Butiku: Viongozi watambue wanaongoza watu siyo kuku au mbuzi

Butiku: Viongozi watambue wanaongoza watu siyo kuku au mbuzi

Ibanga unatia huruma sana na bado hadi 2025 tutawapiga kama ngoma. Na wote mmewaua mkawabakisha waswahili wenzenu, hii damu itamfata JK hadi kaburini
 
Ninani alizuiwa kutoa maoni?weka ushaidi wa video Bashiru akizuia watu wasikosoe utawala wao,akina Bashe na Nape walikuwa wanakosoa mchana kutwa,mpaka mwenyewe Bashiru akaulizwa kuhusu kauli za Bashe na Nape wala hakujibu vibaya, mpaka Bashe alipewa unaibu Waziri wa kilimo,kwa ukosoaji wake, mpaka Magufuli wakati wa kumwapisha akamwambia hayo uliyokuwa unayakosoa nenda kayafanye, Makamba na Nape Kinana, Ngereja Zitto, walikuwa wanatukana,mbona hatukuwahi kusikia wakitekwa? acheni siasa za kishamba, mnadai Samia karudisha democrasia kwenye chama watu wanatoa maoni yao bila wasiwasi, wakati watu wakisema wanashambuliwa.

Huyo Nape si alitolewa hadi bastola hadharani? Kinana, Nape, Makamba si ndio hao walienda kuomba msamaha kama wanawake? Zito si alitishiwa hadi kifo, au unadhani ukipaniki ndio ukweli tutasahau? Wakati Magufuli anamuagiza Ndugai awatoe wapinzani bungeni kisha atadeal nao huku ulikuwa hujaja mjini nini?
 
Huyo Nape si alitolewa hadi bastola hadharani? Kinana, Nape, Makamba si ndio hao walienda kuomba msamaha kama wanawake? Zito si alitishiwa hadi kifo, au unadhani ukipaniki ndio ukweli tutasahau? Wakati Magufuli anamuagiza Ndugai awatoe wapinzani bungeni kisha atadeal nao huku ulikuwa hujaja mjini nini?
Niambie aliyekosoa akavuliwa ubunge au kuitwa kamati kuu, Magufuli alikuwa anakataa matusi ndio maana Wabunge walikuwa wakifika bungeni baada ya kujenga hoja ili kusaidia selikali wanaanza kuporomosha matusi kwasababu ya kinga ya bunge, ndio Maana Magufuli alivyoona bunge limekuwa kichaka cha kuporomosha matusi, akamwambia Ndugai hawe anawatoa nje iliwakitukana wakiwa nje wakumbane na mkono wa sheria,nakumbia tena Bashe alipata uwaziri kwasababu ya ukosoaji wake.
 
Niambie aliyekosoa akavuliwa ubunge au kuitwa kamati kuu, Magufuli alikuwa anakataa matusi ndio maana Wabunge walikuwa wakifika bungeni baada ya kujenga hoja ili kusaidia selikali wanaanza kuporomosha matusi kwasababu ya kinga ya bunge, ndio Maana Magufuli alivyoona bunge limekuwa kichaka cha kuporomosha matusi, akamwambia Ndugai hawe anawatoa nje iliwakitukana wakiwa nje wakumbane na mkono wa sheria,nakumbia tena Bashe alipata uwaziri kwasababu ya ukosoaji wake.

Magufuli alikuwa anakataa matusi kisha akawaambia watu wabaki na mavi yao nyumbani! Bunge linaendeshwa na kanuni na sio mapenzi ya rais.
 
Sasa mtu kama hautaki
Magufuli alikuwa anakataa matusi kisha akawaambia watu wabaki na mavi yao nyumbani! Bunge linaendeshwa na kanuni na sio mapenzi ya rais.
Sasa kama hautaki kulipa 200 za uduma ya choo ili watu walipwe wa kufanya usafi,sinibora ubaki na mavi yako, Wewe stendi ya Mbezi ulitaka abiria wote wale wanisanidie bure?
 
Sasa mtu kama hautaki

Sasa kama hautaki kulipa 200 za uduma ya choo ili watu walipwe wa kufanya usafi,sinibora ubaki na mavi yako, Wewe stendi ya Mbezi ulitaka abiria wote wale wanisanidie bure?

Kwahiyo hiyo ni lugha ya kutumiwa na rais unayesema alikuwa hataki matusi?
 
