Bwana Tundu Lissu, Hoja ya Chato na Maendeleo ya sasa inajibika Kimantiki

Mbona ukiwa Chato ,Bukoba ni karibu lakini kuna uwanja wa ndege. Hujui uwanja wa ndege wa Chato unafaida nyingi ikiwa na matumizi ya dharula kama uwanja wa Mwanza kuna Tatizo.

Usipende kupinga kila jambo, akitoka madarakani mtakuja Chato kung'oa runway?

Kwani akitoka madarakani huu uwanja hautawanufaisha watanzania?
 
Sijui Kama Huyu Mara
Kwa kuwa Mwanza kuna uwanja ndio Geita usijengwe uwanja? Unajua umbali wa Chato to Mwanza

Mimi sitetei, sioni sababu za msingi kunishawishi kupinga Chato kuwa na uwanja.
Siyo lazima wakubwa na watu wenye akili timamu wanapochangia na wewe uandike,
GEITA na CHATO hupajui na hutakaa upajue,
Tatizo huna majukumu,waulize wazazi wako wanavyo kuhangaikia kukutafutia mlo wa siku ,ndipo utapata jibu.
 
....... watu walio karibu na magufuli.....

 
Mradi gani ambao haupo Chato, na kwa Umuhimu wa mji wa Chato unapendekeza Ujengwe Chato!?
 
Sijui Kama Huyu Mara

Siyo lazima wakubwa na watu wenye akili timamu wanapochangia na wewe uandike,
GEITA na CHATO hupajui na hutakaa upajue,
Tatizo huna majukumu,waulize wazazi wako wanavyo kuhangaikia kukutafutia mlo wa siku ,ndipo utapata jibu.
Naomba namba ya simu ya mama yako.
 

Nianze na methali isemayo..." siri ya mutungi aijuaye ni kata..."
Bwana Deo Mutungi usitake kutufanya Watz wote hatuna akili please. We kweli ni mutungi wa maji na kata ndo inayokujulia.....!!!!

Wakti wa propaganda za kijinga, kipuuxi na kisiasa zilishapitwa na wakti bwana Mutungi. Nchi hii inaongozwa kulingana na KATIBA NA SHERIA za nchi ya JMT.
Huwezi kunambia ati kila Utawala na mambo yake.....this is a BIG NO. Rais yeyote anayeingia Ikulu anaapa kulinda na kutetea Katiba ya JMT.

Marais wa Awamu zote 1-4 walifuata Katiba ya JMT ndo maana hawakufanya huu upuuxi anaofanya Magufuli katika awamu hii!! Mwl. Nyerere Baba wa Taifa hakuwahi kujenga Uwanja wa Ndege Kimataifa si Mwitongo- Butyama wala Mwisenge- Musoma.....!!!! Nyerere alikataa hata kujengewa nyumba ya Kifahari pale Mwitongo akihoji yeye hakuwa Tembo.....!!! Hii ni hikma na busara ya hali ya juu kwa maana ya kutaka Fedha yote ya Walipa KODI IKAFANYE KAZI YA MAENDELEO YA WATU na siyo KUNUFAISHA MTU MMOJA NYUMBANI KWAKE KAMA ANAVOFANYA MAGUFULI PALE CHATO.....!??

Hivi Magufuli ana tofauti gani na Mobutu Seseseko Kuku Wazabanga?? Kujenga Chatto uwanja wa ndege wa Kimataifa na Majumba ya kifahari kuna tofauti gani na kijjii alichojennga Mobutu Seseseko pale Badolite nchini Zaire au Nkandla ya Jacob Xuma wa Sauz.....it's all the same!! Nataka nkuhakikishie kwamba siku Magufuli akiachia Madaraka na wakaja Wazalendo Halisi kuiongoza nji hii basi Jiwe atakuwa na kesi ya kujibu Mahakamani kwa Ufisadi wa kujilimbikixia mali na kujinufaisha yeye binafsi na familia yake pale Chatto. Mbona ni swala la muda tu!!
 
Rais angechagua watu wenye akili timamu wa kumtetea na kutengeneza propaganda, tena ikibidi wapigwe darasa kali sana la kutetea na kueneza propaganda. Sasa huyu ametetea nini hapa? Hakuna utofauti wa anachokifanya Uncle magu na hao madictator wengine labda utofauti wa nyakati na muda walioutumia kuyatekeleza matakwa yao.

Najiuliza hivi hakuna wenye akili huko au haya mambo hayana utetezi kiasi kila mtu anajikanyaga kanyaga tu.
 
Hoja hujibiwa kwa hoja. Tueleze mantiki ya kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa Chato iliyo km chini ya 300 toka Mwanza ukaacha Mtwara ama Songea ama Kigoma? Kuna mantiki gani kujenga uwanja wa mpira mkubwa Chato ukaacha Bukoba ama Tabora ama Songea. Hivi kweli ni sawa kweli kuweka taa za barabarani Chato wakati hata Geita hamna. Kwa watu wenyewe wa Chato je isingekuwa bora kwao kama badala ya kutumia mabilioni yote hayo kuifanya Chato ionekani ya kisasa akawapendelea kuwasambazia maji vijiji vyote?9
 
Nakubaliana na wewe kabisa. Hoja kubwa ni kuwa hayo yanayofanyika huko yana uwiano na yanayofanyika kwingineko hapa Tanzania? Chato ni makazi binafsi ya rais ambaye kwa nafasi yake halazimiki kwenda kujengea makazi ya hadhi ya rais kwasababu ana ikulu.

Baada ya kumaliza kujenga nyumba yake yenye hadhi ya rais na uwanja wa ndege anaendelea kujenga vitu vingine ambavyo sasa naona kwamba siyo kwa ajili yake bali kwa ajili ya wananchi wote. Hata kama tutamsamehe kwa hayo ya kwake binafsi, hayo mengine yanayofanyika kwa ajili ya wananchi wote ndiyo hasa yanayopaswa kuhojiwa katika mipango ya taifa na yanapitishwa na bunge bila ushawishi wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…