Butiku: Viongozi watambue wanaongoza watu siyo kuku au mbuzi

Butiku: Viongozi watambue wanaongoza watu siyo kuku au mbuzi

Dr.Bashiru ni mbunge nashangaa unaandika anakosa mlo, hakuna kitu kama hicho.

Dr. Bashiru ameongea pointi ya msingi sana, na hata kama aliwajaza ujinga wakati ule, kama wakati huu anawaambia ujinga aliowajaza haufai muuache, lakini kuendelea kukomalia ule ujinga naona ndio ujinga zaidi.
Alichoongea Bashiru ni kitu sahihi na ni cha wazi kabisa kimantiki. Ni common sense kwa binadamu wenye akili. Hakihitaji mjadala; sio “hoja” ya kujadiliwa. Ni kama kumdai mtu akupe hoja za umuhimu wa vitamin C mwilini.

Sasa tunapomsikiliza binadamu akitoa common sense au hata ujinga kuna mengine muhimu ya kuangalia kuhusu huyo mtu. Nayo ni “credibility” (kuaminika) na “integrity” (uadilifu) wake. Bashiru mwanaharakati alisaidia sana kuonyesha ubovu wa siasa na mifumo yetu ya uongozi nchini na umuhimu wa katiba mpya.

Kwenye utawala wa awamu ya tano akashiriki kuikana hoja ya katiba mpya na kujiunga na waimba sifa na watukuzaji wa Rais wa wakati huo kwa kila jambo hata lihusishe utawala mbovu na ukiukwaji wa haki za binadamu. He lost his presumed credibility and integrity.

Leo anatuletea habari ambayo wote wenye akili tunaijua miaka nenda miaka rudi kuwa ni common sense kwamba ni “ujinga kutukuza viongozi tuliowachagua”, halafu mnatuambia tujadili “hoja ya Bashiru”? Yeye ndio anatakiwa ajipime amesimamia wapi! Alishapoteza credibility yake. Ni sahihi yeye kuwa somo (subject) la kujadiliwa - kwa kuwa kigeugeu kiasi hicho. Hatuwezi kupoteza muda kujadili common sense eti kuiita hoja!

Akitaka kutiliwa maanani kwa mambo ya maana kwanza atuthibitishie kuwa alipotoka awamu ya 5, kwamba ameuona upungufu wake na kuamua kurejea kwenye ukweli, atuombe radhi na kujiunga na mapambano dhidi ya utawala mbovu kikamilifu. Arejee msimamo wake kuhusu haja ya katiba mpya.
 
Akizungumzia haki na uhuru wa watu kuzungumza, Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amesema viongozi wanatakiwa kuthamini utu wa watu, hivyo wana haki ya kulinda uhuru na haki ya kila mtu.

“Kwangu mimi viongozi anatakiwa kutamba kuwa anaongoza watu na siyo Mbuzi, Ng’ombe au kuku,” anasema Butiku na kuongeza kuwa kiongozi ambaye natambui hilo basi huyo si kiongozi.

Amesema “Lazima wakumbuke wanaongoza watu wanaopenda utu, unaweza kulewa kidogo madaraka ukasahau kama unaongoza watu, lakini pia hata wananchi nao wanaweza kuwa na tabia mbaya kama wanamchagua kiongozi na kisha hawamsikilizi.


Chanzo: ITV
Repoters Chanzi TV wamekosea sana. Butiku ambaye amestaafu sio Mkurugenzi tena wa hii Taasisi bali ni Mwenyekiti wa Bodi. Nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Salim Ahmed Salim ambaye kwa sasa anaumwa.
 
Kuna mijitu mipunbafu eti Mama Samia Hana uwezo wa kuongoza. Sasa nchi miaka 60 nimaskini hao waliokuwa wanatawala walikuwa na uwezo gan? Acheni ujinga muache mama afanyekazi wenye akili tunaona Mambo makubwa anayofanya. Msitake chuki zenu binafisi kwa mama mtuhusishe na sisi. Na mama tunae Mungu akijalia mpaka2030
Sie watanganyika tunataka rais Sio Mama hayo Mambo yakuitana Mama pelekeni huko nyumbani kwenu,eti Mama,mambo ya kutafuta uruma,hizo uruma za kuitana Mama perekeni Zanzibar yenye watu million 2.
 
Hao vikaragosi hawana uwezo wa kujibu hoja za Bashiru wamebakia kupuyanga tu kama bawana vichwa! Ni wapuuzi sana hawa! Sasa Butiku anawachana chana mabwege hawa!
Mkuu bashiru kasemaje? Naomba video
 
Uko sahihi kwa asilimia 100. Bashiru ni mnafiki hata kama ameongea ukweli. Lakini yeye ndio muasisi wa watu kuzuiwa kutoa maoni yao. Chini ya utawala wa kina Bashiru wetu ndio walikuwa wakitekwa, na chaguzi za nchi hii kunajisiwa.
Ninani alizuiwa kutoa maoni?weka ushaidi wa video Bashiru akizuia watu wasikosoe utawala wao,akina Bashe na Nape walikuwa wanakosoa mchana kutwa,mpaka mwenyewe Bashiru akaulizwa kuhusu kauli za Bashe na Nape wala hakujibu vibaya, mpaka Bashe alipewa unaibu Waziri wa kilimo,kwa ukosoaji wake, mpaka Magufuli wakati wa kumwapisha akamwambia hayo uliyokuwa unayakosoa nenda kayafanye, Makamba na Nape Kinana, Ngereja Zitto, walikuwa wanatukana,mbona hatukuwahi kusikia wakitekwa? acheni siasa za kishamba, mnadai Samia karudisha democrasia kwenye chama watu wanatoa maoni yao bila wasiwasi, wakati watu wakisema wanashambuliwa.
 