Comrade Bashiru Ally Kakurwa Hatimaye Wamekuja Wenyewe Waliosema Mwembe Unaalika Maua
 
You might be very right. It seems bashiru ana kundi kubwa nyuma yake maana hawa wazee akina Butiku, Warioba unaona kabisa wanamtetea. Na akina Butiku na warioba, wana kundi lao...ambalo it seems liko against Samia

Definitely alichosema Bashiru ni ukweli, kweli mtupu, LAKINI yeye katika historia ya Tanzania, ndiye amekuwa mtu katili , muuaji, mfungaji watu, mbambikia makosa/kesi watu akitimiza maagizo ya Magufuli. Alimuona magufuli kama Mungu na alimpamba kama wa sasa wanavyompmba Samia anayewawezesha kupata mlo wao.

Likewise, Bashiru alimuabudu magufuli kwa vile alikuwa anapata mkate wake toka kwa Magufuli. Kwahiyo ni mnafiki, siyo kuwa anawaonea huruma wakulima, bali ni kwa vile amekosa mlo aliokuwa anaupata toka kwa Magufduli.
Samahani mkuu, kwa nia ya kufunzana na kuweka rekodi sawa naomba tafadhali sana unielezee kwa mifano na vielelezo ukatili, uuaji, ubambikiaji na ufungaji watu wa bashiru ally
 
jambo la msingi kukumbuka siku zote, tusijefanya makosa kuwaamini sana viongozi kama tulivyofanya kwa mwendazake, tukaambulia mabua. hili kosa halitakiwi kujirudia, hatakiwi kiongozi anayeishi kwa kodi zetu awe mungumtu, hilo litakuwa kosa kubwa sana. anatakiwa kukosolewa na kuwajibika kwa wananchi.
 
Hao wote awana hoja kipindi wenzao walipokuwa wanaongea waliwaona wanawashwa washwa sasa ni zamu yao tutaona nani anajikuna
Haimzuii na ni haki yake kusema kile anachojisikia kusema isipokuwa ajavunja sheria.

Kwani huyu wa sita alikuwa wapi wakati huo? Kwanini akujiuzuru
 
Ibanga unatia huruma sana na bado hadi 2025 tutawapiga kama ngoma. Na wote mmewaua mkawabakisha waswahili wenzenu, hii damu itamfata JK hadi kaburini
Unatia huruma wewe sijui mhaya gani unakuwa na uelewa Mdogo. Mimi huwa sipelekeshwi na mihemuko ya watu. Mungu kanipa akili ya kungamua Mambo kabla ya kutoa uamuzi au kumlaumu mtu. Mimi Samia anapofanya vizuri na sema anapo fanya vibaya nasema . Lakini Kuna watu wao raisi Hana alifanyalo jema wakalikubali wao kutwa kucha nikulaumu tuuu.
 
DKT. BASHIRU: KATIBU MKUU MSTAAFU WA CCM 'ANAYEFUKIWA' AKIWA ANGALI HAI!

Wakati ninawekwa kizuizini na Jeshi la Polisi kwa ajili ya kuhamasisha katiba mpya tarehe 15 Februari 2021, Dkt. Bashiru alikuwa ndiye Katibu Mkuu Kiongozi na pia Katibu Mkuu wa CCM. Ukiachia Rais Magufuli, Dkt. Bashiru ndiye aliyekuwa mtu mwenye nguvu kubwa ndani ya CCM na Serikali yake pengine kuliko mtu mwingine ye yote yule.

Mnakumbuka msafara wake mrefu wa magari yale ya kijani pamoja na kikosi cha kumlinda? Je, mnajua kuwa pamoja na makeke yake, hata yule Kiranja Mkuu wa Wakuu wa Mikoa enzi hizo ambaye alitamka kuwa hata mkuu wa mawaziri alikuwa anamheshimu, lakini na yeye alikuwa anamuogopa Dkt. Bashiru? Rejea pia hotuba za viongozi katika ibada ya maziko ya Dkt. Mengi kule Kilimanjaro jinsi ambavyo Kiranja Mkuu alivyonywea mbele ya Bashiru.

Wakati mwanaharakati huru, Cyprian Musiba akiwanyanyasa watu wazima akiwemo Membe, Makamba na Kinana; Dkt. Bashiru hakuwahi kusikika akimkemea Musiba. Ritorikia ya Dkt. Bashiru wakati ule ilikuwa ni kuwa wanatumia Dola kubaki Madarakani. Alijua fika kuwa hata akina Musiba, Makonda na Sabaya walikuwa wanatumia Dola iliyokuwa chini ya CCM ya Dkt. Bashiru ili kunyamazisha sauti huru.

