwa nchi yetu, kwenye kila nyanja, ila unashangaa hapa kwetu kuna kakikundi fulani ka watu wao ndio wanatuamulia nani awe raisi mwaka 2025(hii sanduku la kura ni geresha na kiini macho) yote ni kwaajili ya matumbo yao na kizazi chao.

Katika mijadala mzee mmoja alisema anatamani kama Mungu angekuwa anasikia maombi direct,angekiangamiza kizazi chote cha mafisadi na wahujumu nchi ili tupate kizazi fresh kwa mwanzo mpya.
Kupangiwa maisha inaumiza sanaaa chief.
 
Kwani mzee Butiku hajui kwamba hao viongozi wanatambua kuwa wanawaongoza watu ambao kwa sababu zisizojulikana watu hao wamejishusha utu wao na kuwa karibu na wanyama?

Watu wamewakabidhi utu wao kwa viongozi wafanye wanachotaka.

Ndiyo maana hao viongozi hawastuki.
 
Imebainika watu wa Tanzania,wanaongozwa kama mbuzi,yaani ni kama walking corpse.
 
Huyu na mwenzake warioba, toka watolewe kwenye system na mzee Ruksa, hawajawahi kusamehe😄🙆‍♀️
 
Akizungumzia haki na uhuru wa watu kuzungumza, Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amesema viongozi wanatakiwa kuthamini utu wa watu, hivyo wana haki ya kulinda uhuru na haki ya kila mtu.

“Kwangu mimi viongozi anatakiwa kutamba kuwa anaongoza watu na siyo Mbuzi, Ng’ombe au kuku,” anasema Butiku na kuongeza kuwa kiongozi ambaye natambui hilo basi huyo si kiongozi.

Amesema “Lazima wakumbuke wanaongoza watu wanaopenda utu, unaweza kulewa kidogo madaraka ukasahau kama unaongoza watu, lakini pia hata wananchi nao wanaweza kuwa na tabia mbaya kama wanamchagua kiongozi na kisha hawamsikilizi.

Chanzo: ITV
Ni ujinga kuomba huruma ya viongozi
Na jambo hilo ndiyo linafanya wazidi kujiona miungu watu
Huyo Butuku bora tu angenyamaza
 
Definitely alichosema Bashiru ni ukweli, kweli mtupu, LAKINI yeye katika historia ya Tanzania, ndiye amekuwa mtu katili , muuaji, mfungaji watu, mbambikia makosa/kesi watu akitimiza maagizo ya Magufuli. Alimuona magufuli kama Mungu na alimpamba kama wa sasa wanavyompmba Samia anayewawezesha kupata mlo wao.
Alienda mbali zaidi mpk kubaka haki ya kuchagua na kuchaguliwa akasema "ccm itatumia dola kusalia madarakani". Mpuuzi sana huyu Bashiru.
 
Akizungumzia haki na uhuru wa watu kuzungumza, Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amesema viongozi wanatakiwa kuthamini utu wa watu, hivyo wana haki ya kulinda uhuru na haki ya kila mtu.

“Kwangu mimi viongozi anatakiwa kutamba kuwa anaongoza watu na siyo Mbuzi, Ng’ombe au kuku,” anasema Butiku na kuongeza kuwa kiongozi ambaye natambui hilo basi huyo si kiongozi.

Amesema “Lazima wakumbuke wanaongoza watu wanaopenda utu, unaweza kulewa kidogo madaraka ukasahau kama unaongoza watu, lakini pia hata wananchi nao wanaweza kuwa na tabia mbaya kama wanamchagua kiongozi na kisha hawamsikilizi.

Chanzo: ITV
Hiv lile jengo Lao wameshakamilisha?
 
Back
Top Bottom