Tatizo lilipoanzia.
 

Attachments

  • y2mate.com - JPM Nilipotaka kumteua Dkt Bashiru niliambiwa ni CUF na wana CCM_v240P.mp4
    2.6 MB
UKWELI usemwe tu,

Msema UKWELI huo yawezakuwa ameamua kubadilika na kuingia njia sahihi.

Apokelewe Kwa UKWELI wake, alilewa Madaraka enzi zile, Pombe imekata nw.😃😃

Sijawahi kumuamini mnafiki yoyote toka CCM hata aongee ukweli gani, hasa anapokuwa nje ya mlo.
 
Sijawahi kumuamini mnafiki yoyote toka CCM hata aongee ukweli gani, hasa anapokuwa nje ya mlo.
Bt Pana waadilifu wengi tu ndani ya CCM, ingawa ni Wachache ukilinganisha na waliopotoka.

Wasiwekwe wote kapu moja.
 
Sijawahi kumuamini mnafiki yoyote toka CCM hata aongee ukweli gani, hasa anapokuwa nje ya mlo.
Wale waliokula billions 10 za Lowassa ndio wa kuaminiwa?, chadomo na wewe ni [emoji706][emoji706][emoji706][emoji706]
 
Akizungumzia haki na uhuru wa watu kuzungumza, Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amesema viongozi wanatakiwa kuthamini utu wa watu, hivyo wana haki ya kulinda uhuru na haki ya kila mtu.

“Kwangu mimi viongozi anatakiwa kutamba kuwa anaongoza watu na siyo Mbuzi, Ng’ombe au kuku,” anasema Butiku na kuongeza kuwa kiongozi ambaye natambui hilo basi huyo si kiongozi.

Amesema “Lazima wakumbuke wanaongoza watu wanaopenda utu, unaweza kulewa kidogo madaraka ukasahau kama unaongoza watu, lakini pia hata wananchi nao wanaweza kuwa na tabia mbaya kama wanamchagua kiongozi na kisha hawamsikilizi.


Chanzo: ITV
Wacha waumane tu
 
You might be very right. It seems bashiru ana kundi kubwa nyuma yake maana hawa wazee akina Butiku, Warioba unaona kabisa wanamtetea. Na akina Butiku na warioba, wana kundi lao...ambalo it seems liko against Samia

Definitely alichosema Bashiru ni ukweli, kweli mtupu, LAKINI yeye katika historia ya Tanzania, ndiye amekuwa mtu katili , muuaji, mfungaji watu, mbambikia makosa/kesi watu akitimiza maagizo ya Magufuli. Alimuona magufuli kama Mungu na alimpamba kama wa sasa wanavyompmba Samia anayewawezesha kupata mlo wao.

Likewise, Bashiru alimuabudu magufuli kwa vile alikuwa anapata mkate wake toka kwa Magufuli. Kwahiyo ni mnafiki, siyo kuwa anawaonea huruma wakulima, bali ni kwa vile amekosa mlo aliokuwa anaupata toka kwa Magufduli.
Acha kuweweseka!

Bashiru bado anapata hela nyingi toka selikalini
 
Samia ni dhaifu, kwasababu kama ana wateule wasiojielewa kwanini asiwaondoe?

Nyie waimba mapambio ndio mnazidi kumuharibu Samia, mwambieni ukweli abadilike, sio kumficha azidi kuwa mjinga.
Kwanza, Mhe. Rais ameingiaje hapa? Umemtaja pasipo na sababu. Pili, tumia maneno ya heshima unapomtaja Mhe. Rais. Huyu ni mkuu wa nchi.🙏🙏🙏
 
Ataongeaje hayo wakati yuko kwenye utekelezaji nawe tumia akili kidogo
Kwa hiyo ukiwa kwenye utekelezaji (ulaji) hutakiwi kuongea! Ila ukiwa nje ya huo utekelezaji, ndiyo unatakiwa sasa kuongea! Ok.
 
Raisi Samia ruhusu mikutano ya siasa watu wapate pa kupumulia. Usipofanya hivyo, yale yale yaliyompata bwana yule hayako mbali pua.

Ni hatari sana kutengeneza upinzani wa ndani ya chama kuliko nje ya chama. Kwa chama tawala, vyama vya upinzani husaidia kuleta uzani na uwiano wa kiutawala.

Kuendelea kuvibinya ni kuendelea kujibinya mwenyewe. Magu aliko anajua hilo.



Sahihi kabisa.
 
Back
Top Bottom