Sijaelewa, Butiku anamuunga mkono Bashiru, pia Mzee Warioba anamuunga mkono Bashiru, ndio kusema Bashiru ana hao wazee na genge lake wako nae..
Ila wanasiasa sio watu kabisa, juzi kati hapa wakati wa Jiwe, huyo Bashiru alikuwa ni Mungu mtu yaani, alikuwa anajua watu wanauliwa, wanapotea, wanafilisiwa mali zao, wanateswa vibaya na kikosi kazi maalum, hakuna uhuru wa mawazo au kuongea ila Bashiru alikuwa kimyaaaa, aliona mambo sawa kabisa, nchi ilifikia sehemu ya hatari sana, kupotezwa ilikuwa dakika tu, ila Bashiru alikuwa haoni, sbb ya upigaji, anakula asali na kulalia asali..
Bashiru leo katoka kwenye inner circle ya asali, kaanza kupiga kelele bila aibu kumkashifu Mama Samia, yaani mm ningekuwa ndio Mh. Rais Samia, namfuta ubunge wa kuteuliwa haraka na arudi chuoni akafundishe ashike adabu..
Bashiru sio mtu, hafadhiliki, mnafiki sana.