Kama kitendo cha kumsengenya kwa siri Rais Magufuli kiliwafikisha akina Kinana, Membe na Makamba Snr mbele ya Kamati ya Maadili ya CCM na baadaye kujadiliwa na Kamati Kuu na hatimaye Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM kuhitimisha jambo hilo, itakuwaje kwa Dkt. Bashiru ambaye amesemea akiwa juu ya paa la nyumba iliyo katikati ya mji mchana kweupe?

CCM ya Bashiru haikuwahi kuwavumilia watu waliokuwa na maoni mbadala iwe nje au ndani ya CCM na Serikali. Unakumbuka kauli ya RC Ali Hapi aliposema wazee wastaafu wafunge midomo yao? Je, Dkt. Bashiru aliwahi kuingilia kati na kusema watu waachwe watoe maoni yao? Wakati Mdude Nyagali anaozea magereza kwa kumsema Rais Magufuli, uliwahi kumsikia Dkt. Bashiru akisema aachwe atoe maoni?

Sasa naye Dkt. Bashiru ambaye ni Katibu Mkuu wa CCM mstaafu na Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu ametoka hadharani na kutoa maoni yake yaliyo huru. Tayari ameaanza kuandamwa kutoka ndani ya CCM na ndani ya Serikali. Watu wale wale waliokuwa chini yake wanapoka haki ya Dkt. Bashiru ya kutoa maoni yake. Kibo!

Sisi Askofu Mwamakula tumejitosa kumtetea na kumpazia sauti ili aachwe atoe maoni yake. Katika hili tumeungana na Mzee Jaji Joseph Sinde Warioba, Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais mstaafu. Hebu Mwambieni Dkt. Bashiru kuwa Askofu Mwamakula atatetea uhuru wake wa kutoa maoni hadi mwisho!

Waambieni na hao wanaharakati wa vyama vya upinzani kuwa wasitufokee sisi Askofu pale tunapomtetea Dkt. Bashiru. Wakumbuke kuwa huko nyuma tulisema kuwa utakuja wakati ule ambapo watesi watageuka kuwa wateswaji. Tulisema kuwa sisi wajibu wetu ni kuwatetea wanaoteswa bila kujali rangi za vyama vyao. Kwa hiyo, tunamtetea Dkt. Bashiru ambaye jana alikalia kiti chenye utukufu wakati vijana 'bakundwe' wakimmiminia lisasi korija kadhaa Tundu Lissu na kuwanyanyasa akina Kinana.

Hebu tulia kwanza, ninaota wakati sijalala! Loo! Ndoto hii inasema kuwa mwakani na baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2025, Iziraeli wa mateso atawageukia vigogo wengine walioko Serikalini na ndani ya CCM. Ndoto hii inamuonyesha mtu mmoja kutoka Kibosho akiomba kwa Mungu ili aniweke hai kusudi nije kuwatetea watu hao. Ndoto imekatika ghafla na sijui tafsiri yake.

Halafu na ninyi watu wa Usagara! Ole wenu kama mtamdhuru Cyprian Musiba! Hamjui kuwa Mungu alikataza mtu ye yote kumzuru Kaini? Kwani yuko wapi Musiba sasa hivi? Ngoja tumtafute aliko Kangi Lugola atueleze aliko Musiba! Ndio! Hawa wawili ni majirani kule Mwibara, Mara.

Waambieni wale waimba kwaya kuwa kama mtunzi wa nyimbo anaweza kutemewa mate, je itakuwaje kwa mwimba kwaya wa kawaida? Acheni ujinga, unganeni na sisi kudai Katiba Mpya. Katiba Mpya ingelikuwepo sasa, baadhi ya vijana wa UVCCM na baadhi ya Wabunge na makada wa CCM wasingeanza kumdhalilisha Katibu Mkuu wa CCM mstaafu na Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu na Mbunge! Mtamfukiaje Dkt. Bashiru akiwa angali hai? Umbwenelehi?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
 
Kwangu mimi kiongozi anatakiwa kutamba kuwa anaongoza watu na siyo Mbuzi, Ng’ombe au kuku
Awamu iliyopita vilikuwa vime mute.
By the way havina impact yoyote
hivyo vizee viywa gongo (Warioba na Butiku)
 
Back
Top Bottom